google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 28, 2017

Utaendelea Kubaki Na Maisha Haya Mpaka Lini?

No comments :
Kati ya kitu ambacho unatakiwa ujiulize sana ni hali ya maisha yako uliyonayo sasa. Je, maisha uliyonayo unayopenda au unaishi tu ilimradi siku ziende? Kama maisha uliyonayo kwa sasa huyapendi, swali lingine la msingi, jiulize utaendelea kuwa na maisha hayo mpaka lini?
Je, kuna hatua ambazo unachukua? Je, kuna mikakati ambayo unaiweka ambayo inaonyesha kweli umechoshwa na maisha hayo? Kuendelea kusema tu peke yake bila kuchukua hatua yoyote ya msingi huko nikujichosha wewe menyewe. Unatakiwa uamue mwisho wa ugumu wa maisha yako ni lini?
Hutaki kuamua, basi kaa kimya usiendelee kulalamika au kupiga kelele zisizo za msingi, tayari jibu ambalo tunakuwa nalo kichwani ni kwamba hayo maisha unayoyaishi kuna namna unavyoyapenda, ndio maana hutaki kuchukua hatua sahihi zitakazoweza kukusadia na kukutoa hapo ulipo.

Usitegemee kutakuwa na urahisi katika kutoka hapo ulipo. Mabadiliko yoyote yahitaji nguvu tena nguvu kubwa ili kuweza kubadilisha maisha yako na yakawa na tija. Lakini kama unataka kubadilisha maisha yako halafu ukaendelea kufanya mambo yale yale, hakuna utakachoweza kukibadili.
Kubali kujikana kwa muda kubadilisha kila kitu kwenye maisha yako. Kubali kubadilisha muda wa kufanya kazi, kubali kubadilisha marafiki na hata aina ya maisha unayoyaishi, kinyume cha hapo utaendelea kubaki na maisha hayohayo na ugumu uleule karibu kila siku.
Kila kitu kinawezekana na pia unaweza kubadilisha maisha yako ukiamua kuweka juhudi za lazima. Nini kinachoshindakana kwako? hutakiwi kuwa na maisha magumu wakati wote. Ni wakati wa kubadilisha maisha yako na kuyafanya kuwa bora, hilo litafanikiwa kwa kuchukua hatua na sio kwa kuishia kusoma makala haya tu.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.