Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, May 5, 2016

Mambo 3 Yanayoogopwa Na Watu Wengi Katika Maisha.

No comments :
Ni ukweli usiopingika kwamba kati ya kitu kimojawapo kinachomsumbua binadamu ni woga wa mambo mbalimbali. Binadamu huyu amekuwa mwoga wa kifo, ni binadamu huyu huyu pia amekuwa mwoga wa kuachwa na mpenzi au mwoga wa mambo madogo hata yale ambayo anauwezo wa kuyamudu au hayastahili kuogopwa sana.
Lakini pamoja na woga wa mambo hayo, yapo mambo matatu ambayo yamekuwa yakiogopwa sana na watu wengi katika maisha. Mambo haya yamekuwa yakiwanyima na kuwapotezea wengi furaha hasa pale kila wanapoyakumbuka. Kwa kusoma makala haya utayajua mambo haya vizuri ambayo wengi wanayaogopa. Je, unajua ni mambo gani? Twende pamoja kujifunza.
1. Woga wa kuogopa kuzeeka.
Kati ya kitu ambacho kinawatisha watu walio wengi ni kule kuogopa kuzeeka. Hakuna ambaye anapenda kuzeeka. Kila mtu anapenda kuonekana akiwa kijana siku zote ingawa kiuhalisia ni kitu ambacho hakiwezekani. Utake usitake ni lazima uzeeke hata ufanyaje. Kuzeeka ndio asili ya maumbile yetu wanadamu. Hofu hii ya kuzeeka ipo sana kwa watu wengi ingawa lakini, kwa wanawake ndio wanaongoza kwa kuwa na woga wa kuzeeka kuliko wanaume.

Jifunze kuukabili woga wako.
2. Woga wa kuogopa kuwa mpweke.
Si woga tu wa kuzeeka ambao unaonekana kuwa tishio kwa watu wengi, bali pia kwa siku za hivi karibuni woga wa kuwa mpweke umeshika kasi sana. Wengi wanaogopa kuishi maisha ya upweke. Upweke ninaozungumzia hapa ni upweke wa kuishi bila mume au mke. Pia kwa bahati mbaya na katika hili wanawake wapo kwenye hofu sana ukilinganisha na wanaume. Hofu ya upweke imekuwa ikitawala sana kutokana na watu wengi kutotaka kuoa au kuolewa. Hivyo wengi wanakuwa wana wasiwasi na kujiuliza kama watakuwa wapweke sasa, uzeeni itakuwaje?  

Wengi upweke unawatesa.
3. Woga wa kuogopa mabadiliko.
Woga mwingine unaoogopwa na wengi ni woga wa kuhofia mabadiliko. Kiasili binadamu ni mwoga wa madiliko hata kama mabadiliko hayo yana manufaa kwake. Kitu ambacho mtu anakata ni kubaki katika lile eneo alipo na kutulia hata kama liamuumiza, lakini ili mradi mabadiliko kwake mtu huyo ysiwepo. Kutokana na wengi kuhofia sana mabaliliko hali hiyo hupelekea maisha kuzidi kuwa magumu kwa wengi kutokana na kule kushindwa hata kubadili mambo yatakayowasaidia katika maisha yao.

Fanya mabadiliko ya kukutoa kimaisha.
Kwa walio wengi hayo ndiyo mambo wanayoyaogopa sana katika maisha yao. Wewe je,ni nini kinachokuogopesha kwenye maisha yako? Kama hakuna hongera sana.
Ansante kwa kusoma makala haya na endelea kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email; dirayamafanikio@gmail.com

No comments :

Post a Comment