Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Tuesday, November 24, 2015

Kama Utatumia Kanuni Hii, Mafanikio Ni Yako.

No comments :
Siku zote elewa ukweli huu, chochote unachokifanya katika maisha yako kinauwezo wa kukufanikisha. Hiyo haijalishi kitu unachokifanya ni kidogo au kikubwa kiasi gani. Kitu cha kuzingatia ili kupata mafanikio hayo ni kukifanya kwa juhudi zote huku ukitumia kanuni za mafanikio. Kanuni hizi za mafanikio zinapotumika ni lazima mafanikio hutokeo.
Bila shaka unajua hili na ni mara nyingi tumekuwa tukiongelea juu ya umuhimu wa kutumia mbinu na kanuni mbalimbali za mafanikio ili kutufanikisha. Sababu ya kubwa ya kufanya hivi ni kwa sababu kila zinapotumika matokeo chanya huweza kuonekana. Leo hii napenda nikukumbushe kanuni moja nyingine ya mafanikio ambayo ukiitumia ni lazima ibadili maisha yako kwa sehemu kubwa.
Kanuni hii inasema ‘fanya kama kila mtu anakuangalia’. Kwa kila jambo unalolifanya katika maisha yako lifanye kama vile mtu anakuangalia. Kama ni malengo panga malengo yako ukiamini kabisa pembeni yako kuna mtu anakutazama. Kama ni kupokea simu, pokea simu ukiamini kuna mtu anakutazama. Kwa kila tendo na mwenendo mzima fanya hivi kama unatazamwa na mtu mwingine.
Kwa kufanya hivi, itakusaidia sana kufanya mambo yako kwa umakini mkubwa na utakuwa bora zaidi siku zote. Hebu jaribu kufikiria wakati ambapo ulifanya kazi zako kwa kusimamiwa, hizo kazi zako ulizifanyaje? Bila shaka ulifanya kwa umakini sana. Na ulifanya hivi kwa sababu ya kuogopa kuharibu kile kitu ambacho ulikuwa ukisimamiwa na kuonekana wa ajabu.

FANYA KAMA KILA MTU ANAKUANGALIA
Hivi ndivyo kanuni hii inavyofaya kazi. Itumie kanuni hii, kwa kujijengea picha na kujitazama wewe kama vile unavyotazamwa na mtu mwingine ukifanya mambo yako. Kwa hili bila shaka hutaleta mchezo ni lazima uwe makini. Fikiria jambo hili pia, kama ingekuwa inatokea malengo yako ukayaweka hadharani ni nini kingetokea? Bila shaka ungekomaa sana mpaka yatimie. Unajua kwa nini? Kwa sababu usingekuwa tayari kukubali kuchwekwa kwa kushindwa kutimiza malengo yako.
Mara nyingi wengi wetu tunaharibu katika maisha yetu kwa sababu ya kujua kwamba eti hatufatiliwi. Jifunze kujisimamia mwenyewe kwenye maisha yako kama vile ambavyo unasimamiwa na mtu mwingine. Kumbuka siku zote hili katika maisha yako, ili kufikia mafanikio makubwa. FANYA KAMA VILE MTU ANAKUANGALIA.
Kwa umejua hili jipe ahadi mwenyewe ya kufanya kila jambo kama vile mtu mwingine anakuangalia. Sina shaka ukiweka picha hii vizuri kichwani mwako utajituma sana na itakusaidia sana kufanikisha mambo mengi ambayo ingekuwa siyo rahisi kwako kuyafanikisha kama usingekuwa na picha hii vizuri.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment