google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 2, 2017

Usirudishe Maisha Yako Nyuma Kwa Sababu Hii...

No comments :

Usikubali hata siku moja, kuyarudisha maisha yako nyuma, kwa sababu ya mawazo na matendo yako ya kila siku. Kila wakati unatakiwa uhakikishe mawazo yako na matendo yako viwe msaada mkubwa sana katika kukupeleka mbele kimafanikio.
Jaribu kujiuliza hapo hapo ulipo, mawazo na matendo yako ni msaada kwako? Ili kufanikiwa unatakiwa uwe na mawazo na matendo ya kukujenga kila siku na sio kukubomoa. Unatakiwa kujenga mawazo chanya na matendo chanya kila siku bila kukosa.
Kama vile ambavyo nyumba inajengwa kwa tofali moja juu ya lingine hadi kukamilika, halikadhalika mawazo na matendo yako nayo unatakiwa kuyajenga kwa utaratibu huo ili kujenga maisha yako. Wazo moja leo, ukiongeza na lingine wazo bora kesho, mwisho wa siku utafanikiwa.

Tatizo la wengi wanakwama na kushindwa kufanikiwa kwa sababu ya mawazo na matendo yao. Hakuna aliyekuloga hadi ukashindwa kufanikiwa wala hauna mkosi hadi ushindwe kufanikiwa. Kushindwa kwako kunaanzia kwenye MAWAZO YAKO NA MATENDO YAKO na si vinginevyo. Ukibadilika hapo, umefanikiwa.

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.