Jul 1, 2016
Mfumo Wa Kutotoresha Vifaranga Kwa Kutumia Mafuta Ya Taa.
Baada ya Rais wa
Jamuhuri Ya Muungano Tanzania kutangaza ya kwamba katika katika uongozi wake,
itakuwa ni serikali ya viwanda, watu wengi walijiuliza ni kivipi, inawezakana
kuwa hivyo?
Hata mimi ni
miongoni mwa watu hao, ila baada ya kufanya uchunguzi mtu anapozungumzia
viwanda maana yake nini? basi nikaja kupata majibu ya kina kuwa Tanzania ya
viwanda inawezekana kabisa.
Ngoja nikushirikishe
juu ya utafiti wangu. Unapozungumzia Tanzania ya viwanda katika fikra za watu
ni kwamba watu wengi wanawaza katika picha kubwa sana, ukiwaza katika misingi
hiyo utakuja na jibu ya kwamba haiwezekani kabisa.
Lakini endapo
utawaza Tanzania ya viwanda katika picha ndogo pia inawezekana kabisa. Katika
kuwaza katika picha ndogo utakuja kugundua ya kwamba nchi ya Tanzania ina
viwanda vidogo vidogo vingi sana ambavyo endapo vitaweza kutambuliwa vinaweza
kuifanya Tanzania kuwa katika sura mpya ya viwanda zaidi.
Ukichunguza kwa kina
hapa nchini hata yule mtu anayeshona nguo, anayepasua mbao, anafanya uhunzi wa
kutengeneza majiko,sufuria, vijiko, kufyatua tofari vyote ni viwanda ila kwa
sababu hatuvipi thamani vitu hivyo tunaona ni vitu vya kawaida sana.
John Haule kulia akiwa na Afisa Mipango Benson |
Hata hivyo endapo
vitachukuliwa kama ni viwanda wapo baadhi ya watu kutoka mataifa mbalimbali
wataagiza vitu hivyo kutoka hapa nchini. "Usipeleke hirizi
sokoni ila kuwa wa mbunifu kwa jambo ambolo unalifanya"
Huu ni msemo ambao
unatupa hamasa kama kweli tunahitaji Tanzania ya viwanda, kama tunahitaji
ubunifu wa vitu vyetu na sio kuiga vitu ambavyo vimekwisha tengenezwa.
Katika harakati za kutafuta ukweli wa jambo hilo, niliweza kukutana na John haule ambaye alinishangaza juu ya ubunifu wake. Yeye ameweza kutengeneza mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku ambayo inatumia mafuta ya taa.
Katika harakati za kutafuta ukweli wa jambo hilo, niliweza kukutana na John haule ambaye alinishangaza juu ya ubunifu wake. Yeye ameweza kutengeneza mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku ambayo inatumia mafuta ya taa.
Mashine hizi zipo za
aina tofauti kulingana na mahitaji ya mteja, mashine Hii ipo ambayo ina uwezo wa
kutotolesha idadi ya vifaranga kuanzia 30 na kuendelea. Mashine hii inauwezo wa
kutumika mahali popote pale amabo mfugaji atahitaji kufanya shughuli zake.
Muonekano wa mashine
hii;
Mwonekano wa nje wa mashine |
Ina nafasi pana kwa
ajili ya kuweka mayai kwa ajili ya kutotolesha vifaranga. Upande wa ndani ina
taa za mafuta ya taa ambayo itawaka kipindi chochote cha kukutolesha vifaranga,
pia mashine hii ina thermometer ambayo kazi yake ni kupima joto litakalokuwepo
pindi Mayai yanafanya kazi ya kutaka kujitotolesha
Namna ya kuchagua mayai kwa ajili ya kuweka kwenye
mashine hiyo.
1.Hakikisha yai au
mayai ambayo unayaweka hayazidi siku 12 tangu kutotolewa.
2. Hakikisha yai
ambalo halijatagwa na kuku mzee.
3. Pia hakikisha
mayai hayapatwa na msukosuko mingi kama kupakia kwenye baiskeli.
4. Hakikisha kwamba
mayai ambayo unaweka kwenye mashine hii yanakuwa sio mayai ambayo machafu.
5.Hakikisha kuweka mayai ambayo umekusudia kuweka maana endapo utaweka hata yai la nyoka utalikuta baada ya kutotoleshwa utakuta hata watoto wa nyoka.
Namna ya kuitumia mashine.
Hakikisha kuwa taa inawaka muda wowote, wa kuatamia kwa mayai. Pia pindi mafuta ya taa yakiisha unaongeza.
5.Hakikisha kuweka mayai ambayo umekusudia kuweka maana endapo utaweka hata yai la nyoka utalikuta baada ya kutotoleshwa utakuta hata watoto wa nyoka.
Namna ya kuitumia mashine.
Hakikisha kuwa taa inawaka muda wowote, wa kuatamia kwa mayai. Pia pindi mafuta ya taa yakiisha unaongeza.
Hakikisha ya kwamba
kila baada ya masaa 6 unachezea mayai kama ambavyo kuku hufanya.
Hakikisha pia
unakuwa unaangalia joto ambalo linakuwa ndani ya mashine hiyo kupitia
thermometer hiyo. Joto kwenye thermometer hiyo linakuwa kati ya 37. Maana
likizidi au likipungua linakuwa na madhara kwa mayai.
Baada ya hapo vifaranga hivyo kutolewa utaviacha ndani ya mashine hiyo ambayo inatumia taa kwa siku mbili kisha unavitoa na kuvipeleka katika banda la kufugia vifaranga ( bluda) kisha unavianzisha vifaranga hivyo chakula cha mwanzo cha vifaranga (stata )
Baada ya hapo vifaranga hivyo kutolewa utaviacha ndani ya mashine hiyo ambayo inatumia taa kwa siku mbili kisha unavitoa na kuvipeleka katika banda la kufugia vifaranga ( bluda) kisha unavianzisha vifaranga hivyo chakula cha mwanzo cha vifaranga (stata )
Kutokana na takwimu kutoka bodi ya takwimu ya
mwaka 2012 zaidi ya kaya milioni 2.3 zinafanya ufugaji ambao ndio chanzo
cha watu wengi kupata kipato.
Hata hivyo takwimu
ya bodi hiyo inasema milioni 35.5 ni idadi ya kuku wa asili, milioni 24.5 ni
idadi ya kuku wa kisasa ambayo inatupa jumla ya milioni 60.1.
Pia takwimu hizo
zinaonesha ya kwamba kwa hapa Tanzania baadhi ya mikoa ambayo inaongoza katika
ufugaji ni Shinyanga, Mbeya, Mwanza , Tabora, Morogoro, Iringa, Simiyu,Tanga na
sehemu zinginezo pia inakadiliwa kuwa kilo 6.8 za nyama huliwa kwa mwaka.
Uzuri Wa mashine hii
ni kwamba unaweza kutengeneza kipato kingi na kuacha kulalamika suala la
umaskini au ajira kwa ujumla wewe kijana mwenzangu.
Hii ni fursa tosha
ya kufanya ufanikiwe zaidi leo hii endapo utaamua kuifanya. Pia kwa kuwa ni
fursa ambayo inaenda sambamba na Tanzania ya viwanda hivyo inakujali sana kwa
namna moja ama nyingine katika kuondokana na umaskini.
Pia uzuri mwingine
wa kifaa hiki ni kwamba inabana matumizi ya umeme na kama ni kijijini ambako
ndiko kwenye idadi kubwa ya watu.
Pia tumshukuru Mtanzania
mwenzetu kwa mara nyingine tena John Haule. Kwani amekuwa mbunifu kuweza kuleta
njia ya kuondokana na umaskini kwani ni zamu yetu kuwa wazalishaji na mataifa
ya nje kuwa watumiaji Wa bidhaa zetu.
Kuna mataifa
ambayo naamini ya kwamba ni zamu yao kutumia bidhaa zetu.
Unaweza ukawasiliana
nami afisa mipango, ikiwa unapenda kujua zaidi kuhusu mashine hizi, nami
nitakuunganisha na mtaalamu wetu John Haule.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Hongera sana kwa ubunifu huo utakaomwezesha mtanzania wa hali ya chini kuyafikia malengo yake kimaisha.
ReplyDeleteVizuri sana na hongera sana kwa kaz hii kubwa zaid kwa taiga letu LA Tanzania. Kwa kua site tuna lengo LA kujenga taifa moja basi hatuna budi kushirikiana ktk nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
ReplyDeleteOMBI LANGU.ninaomba utupe elimu pia jinsi ya kuitengeneza machine hiyo ili watanzania walio wengi waweze kunufaika nayo nakuweza kufikia malengi yetu ya Tanzanian ya viwanda. Ikiwa Ni pamoja na kutueleza changamoto zake. ASANTE
Naomba namba ya tigo pia je unaziuza kama unauza bei gn
ReplyDelete