May 25, 2017
Sababu Sita (6) Ni Kwanini Unatakiwa Kuacha Kutumia Sukari Kwa Wingi.
Kwa sasa vipo vyakula vingi
sana ambavyo vimekuwa na sukari na tunavitumia karibu kila siku. Kwa bahati
mbaya au nzuri vyakula hivi vya sukari vimekuwa vikipendwa na wengi bila ya
kujali madhara yake kiafya yakoje.
Wengi wetu hatujui sana
kiundani hasa pale tunapotumia vyakula vingi vya sukari, ni madhara gani ambao
yanaweza kukutokea zaidi, tumekuwa tukijua juu juu tu kwamba ukila vyakula vya
sukari vinaweza kukuletea shida hii au ile bila kuwa na uhakika sana.
Kwa sababu hiyo ndani ya
makala haya ya afya, tutakueleza kinagaubaga sababu ya msingi ni kwa nini
unatakiwa uache kutumia sukari kwa wingi mwilini mwako na ikiwezekana kuacha
kabisa baadhi ya matumizi ya vitu vyenye sukari nyingi sana.
1.
Sukari nyingi mwilini ni kisababishi cha magonjwa.
Matumizi ya sukari kwa wingi
ni chanzo kimojawapo cha kuongezeka kwa uzito, lakini si hivyo tu sukari
inapokuwa nyingi mwilini inaweza kukupelekea kupata magonjwa kama vile
magonyjwa ya moyo na kuongezeka kwa shinikizo la damu jambo ambalo ni hatari
kwa afya yako kwa kiasi kikubwa.
2.
Sukari nyingi mwilini inapunguza uwezo wa kuona.
Mara nyingi wanaoutumia
sukari kwa wingi sana au wale amabao viwango vya sukari vimeongezeka mwilini
mwao, moja ya madhara yake kwa baadae ni
kutokuona vizuri. Hilo hutokea kwa sababu, sukari inapokuwa nyingi hupelekea lensi ya
jicho kuongezeka na matokeo yake matatizo ya macho huanza kujitokeza kwa
mhusika.
Punguza matumizi ya sukari. |
3.
Sukari nyingi huozesha meno.
Bila shaka hili umeshawahi
kulisikia au kuliona. Na mara nyingi hutokea sana kwa watoto, meno huweza kuoza
baada ya matumizi ya sukari kwa wingi. Kinachotokea sukari huzalisha bakteria
wenye sumu ambapo hao huweza kuharibu meno na kupelekea kuweza kuoza kabisa.
4.
Sukari nyingi inapoteza uwezo wa mwili kukabiliana na magonjwa.
Wale wote ambao sukari
inakuwa imeongezeka miili yao inakuwa haina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Unajua
ni kwa nini? iko hivi,.. unapokuwa na sukari nyingi mwilini inatabia ya kuua
seli nyeupe ambazo husaidia kupambana na magonjwa. Kwa hali hiyo ndio maana
watu wenye visukari hawaponi vidonda kwa sababu kama hii.
5.
Sukari nyingi mwilini zinasababisha mwili kuonekana umeezeka.
Kila sukari inapokuwa nyingi
mwilini, inazalisha kemikali ambazo baadae kemikali hizo hupelekea mwili wako
kuanza kuoneana kama vile umezeeka. Hapa njia pekee ya kuondokana na hali hiyo
ni kupunguza matumizi ya sukari. Vinginevyo utaanza kuonekana kikongwe.
6.
Sukari nyingi husababisha viungo vya mwili kulegea.
Zipo ‘joints’ kama vile za miguu hasa pale unapokuwa unatembea zinakuwa zinachoka
upesi na kulegea kama mwili wako una sukari nyingi. Hali hii hutokea sana hasa
kwa wagonjwa wenye kisukari. Hii ninhali ambayo huwakuta wengi wagonjwa wa
kisukari na inakuwa ni hali inayosumbua.
Mwisho kabisa hapa sina shaka
mpaka unafika mwisho wa makala haya utakuwa umeelewa hatua za kuchukua na hiyo
haitoshi ni vyema ukamshirikisha na mwingine makala haya ili aweze kujifunza na
kundokana na matatizo ambayo pengine yangemkuta.
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0628
92 98 16,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.