May 12, 2017
Mambo Manne (4) Ya Kimafanikio Ya Kumfundisha Mtoto Wako Mapema.
Msingi
mkubwa wa mafanikio ya mtu yeyote kitabia unatokana na malezi bora aliyopata
hasa akiwa mtoto kuanzia mwaka mmoja hadi miaka kumi na mbili. Katika kipindi
cha mwaka 1 hadi 12 ndio kipindi muhimu sana cha malezi.
Tabia
nyingi ambazo zinatengenezwa au kufundishwa katika kipindi hiki, huwa kuna uwezekano
mkubwa wa kudumu maishani mwako kote. Hapa hii inatokea bila kujali tabia hiyo
ni nzuri kwako au mbaya.
Kwa mfano,
kama ulikuwa unaendekeza uvivu au kama ulikuwa mtu wa kuchapa kazi sana na
kujiona huo ndio kama utamaduni katika kipindi cha mwaka 1 hadi 12, ni rahisi
tu tabia hizo kuendelea hadi ukubwani.
Kwa mantiki
hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kumfundisha mtoto wako mambo ya kimafanikio yatakayomsaidia
kwa baadae kwenye maisha yake. Mambo hayo
ni yepi? Karibu na twende pamoja tujifunze.
1.
Mfundishe, njia bora ya kufikiri.
Ikiwa
hupendi sana maisha yako yalivyokuwa mwanzoni yaendelee kwa kizazi chako, sasa
ni wakati wa kumfundisha mtoto wako namna bora ya kufikiri. Hapa ni lazima
umfanye mtoto wako aweze kufikiri chanya.
Unaweza
kumfanya moto wako afikiri chanya kwa kumpa vitabu vizuri chanya kama uwezo wa
kusoma anao au kwa maneno maneno unayomwambia. Hiyo haitoshi pia unaweza
ukamtafutia marafiki wazuri wenye mtazamo chanya.
Kama
mtoto wako unamlea kwa mtazamo chanya, kufikiri kwa njia bora itakuwa kwake ni
jambo ambalo halikwepeki. Anza leo kuweka mikakati yakumjengea mwanao njia bora
ya kufikiri itakayomsaidia hata kumjengea mtazamo chanya pia.
2. Mfundishe, kujitegemee mapema.
Kati
ya kitu kitakachofanya ujenge msingi imara kwa watoto wako kwa baadae ni kule
kufanya wajitegemee mapema. Hapa inatakiwa umfundishe mtoto wako kufanya baadhi
ya mambo mwenyewe.
Kwa mfano, anapokuwa mkubwa kidogo kama ni kufua mwache afue mwenyewe. Kama ni
kusaidia kazi fulani acha aifanye. Njia hii inakuwa bora kwa kujua kwamba kuna
vitu fulani anatakiwa awajibike.
Lakini
kama utakuwa ni mtu wa kumlea mtoto wako kwa kutaka kila kitu afanyiwe basi wewe ndiye utakuwa mtu wa
kwanza kumharibu mtoto wako. Mfanye mtoto wako ajitegemee mapema, itamsaidia
sana kwa baadae katika makuzi yake.
3.
Mfundishe, ajifunze kuchukua hatua mapema.
Siku zote vitendo ni bora
sana kuliko kusema. Kwa kuwa unajua umuhimu wa hili anza kumfundisha mtoto wako
juu ya umuhimu wa kuchukua hatua mapema katika maisha yake hata kwa vitu vidogo
ambavyo anavyofanya.
Kwa kumfundisha hivi unakuwa
unajenga utamaduni imara ambao utamfanya mtoto wako hata atakapokuwa mkubwa
atakuwa anajua na kutambua umuhimu wa kuchukua hatua mapema pia kwenye maisha
yake.
Ili hili lifanikiwe, mfundishe
kitu fulani halafu anza kufatilia utekelezaji. Unaweza ukamwacha hata maswali
kama kazi ya nyumbani, halafu uone atamaliza baada ya muda gani? Utakuwa
unafanya hivyo mara kwa mara ili kumfanya achukue hatua mapema zaidi.
4. Mfundishe ajue mambo yote huwa
hayaendi kama yalivyopangwa.
Katika
kumfundisha atambue kwamba mambo kuna wakati hayaendi kama yanavyopangwa,
subiri kipindi ambapo anataka kitu fulani tena kwa hamu kubwa. Inapofika katika
hicho kipindi kwa makusudi mnyime.
Najua
kama ilivyo kwa watoto walio wengi tabia zao atalia. Mwache alie halafu tafuta
siku ama muda akitulia, kama kile kitu kilikuwa cjha kununua, mnunulie na mpe somo
mapema atambue kuna wakati mambo hayaendi moja kwa moja kama uliyopanga.
Fanya
hivi kwa mtoto ambae ameshaanza kujitambua ikiwezekana kuanzia angalau darasa
la tano. Rudia tena na tena zoezi hili, mpaka ifike mahali ajue kwamba
mategemeo na uhalisia ni vitu viwili tofauti.
Yapo
mambo mengi unayoweza kumfundisha mwanao ya kumweka juu kimafanikio kwa baadae.
Unaweza kumfundisha mwanao pia jinsi ya kuishi na watu sahihi, uaminifu katika
maisha, misingi bora ya kuishi maisha ya kiroho napengine hata faida ya
kujiamini.
Fanyia
kazi haya machache kwa leo na chukua hatua katika kuweza kufikia mafanikio yako
makubwa.
Ni wako
rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713
04 80 35,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.