Mar 14, 2018
Kufanikiwa Au Kushindwa Kunatengenezwa Sana Na Mambo Haya…
Mafanikio utayapata , kama utadhamiria kweli kuifanya dunia kuwa sehemu bora kuliko sasa, na kushindwa kutakuja kwako kama wewe utaiona dunia ni sehemu mbaya na tena iko kinyume na wewe, kwa hiyo hapa ni lazima utaweza kushindwa.
Mafanikio
yatakuja kwenye maisha yako kama utakuwa mtu wa kutafuta na kutengeneza
thamani. Kushindwa kunakuja kwenye maisha yako, kama unategemea dunia itakupa
kitu na utaishi kwa thamani zilizotengenezwa na watu wengine.
Mafanikio
yatakuja kwenye maisha yako kama utafungua milango ya kujifunza zaidi kutoka
kwa wengine na kwenye vitabu. Kushindwa kutaanza kukunyemelea hasa pale
inapofika wakati ukasema kwamba wewe unaweza kila kitu.
Mafanikio
yatakuja kwako, ikiwa utakuwa mtu wa kutazama chanya na kuangalia fursa
zinazokuzunguka. Kushindwa kutakuja kwako ikiwa tu, utakuwa mtu wa kutoa sababu
kila wakati na kushindwa kuangalia mambo ya kukusaidia.
Mafanikio
ni matokeo ya mawazo, mtazamo wako na juhudi unazoziweka kila siku katika
kuweza kufikia mafanikio. Na kushindwa pia ni matokeo ya mawazo, mtazamo na
juhudi zako. Iwe kushinda au kushindwa kunatokana sana na mambo hayo matatu.
Ukiona
mtu yeyote amefanikiwa maeneo matatu ambayo yana mchango mkubwa sana wa
kushindwa au kufanikiwa kwake ni hayo. Unachotakiwa kufanya ni kuyatumia maeneo
hayo ambayo ni mawazo, mtazamo na juhudi kwa vizuri.
Unaweza
ukajikuta kila mara unashindwa sana kwenye maisha yako kwa sababu ya kushindwa
kutumia mawazo yako vizuri. Unatakiwa kutumia mawazo yako kwa uhakika kufikiri
fursa na mambo ya kukusaidia kufanikiwa.
Pia unaweza
kila wakati ukiwa unashindwa kwa sababu ya kuwa na mtazamo ambao sio sahihi. Kile
ambacho wenzako wanaona kinawasaidia wewe huoni. Unapokuwa na mtazamo kama huu
ambao ni duni, kufanikiwa kwako kutakuwa ni shida sana.
Unaweza
pia ukajikuta ni mtu wa kushindwa, kwa sababu ya juhudi zako hazitoshelezi
kufika kule kwenye mafanikio sahihi. Unatakiwa uweke juhudi sahihi na kwa nguvu
zote katika kutengeneza mafanikio yako.
Ili kufanikiwa
unapaswa kujua na kulewa, mafanikio yako yanatengenezwa sana mambo haya matatu
ambayo ni mawazo, mtazamo na juhudi zako. Yafanyie kazi mambo haya matatu na
kisha utaona matokeo yake.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.