google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jul 9, 2020

Kama Hujui, Ndoa Imara Ni Tamu Kuliko Fedha.

No comments :
Karibu tena mpenzi msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO. Karibu tena katika siku nyingine ya kuweza kujifunza yale yote yaliyomuhimu kuweza kuboresha maisha yetu. Katika makala yetu tutaangalia umuhimu wa kuwa na ndoa bora ambayo inaweza ikatusaidia kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka, unapokuwa katika migogoro mingi ya kifamilia itakuwa ni ngumu kwako kufanikiwa kutokana na vurugu za hapa na pale kila siku.
Je, wewe binafsi unaamini katika kuoa au kuolewa, kwamba ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu? Kama huamini sana katika jambo hilo, huenda inabidi uanze kuamini. Kwa nini?
Tafiti za karibuni kuhusiana na furaha maishani, zinaonyesha kwamba, watu waliolewa au waliooa wameonesha kuwa na furaha zaidi kuliko wale wasiooa au kuolewa, bila kujali kipato.
Wale watu wenye kipato kizuri na ambao wameoa au kuolewa wamebainikia kuwa na furaha kwa asilimia kubwa zaidi. Wale watu ambao wameolewa au kuoa, bila kujali kipato chao, wanaripotiwa kuwa na furaha kuliko wale wasiooa au kuolewa, ambao ni matajiri.
Watu sita kati ya kumi ambao wameoa au kuolewa, wanadaiwa kuwa na ridhiko la namna maisha yao yanavyoenda, ukilinganisha na wanne kati kati ya kila kumi ambao hawajaoa au kuolewa.

Inaonyesha kwamba, kuna uhusiano kati ya fedha, ndoa na furaha na ridhiko kwenye maisha ya watu. Watafiti wengi hivi sasa wanakiri kwamba, ndoa ina thamani na maana zaidi kuliko fedha, linapokuja suala la furaha au ridhiko la maisha kwa binadamu.
Mtu mwenye ndoa ya furaha, anakuwa na ridhiko na furaha kubwa maishani, bila kujali pato lake. Yule ambaye hayuko kwenye ndoa, bila kujali pato lake, kiwango chake cha furaha huwa ni cha chini sana. Kama unafikiri natania waulize wenye ndoa ambazo zina usalama ndani yake watakwambia ukweli wa hili zaidi.
Nimesema ndoa ya furaha kwa sababu, mtu aliye kwenye ndoa ngumu, kiwango chake cha furaha kinakuwa chini kuliko kile cha mtu ambaye hayuko kwenye ndoa, bila kujali vipato vyao.
Tafiti zinaonyesha pia kwamba, karibu watu sita kati ya kila kumi walio kwenye ndoa za furaha, ambao wanapato la chini hufurahia maisha yao na wanaridhiko kubwa zaidi. Ni watu watano kati ya kumi tu ya  wale wenye pato kubwa, ambao hawako kwenye ndoa, wanaofurahia maisha.
Hata hivyo, wale walio kwenye ndoa, ambapo pia wanakipato kikubwa, wameonekana kuwa na furaha zaidi. Ni saba kati kati ya kumi kati ya watu hao, ambao wamebainika kuwa na furaha na kuridhishwa na maisha wanayoishi.
Kuna wimbo ambao nimewahi kuusikia ukisema, kwamba, watu wanashangaa wanandoa fulani maskini, kwani kila siku wanawaona wanandoa hao wakitabasamu, pamoja na ‘njaa’ waliyonayo. Ni kweli, walio kwenye ndoa imara, wanajisikia vizuri bila kujali kama wanafedha au hawana.
Wasio kwenye ndoa au wenye ndoa ngumu,  hata kama wanamamilioni ya fedha vipi, maisha yao ni mzigo mzito sana. Kwa nje wanaweza kuonekana kama ni watu walioridhika, wakati kwa ndani wanamashaka makubwa na maumivu yasiyosemekana.
Ndio maana baadhi ya wanauchumi wanasema, watu waliokwenye ndoa imara ni rahisi sana kwao kupata pesa. Urahisi huu unaletwa na ule ukweli kuwa, watu hawa wanafuraha na wameridhishwa na maisha yao, kiasi kwamba huyaona mambo kwa upana wake.
Pamoja na kwamba, watu wengine kwenye ndoa, huwa wanaamini kwamba, wakipata fedha ndipo watakapokuwa na furaha katika ndoa zao, hali ni kinyume.
Ndoa isiyo imara haiwezi kubadilishwa na kuwa imara kwa kupatikana kwa fedha, zaidi italeta matatizo mengine. Lakini ndoa imara ni nzuri na tamu kuliko kuwa na fedha.
Kwa makala nyingine nzuri zaidi endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza kila siku na kuboresha maisha yako. Pia usiache kuwashirikisha wengine kuweza kujifunza kupitia mtandao huu.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0687449428.




  

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.