Jan 19, 2016
Mambo Matatu Ya Kukusaidia Kujua Biashara Unayotakiwa Kuifanya.
Pengine
umekuwa ukiwaza, ukifikiri ni kwa namna gani au ufanye biashara ipi itakayokusaidia
kukuingizia pesa nyingi na za kutosha. Na wakati mwingine umekuwa ukisumbuka
pia kutafuta ushauri ni biashara gani ya kufanya. Hayo naamini ndiyo yamekuwa
mawazo yako kwa muda mrefu.
Ikiwa
kweli hayo ndiyo yamekuwa mawazo uliyonayo kwa muda sasa, hilo lisikupe shida.
Unao uwezo mkubwa wa kujua na kutambua aina gani ya biashara unayotakiwa
kuifanya na ikakupa faida. Je, unajua ni mbinu gani utatumia kutambua aina ya
biashara unayotakiwa kuifanya?
Hivi Ndivyo unavyoweza Kujua Ni Aina
Gani Ya Biashara Ufanye.
1. Biashara uliyoichagua inauwezo wa
kutatua tatizo katika jamii?
Hapa
sio suala tu kufanya biashara, je jiulize biashara hiyo ina uwezo wa kutatua
matatizo ya watu kwa sehemu kubwa? Kama jibu ni ndiyo basi unaweza ukaifanya
biashara hiyo na ikakuletea mafanikio. Lakini kama utajikuta umechagua biashara
ambayo haina uwezo wa kutatua matatizo ya watu, hiyo haikufai na utapoteza muda
wako kuifanya.
IPENDE BIASHARA YAKO. |
2. Je, unaipenda kweli biashara hiyo?
Biashara
unayokwenda kuifanya uwe na uhakika itakuchukulia muda wako mwingi sana. Kitu
cha kujiuliza wewe binafsi je,ni kweli una mapenzi nayo? Unaipenda na upo tayari
kutoa kila kitu ili kufanikiwa. Haijalishi biashara yako inatatua matatizo
makubwa vipi kwenye jamii kama huna mapenzi nayo ya dhati ni wazi utaiua na
hutafika popote.
3. Je, upo tayari kukabiliana na
changamoto?
Acha
kutegemea ukaingia kwenye biashara leo na ukapata faida ni kitu ambacho
hakiwezekani. Kama ni hivyo na unaona una wazo zuri la biashara yako, jiulize je
utakuwa tayari kukabiliana na changamoto zozote zile zitakazojitokeza? Kama
unaona uwezo huo unao, basi hakuna pingamizi unaweza ukaanza biashara yako mara
moja.
Kwa
msingi huo kama unataka kuanzisha biashara unayoamini itakupa faida, hayo ndiyo
mambo ya msingi sana kwako kuyazingatia.
Dira
ya mafanikio inakutakia mafanikio mema katika biashara yako. Na kumbuka endelea
kujifunza kila siku bila kuchoka.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama
una maswali, changamoto au unahitaji ushauri wa kibiashara, usisite kuwasiliana nasi kwa:-
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.