Jul 26, 2016
Hatua Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.
Ili
biashara yako iweze kukua na kukupa mafanikio ni lazima ipitie katika hatua nne
muhimu. Hizi ni hatua ambazo biashara yoyote ile, ili iweze kuleta mafanikio, ni
lazima ipitie hapo bila kuruka hata hatua moja.
Kama
ulivyo umuhimu wa hatua za malezi kwa mtoto kuanzia kutambaa hadi kukimbia na
pia hatua hizi ni muhimu katika mafanikio ya biashara hivyohivyo. Ikiwa ikatokea
hatua moja imerukwa ni rahisi kwa
biashara husika kupoteza mwelekeo au kufa kabisa.
Mpaka
hapo bila shaka utakuwa umeona ni kwa jinsi gani hatua hizi zilivyo za muhimu
katika kukua kwa biashara. Ni hatua ambazo zinampa mfanyabiashara uzoefu wa
kukua siku hadi siku na kupelekea biashara kuleta mafanikio mkubwa.
Je,
hatua hizo ni zipi?
Zifutazo Ni Hatua
Nne Za Kukua Kwa Biashara Yako.
1.
Hatua ya mbegu (Seed stage).
Katika
hatua hii, mara nyingi mjasiriamali anakuwa yupo katika hatua ya kujaribu wazo
la biashara yake kama linafanya kazi au la. Ni hatua ambayo humfanya
mjasiriamali ajaribu mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya kuchunguza soko jinsi lilivyo.
Pia
hii ni hatua ambayo biashara kwa namna yoyote ile huhitaji pesa ili iweze
kusonga mbele. Kwa kifupi hii ni hatua inayohitaji umakini sana kwa sababu ndio
msingi na mwanzo wa mafanikio wa hatua zingine zinazofuata. Ikiwa umakini
utapotea hapa ni lazima biashara ife.
2.
Hatua ya kuchipua ( Start-up stage).
Baada
ya kujaribu wazo lako na kuona wazo linafanya kazi, hatua inayofuata baada ya
hapo ni hatua ya kuchipua kwa biashara. Hii ni hatua ambayo sasa unaanza
utekelezaji wa wazo lako. Ni hatua ambayo unakuwa unatafuta wateja wako
mwenyewe sasa.
Katika
hatua hii pia mjasiriamali, ni lazima ujifunze jinsi ya kupata mrejesho kwa
wateja wako. Ni lazima ufahamu wateja wako wanataka nini au hawataki nini ili kufanya maboresho.
Unapozidi kuwa makini katika hatua hii ni lazima idadi ya wateja wako
itaongezeka na biashara itakua pia.
3.
Hatua ya kukua ( Growth stage).
Mara
baada ya bidhaa zako kuwa sokoni, ikiwa utaona bidhaa zako zinatakiwa kwa
wingi, elewa kabisa hapo biashara yako hiyo ina dalili tosha ya mafanikio kwa
kukua.
Sasa
kaika hatua hii, hiki ndicho kipindi ambacho mjasiriamali anatakiwa kuanza
kuangalia ushindani na wafanyabiashara wengine. Ikiwa ikatokea umeweza kumudu
vizuri katika hatua hii, basi ni wazi mafanikio kwenye biashara yako ni lazima
yaonekane.
4.
Hatua ya kukomaa ( Maturity stage).
Hapa
katika hatua hii, biashara yako inakuwa imemudu kuweza kukabiliana na ushindani
wa kila aina. Hiki ni kipindi ambacho biashara yako inakuwa inajitatanua na
kutengeneza matawi katika sehemu zingine tofauti.
Kwa
kifupi, hii ni hatua ambayo mjasiriamali anayaona mafanikio yake kwa sehemu
kubwa. Lakini hata hivyo ni hatua ambayo mjasiriamali pia hatakiwi kulewa zaidi
ya kuendelea kuweka juhudi hadi kufanikiwa zaidi na zaidi.
Kumbuka,
hizo ni hatua muhimu nne ambazo biashara yako ni lazima ipitie ili iweze kukua
na kukuletea mafanikio. Hata hivyo, hizi ni hatua ambazo zinategemeana sana. Kushindwa
kwa hatua moja, ni dalili tosha inayoonyesha pia na hatua zingine zitashindikana
kufanikiwa.
Kitu
cha kujiuliza wewe upo katika hatua ipi? Kwa hatua yoyote uliyopo itakusaidia
kujua kama utafanikiwa au la!
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.