Jan 22, 2016
Misingi 5 Ya Kuifahamu Kabla Hujaanza Biashara.
Karibu tena mpenzi
msomaji wa makala hii ya DIRAYA MAFANIKIO, ni wakati
mwingine tunakutana tena katika safu hii ili kuweza kukumbushana
baadhi ya mambo msingi katika biashara zetu, ili kuweza kufanya biashara yenye
faida kubwa.
Mara nyingi baadhi
yetu huwa tunaanza biashara kwa kusikia kwa watu faida ya biashara hiyo, bila
kuwa na msingi halisi wa kuifahamu biashara husika. Lakini katika makala yetu hii ya leo
tutaangalia misingi muhimu ya kuielewa mapema kabla ya kuanza biashara yoyote.
Mambo hayo ya msingi
tutakayojifunza hapa ni maalumu kwa ajili ya wote wanaotaka kuwa wafanyabiashara
wakubwa na wadogo pia. Kwa yeyote anahitaji kupata faida kubwa na kuepuka
kupata hasara zisizo za lazima katika biashara yake, misingi hii ni muhimu sana
kwake kuijua.
1. Eneo la kufanyia
biashara.
Kwa kuwa ndio kwanza
unaanza kufanya biashara lazima ufanye uchunguzi wa kutosha juu ya kile
unatochotaka kukifanya. Eneo hili lakufanyia biashara ni lazima
ulichunguze kwa kuangalia uhitaji wa wa wateja wa eneo husika.
Kwa mfano kama unataka
kufanya biashara ya kuuza vifaa vya shule (stationery) lazima ujiulize ni wapi
ambako unahisi ukiweka biashara yako kuna wateja wengi. Baada ya kufikiri
unaweza ukaangalia kwenye maeneo ya shule,vyuo , kanisani na maeneo mengine.
Lakini hiyo haitoshi nenda
sehemu husika jaribu kufanya uchunguzi ni vitu gani wanavifanya wafanyabiashara
wengine ambao wana biashara kama yako? Angalia ni changamoto gani wanazozipata
ili pindi ukianza kufanya biashara hiyo ujue mbinu za kupambana na changamoto
hizo kirahisi.
2. Wateja.
CHAGUA ENEO ZURI LA KUFANYIA BIASHARA. |
Baada ya kuona ni eneo gani linafaa kufanya biashara jambo la
pili la kujiuliza je wateja wako watakuwa ni wakina nani? Hili ni swali la
msingi sana kujiuliza kwa sababu lengo la kufanya biashara ni kupata wateja
wengi, hata hivyo katika kuangalia hili pia fanya uchunguzi wa kina juu
mahitaji ya wateja.
Hii utakusadia wewe pindi unapofikiri ni biashara gani ya
kufanya.Tukiangalia tena mfano wa kuanziasha biashara ya vifaa vya shule yaani
(stationery) tunaona ya kuwa wateja wako watakuwa ni wanafunzi na baadhi ya
watu wengine kama eneo ambalo ulilifikiri la kufanyia biashara itakuwa kwenye
taasisi yeyote mfano shule au kanisani.
3. Bidhaa.
TAZAMA ENEO LENYE WATEJA WA KUTOSHA. |
Ewe msomaji wa makala
hii unayependa kufanya biashara yeyote eidha ni ndogo au kubwa lazima ufikiri
kwa kina je bidhaa gani ambazo utaziuza? Swali hili la bidhaa utajiuliza baada
ya kufanya uchunguzi juu ya eneo husika la kufanyia biashara? na pia kwa
kuangalia je ni mahitaji gani ya wateja ?
Pia jifunze kuangalia
bidhaa ambazo baada yakufanya uchunguzi na ukagundua ni bidhaa gani adimu
pia zina uhitaji mkubwa chukua kama changamoto na lifanye kama fursa. Ukishapata
majibu fanya utaratibu wote mpaka upate bidhaa hizo.
4. Matangazo.
BIDHAA ZAKO ZIWE NA UBORA |
Kuna usemi husema
biashara matangazo. Hii ni kweli kabisa ili biashara iweze kuwa nzuri ni lazima
wateja wako waipate kupitia matangangazo. Matangazo haya yanaweza kuwa
kuwajulisha wateja wako juu ya ujio wa bidhaa mpya, mabadiliko ya bei na vitu
vinginevyo vihusuvyo biashara.
Matangazo haya unaweza
kuyasambaza kupitia mitandao ya jamii na vyombo vya habari pia kwa mfanyabiashara
mdogo unaweza ukaandika bango la biashara nje ya eneo lako la
biashara unayoifanyia ili kuwajulisha wateja wako.
Tunakutakia kila la kheri
katika mafanikio ya biashara yako.
Makala hii imeandaliwa na:-
Afisa
mipango na mendeleo,
Mr.
Benson .O. Chonya,
Mawasiliano,
Instragram;
Benson Chonya,
Facebook;
Benson Chonya,
Tel;
+255 757 909 42.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.