Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, September 25, 2015

Jinsi Ambavyo Unavyoweza Kuitumia Dakika Moja Kubadili Maisha Yako.

No comments :
Inaweza ikawa ni kitu cha kushangaza kidogo kwako, lakini huu ndiyo ukweli, unao uwezo wa kutumia dakika moja tu kubadili maisha yako. Kama wewe ni mtu wa visingizio kila wakati mara ‘oooh mimi sina muda’ utachelewa na utaacha mipango yako mingi ipotee bure.  Dakika moja ni ya thamani kubwa kwako na inakutosha kufanya uamuzi wa msingi utakao kuletea mabadiliko kwenye maisha yako.
Ni rahisi kusema haiwezekani, lakini inawezekana. Unawezaje kufanya mabadiliko hayo kwa kutumia dakika moja ili kubadili maisha yako na wengine pia? Kumbuka tu kwamba:-
1. Inakuchukua dakika moja tu, kuchukua uamuzi wa kutafakari kile unachokwenda kukifanya katika siku yako ya leo.
2. Inachukua dakika moja tu, kuchukua uamuzi wa kufanikiwa au kushindwa katika maisha yako.
3. Inachukua dakika moja tu, kuamua kujenga hofu ama kujimini katika maisha yako katika kila jambo unalotaka kulifanya katika maisha yako.
4. Inachukua dakika moja tu, kumwambia mtu aliyekata tamaa kuwa ni lazima atafanikiwa.

5. Inachukua dakika moja tu, kusema mwenyewe kuwa basi nimeshindwa kwa kile ninachokifanya au nitaendelea kung’ang’ania mpaka nipate matokeo ninayoyahitaji.
6. Inachukua dakika moja tu, kumwonyesha upendo mtu yule ambaye anajihisi mpweke.
7. Inachukua dakika moja tu, kuamua kuwa wewe ndiye kiongozi pekee wa maisha yako.
8. Inachukua dakika moja tu,  kuamua kuishi maisha ya kuwaumiza wengine au kuwa msaada kwao.
9. Inachukua dakika moja tu, kuamua kuwa utabadilika na kuwa na tabia za mafanikio au utaendelea na maisha yako uliyonayo sasa.
10. Inachukua dakika moja tu, kujikubali kuwa wewe ni mshindi na hakuna kitu kinachoshindikana kwako na kwa uamuzi huo ni lazima ufanikiwe.
Kitu cha kujiuliza hapa, je unaitumia vipi dakika uliyonayo ili uweze kukufanikisha kufikia mafanikio makubwa unayoyahitaji? Kumbuka dakika moja tu inaweza kukufanikisha au kukufanya ukashindwa kwenye maisha yako kutokana na kile unachokiamua ndani ya dakika hiyo.
Watu wengi wameharibu maisha yao kutokana na maamuzi madogo madogo wanayoyafanya kwa dakika hiyo moja. Kwa mfano kama umefanya maamuzi mabaya kwa dakika sitini, tafsiri yake ni kwamba umeharibu maisha yako mara sitini. Kuwa makini na dakika yako moja na itumie vizuri ikufanikishe.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio na endelea kutembelea DIRA YAMAFANIKIO kujifunza na kuhamasika.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
 Imani Ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nami kwa email dirayamafanikio@gmail.com au simu 0713 048035 kwa ushauri na msaada wa haraka.No comments :

Post a Comment