May 29, 2017
Umuhimu Wa Kujiongeza Katika Maisha Ya Mafanikio.
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini
yetu mazima u mzima wa afya tele na unaendelea vyema katika harakati zako za
kuweza kulisukuma gurudumu hili la maendeleo.
Ni siku nyingine tulivu ambayo sina budi nikukaribishe kwa moyo mkunjufu
tuweze kujifunza kwa pamoja.
Siku
ya leo nataka ttuzungumzie namna ambayo una uwezo mwingine wa kutenda jambo
jingine ambalo linaweza kukupa mafanikio makubwa kwa upande wako tofati na hilo
ulitendalo sasa. Unajua nataka tuzungumzie hili kwa sababu wetu wengi
hawafahamu uwezo mwingine walionao, ambao unaweza kuutumia ili uweze
kukamilisha jambo jingine ambalo Mwenyezi mungu kakujalia kulitenda.
Watu
wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa
kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea
kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka
mipaka katika kitu hicho pekee.
Ongeza thamani ya biashara yako kila iitwapo leo. |
Ukweli
haipo hivyo hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi
ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya
kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi
kutengeneza ‘six park’ kwa kufanya
mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali unaweza kutengeza ‘six park’ kwa kufanya mazoezi ya aina
tofauti tofauti.
Kwa muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa
zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo
mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate
wako wa kila siku.
Hata
mwandishi mmoja aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get
what you always gotten” hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale
ambayo umekuwa ukifanya siku zote,
utapata yale yele ambayo siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena
aya hii ili uielewe vizuri.
Kwani
aya hiyo ipo wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi
matokeo yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya aina
tofauti na uliyoyazoea, unachotakiwa
kufanya ni kubomoa uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda
mambo yako ya msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako kwani binafsi naamini una kitu kingine cha
kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.
Mwisho
nimalizie makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako
ya msingi acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa
nyingine, bali unachotakiwa kufanya ni
kubomoa uzio huo ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani
pindi unavyoacha ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na
mwisho wa siku kuelekea jehenamu ya umasikini.
Narudia
kwa kusema tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya
umaskini. Usiogope na kusema afisa mipango anakutisha hapana, ila kazi yangu ni kukwambia ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi
uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni kuwaza ni namna gani utaweza kufika
mbali zaidi.
Kwani
umuhimu wa kujiongeza kunamsaidia mtu kuweza kuwa milango mingi ya kuweza
kufanikiwa zaidi. Pia faida nyingine ya kujiongeza humsaidia mtu kuweza kuwa mbunifu
zaidi kwa kile akifanyacho. Na ubunifu humsaidia mtu aweze kujilikana na
ukijulikana ndo mwanzo wa mafaniko yenyewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada
naomba kazi ibaki kuwa kwako kwa kuamua kwenda kuyatekeleza hayo ambayo nimekwambia. Asante.
Ni wako katika ujenzi wa mafaniko; afisa
mipango, Benson Chonya.
0757909942.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.