google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 23, 2015

Hivi Ndivyo Tunavyowaalika Watu Wabaya Katika Maisha Yetu.

No comments :
Nikupe siri moja? Kwamba, wataalamu hivi sasa wamegundua kwamba, asilimia 95 ya muda wote, ambapo sisi binadamu hutendewa ubaya na wengine, ni sisi ambao tunakuwa tumewaalika watu hao kututendea hivyo bila kujua.

Kila kitu tunachofanya, hasa vile vitendo ambavyo havihusishi kuzungumza, ni mwaliko kwa watu wanaotuzunguka . Kutabasamu kwa mfano ni mwaliko. Hii ni kama ilivyo kuweka ndita, kuonesha huzuni usoni, kuonesha hasira usoni au kuwa na uso wenye kuonesha dhati ya mambo muda wote. Hii yote ni mialiko pia.

Mtu anasimama vipi, anatembea na kukaa vipi, na yenyewe pia ni mialiko tosha, tofauti na tunavyofahamu sisi. Hebu siku moja ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu, jaribu kuwatazama watu hao mmoja mmoja na kujiuliza, kila mmoja kati yao anawaalika watu wengine kumtendea vipi. Halafu jiulize, watu hao wanatendewa kwa namna wanavyowaalika watu kuwatendea?Jibu kwa asililmia 95 litakuwa, ‘ndiyo’ kubwa kabisa.


Ukitaka kumwalika mtu akutendee ubaya, fanya kwa njia yenye kuvuta ubaya huo. Kukunja ndita kunafanya watu wengine kuogopa kuwa karibu nawe, hata kama huna nia mbaya nao. Kutabasamu huwakaribisha watu wenye kupenda urafiki kuwa karibu nawe. Lakini kwa kufanya kinyume na hapo, hivyo ndivyo utakavyozidi kuwaalika watu wabaya katika maisha yako.


Kubinua midomo kwa dharau huweza kuwaleta kwako watu ambao mtakwaruzana nao kwa sababu, tayari wamekuhukumu hata kabla hawajakufahamu. Aliyesaidia kuwafanya wakuhukumu ni wewe mwenyewe. Kwa hiyo, kama ni kuwaalika ni wewe mwenyewe unayefanya hivyo. Waalike wale ambao ni wema basi, badala ya kuwaalika watakaokuumiza kihisia.

Hebu tazama namna watu wanaotembea wakiwa wamejiinamia na wamejipinda wanavyoishi. Mara nyingi ukichunguza maisha yao utagundua kwamba, yana kuonewa na hofu, kutokujiamini na mashaka. Kutembea kwao kinaaonyesha kile kinachokwenda kwenye ma
wazo yao. Ni rahisi watu wa namna hii kuweza kuonewa tena na tena.


Kama hutaki kuishi kwa mashaka, ni lazima uwakimbie watu wanaoweza kukufanya uingie kwenye maisha ya mashaka. Huwezi kukimbia kama wewe mwenyewe unaishi kimashaka. Kama unataka maisha yasiyo na ushirikina ndani, ni lazima uwakimbie watu wanaohusudu ushirikina. Kwa kukimbia, ni wewe kutokuwa sehemu ya ushirikina wowote.

Kwa kuwa sasa unajua kwamba, mara nyingi kama siyo zote, sisi wenyewe ndiyo ambao tunaowaalika watu na kutufanyia ubaya au wema, ni uchaguzi wetu. Tunatakiwa kujiweka kwenye mazingira ambayo yatawavuta watu wema kwetu, kama tunataka amani. Kama tunataka shari, tunaweza kujiweka kwenye njia ambayo tutawavuta wakorofi kuwa karibu nasi zaidi.

Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE.

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.