Sep 24, 2021
Jinsi Ya Kupata Wazo Bora La Biashara.
Kisaikolojia kila mtu ana mawazo bila
kujali ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine binadamu huwa na mawazo mazuri
ambayo kama atayaendeleza na kuyafanyia kazi yanaweza kubadili kabisa maisha
yake.
Mawazo humfanya mtu awe alivyo, aonekane
vile anavyoonekana. Mwenye akili, mpole, mkorofi,mwema au mkatili. Haya yote ni
matokeo ya mawazo aliyonayo mtu kichwani mwake.
Kila siku tunasikia watu wanasema
nina pesa ila sijajua nifanye biashara au mradi gani. Wakati mwingine utasikia mtu
akisema nina wazo zuri la kufungua biashara au mradi tatizo langu mtaji sina.
Katika kuwaza kwao watu hawa mwisho
hujikuta muda umeenda, umri umesonga bila hata kutekeleza wazo moja alilopanga.
Mwenye pesa amekaa na pesa hadi imekwisha
kwa kutatua matatizo ya aina mbalimbali.
Mwenye wazo kawaza mpaka kawazua
mtaji hana na wazo limechina mwisho anakata tamaa na kuamua kufanya kazi
asiyotaraji kuifanya ili kujikimu na mahitaji ya kila Siku katika maisha.
Ni Kitu gani kifanyike ili watu hawa
waweze kufanikiwa? Mwenye wazo na mwenye pesa? usiumize kichwa Kisuda nitakupa
siri yake leo. Kabla sijaeleza namna gani ufanye nikudokezee siri moja muhimu katika
mafanikio.
Tafuta wazo sahihi la kukufanikisha. |
Ili mtu yeyote iwe mimi au wewe uweze
kufanikiwa unahitaji vitu vinne.
1. MAARIFA/UJUZI juu ya jambo
unalotaka kufanya.
2. WAZO BORA NA ZURI la
kukuongoza hatua kwa hatua lenye taarifa sahihi juu ya mradi au biashara
husika.
3. WATU WAZURI wa kushirikiana nao.
Hakuna kazi au mradi unaoweza kuufanya peke yako ila kushirikiana na watu. Hivyo
ni lazima upate watu makini na sahihi wa kushirikiana nao.
4. MTAJI /PESA ya kuanzishia mradi
lakini zingatia kuwa pesa si chochote katika mradi au biashara hata uwe na
mamilioni ya shilingi kama huna hivyo vitu vingine wazo,maarifa na watu sahihi
sahau kuhusu MAFANIKIO utaangukia pua tu.
Kisaikolojia pesa haileti
mawazo, bali mawazo ndiyo huleta PESA. Na hii ndio Imani yangu na falsafa yangu
Kisuda katika maisha yangu ya mafanikio.
Sasa nitoe njia 5 za kuweza kukusaidia
wewe rafiki yangu katika kupata wazo la biashara ili uweze kufanikiwa kirahisi
kwa wewe mwenye pesa na mwenye wazo:-
1.Tafuta uhitaji wa watu/ tatizo
linalowasibu watu kisha tafuta namna ya kuwatatulia shida /tatizo lao utapata
pesa nyingi sana.
2. Boresha wazo la mwingine. Hapa ni
kuangalia tu mapungufu ya mtu katika kazi au biashara halafu una boresha
utendaji kazi na utaona mabadiliko makubwa katika kazi au biadhara yako. Kamwe
usiige wafanyavyo wengine utapata matokeo yaleyale wapatao wao badili njia.
3. Hamisha wazo kutoka sehemu moja
kwenda nyingine. Hapa na maanisha ukiona mradi au biashara sehemu si lazima
nawe ukafanyie pale unaweza anzisha wazo kama hilo sehemu tofauti na
ukafanikiwa sana.
4. Rahisisha mchakato au upatikanaji
wa huduma au bidhaa fulani badala ya watu kuifuata sokoni au mjini wapelekee
wewe nyumbani kwao watakulipa pesa nyingi na gharama ya usafiri kwa nini
wakulipe? Umewaokolea muda wao ili wafanye mambo mengine na pia wamepata
wanachotaka kwa wakati.
5. Tengeneza uhitaji kwa watu. Hapa
ni kubuni Kitu cha ziada ambacho watu wanakihitaji lakini kutokana na muda au
umbali wanaona kama hakina umuhimu sana kwao. Mfano simu za mkononi zimekuja
baada ya barua kuonekana kuchelewa kuwafikia wahusika leo hii taarifa ya dakika
10 imeshasambaa nchi nzima.
Haya sisi wataalamu tunaita ni
kutengeneza mahitaji ya ziada kwa watu ili wakulipe pesa. UWEZO WAKO WA KUJA NA
MBINU AU WAZO JIPYA TOFAUTI NA MAZOEA YA WATU NDIO CHANZO CHA MAFANIKIO YAKO.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Hongera kwa kuendelea kutuelimiksha
ReplyDeleteAsanteni xna
ReplyDeleteNashukuru japo ningehitaji kuwasiliana nawe
ReplyDeleteAu 0744017311
Shukran
ReplyDelete