google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jun 2, 2016

Watu Hawa Badala Ya Kuzeeka Wanazidi Kuwa Wazuri.

No comments :
Je, imeshawahi kukutokea kwako ukatazama kwenye kioo na kubaini kwamba, umekuwa mzuri zaidi ya ulivyokuwa jana? Kama hiyo imeshatokea, ujue kwamba, huko peke yako. Kwa nini huko peke yako? ni kwa sababu, hata watafiti wamebaini kwamba, binadamu hutokea akaoongezeka uzuri kwa kadri siku zinavyokwenda.
Haijafahamika hata hivyo kwamba, ni hisia au mitazamo tu yenye kubadilika au ni kweli watu huongezeka uzuri kwa kadri siku zinavyokwenda mbele. Hata hivyo kiwango cha utafiti uliofanywa kinaonyesha kwamba, huenda kuna ukweli kwamba, kiwango cha mtu kuvutia huongezeka kwa kadri siku zinavyoenda.
Hata hivyo, wanawake wameonekana kuwa kwenye uwezekano wa kuhisi kuongezeka uzuri kuliko wanaume, kwa kadri siku zinavyoenda. Imebainika kwamba, wasichana wanaomaliza elimu ya sekondari na hata vyuo, wako kwenye umri ambao, ndiyo hasa mabadiliko hayo yanaonekana au kujitokeza zaidi. Kuna wale ambao hubaini kwamba, katika miezi kadhaa, wameongezeka uzuri na wengine kubaini kwamba, uzuri wao umeongezeka tofauti na walivyolkuwa miaka mitano nyuma.

Imeelezwa kwamba, wanawake huwa wanaona kwamba, siku zilizopita hawakuwa wazuri na wala hawakuwa na miili mizuri kama waliyonayo hivi sasa na huamini pia kwamba, watakuwa wazuri zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda.
Wanawake wanaamini kwamba, kila siku kuna nafasi kwa upande wao kujibadili linapokuja suala la uzuri, kwa hiyo wanakuwa na matumaini kwamba, watajiwezesha kuwa wazuri kwa kadri siku zinavyosonga. Usishangae sana, shusha pumzi kasha utulie. Kumbuka huu ni utafiti tu, ambao umefanywa na watafiti.
Tunakutakia siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.