Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Friday, May 6, 2016

Tumia Kidogo Ulichonacho, Kikusaidie Kufanikiwa.

No comments :
Je, hapo ulipo huna muda wa kutosha kufanya mambo yako kwa ukamilifu? Kama jibu ni ndiyo, tumia muda kidogo ulionao kufanya mambo yako machache tu tena kwa uhakika.
Je, kila ukifikiria unaona huna pesa ya mtaji na unaona huwezi kabisa kuanza biashara? Kama jibu ni ndiyo, tumia pesa kidogo uliyonayo kuwekeza kwa uwekezaji mdogo ambao utakuwa unakua pole pole badala ya kukaa kusubiri mtaji ambao huna uhakika hata wa kuupata.
Je, unafikiri huna uzoefu wa kutosha kufanya kile unachotaka kukifanya na unahisi ni lazima uongeze uzoefu? Kama jibu ni ndiyo, tumia uzoefu huo mdogo ulionao kufanya hicho unachotaka kukifanya hata kama ni kwa kidogo.
Je, huna marafiki wa kutosha kukusaidia kufikia mafanikio makubwa? Kama ni hivyo anza na marafiki chanya hao ulionao kukusaidia kufikia mafanikio yako, hata kama rafiki huyo ni mmoja anza naye huyo huyo kwanza.

Acha kudharau kidogo ulichonacho.
Je, ni kipi ambacho unafikiri huna, kuanza kile unachotaka kufanya kwenye maisha yako? Kama unasubiri kila kitu kiwe tayari ndio uanze nakupa uhakika itakuwa ngumu sana kuanza na kufanikiwa. Mara nyingi mambo huwa yanaanza hivyo hivyo bila kusubiri kukaa vizuri sana. Ni wakati wako wa kuchukua hatua na si kusubiri.
Yapo mambo mengi yakujifunza unapoanza jambo hata kama unajihisi haupo kamili kuliko ungekaa na kusubiri. Siku zote acha kusubiri, tumia rasilimali ulizonazo, tumia chochote ulichonacho kukusaidia kufanikiwa kuliko kukaa na kusubiri kwamba eti siku moja mambo yako yatakuwa safi, utajichelewesha.
Jaribu kukaa chini na kufikiria ni kitu gani ambacho una uwezo wa kukifanya kwa kutumia kile kidogo ulichonacho. Acha kujidharau, heshimu ulichonacho, kwani kina uwezo mkubwa sana wa kukusaidia kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa ikiwa wewe mwenyewe utaamua iwe hivyo. Ukitumia kidogo ulichonacho uwe na uhakika utafanikiwa.
Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment