Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, November 23, 2015

Kama Utashindwa Kuyatawala Mambo Haya, Huwezi Kufanikiwa Tena.

No comments :
Mafanikio siku zote hayaji kama ajali. Mafanikio ni safari ambayo huwa ipo hatua kwa hatua. Mafanikio kwa kawaida hayaji leo ghafla na kusema umefanikiwa, hapana. Mafanikio mara zote yanakuwa na taratibu zake ambazo ni lazima zifuatwe ili kufanikiwa.
Taratibu hizo au sheria hizo zinaposhindwa kufuatwa hakuna tena mafanikio yanayoweza kujitokeza zaidi ya kushindwa. Moja ya taratibu au sheria ambayo ni lazima uifate na ikupe mafanikio ni ‘sheria ya kutawala’. Ni lazima yawepo mambo ya kuyatawala kwenye maisha yako ili ufanikiwe. Bila kuyatawala mambo hayo itakuwa ngumu sana kufikia mafanikio makubwa.
Wengi hujikuta wakishindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutaka kujaribu kutawala kila kitu au kushikiria kila jambo. Kwa maisha kama hayo inakuwa ni ngumu sana kuweza kufanikiwa. Kwa hiyo kama unataka kufanikiwa ni lazima umudu kutawala mambo haya, ukishindwa kufanya hivyo sahau mafanikio.
1. Kutawala pesa.
Huwezi kupata mafanikio kama matumizi yako ya pesa hayako sawa. Hili ni jambo linalowatesa wengi na kuwasumbua. Lakini ili ufanikiwe ni lazima kutawala pesa na siyo pesa ikutawala wewe. Unapokuwa una mudu kuitawala pesa inakusaidia katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza. Unataka maisha yako yote uishi kiumaskini, acha pesa ikutawale.

TAWALA MUDA WAKO VIZURI.
2. Kutawala hamasa.
Nguvu kubwa ya mafanikio unaipata kutokana na wewe kuwa na hamasa kila siku. Hamasa tunaweza tukasema kama ni mafuta ya kukusaidia kusonga mele. Mara nyingi hamasa inapokosekana inakuwa siyo rahisi sana kuweza kufanikiwa. Kwani kazi kubwa ya hamasa ni kukupa nguvu na kichocheo cha kuendelea mbele zaidi ya ulipo.
3. Kutawala kasi ya mafanikio.
Ni uhimu kutawala kasi yako ya mafanikio yako. Unaweza ukajiuliza kivipi?sikiliza, kasi ya mafanikio unaitawala kwa kuhakikisha unafanya jambo linalokusogeza kwenye mafanikio kila siku. Kwa kufanya jambo hilo kila siku hata kama ni kidogo hapo utakuwa unaendana sawa na kasi ya mafanikio unayoitaka. Ila kama utashidwa kuitawala kasi hii na kushindwa kufanya jambo hata dogo ni lazima uachwe.
4. Kutawala tabia njema.
Ili uwe na mafanikio makubwa ni lazima uwe na tabia njema zinakusogeza kwenye mafanikio kila siku. Ukiwa na uwezo wa kutawala tabia hizi za kimafanikio uwe na uhakika ni lazima uweze kufanikiwa. Lakini kama utatawaliwa na mambo hayo basi tegemea anguko kubwa sana kwenye maisha yako.
5. Kutawala muda.
Muda ni kitu muhimu sana katika mafanikio yoyote. Pamoja na umuhimu wote huu wa muda, kwa bahati mbaya sana wengi wanatumia muda vibaya. Kwa tatizo kama hili la kutumia muda vibaya na kushindwa kutawala muda hupelekea maisha ya wengi kuharibika. Ukitaka kujua hili vizuri, cheza na muda wako sasa, baada ya miaka kumi utaniambia nini ambacho kitakutokea kwenye maisha yako.   
Haya ndiyo mambo unayotakiwa kuyatawala ili kufanikiwa kama ikatokea umeshindwa kutawala jambo mojawapo kati ya hayo basi utakuwa umejiweka kwenye wakati mgumu wa kuweza kufanikiwa.
Nikutakie siku njema, kumbuka endelea kuwashirikisha wengine waendelee kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment