google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 20, 2016

Mfumo Bora Utakao Badili Maisha na Biashara Yako.

No comments :
Kila utayekutana leo endapo utamuuliza unapenda nini katika maisha yako? Jibu ambalo atakupa bila shaka litakuwa linahusiana na masuala ya mafanikio na endapo utakutana na mtu ambaye majibu yake yatakuwa ni  kinyume na  mafanikio ni lazima utabaki unamshangaa huyu mwenzangu vipi? .
Bila shaka idadi ya watu wengi ni kuona kila mmoja anapata mafanikio ila tatizo ni pale linapokuja suala zima unapataje Mafanikio hayo. Tulio wengi ni wazuri wa kunuia (kusema ) kuliko kujua tunapaje Mafanikio hayo.

Leo niamua kuwaza kwa sauti hata wewe mwenzangu usikie nilichokiwaza ili uweze kupata mafanikio hayo na sio kuishia kusema nataka kile bila hata kujua utakipata vipi.

Zifuatazo ndizo mbinu zitakazobadili mfumo wa Maisha yako;


1. Usijadili vitu kwa macho.

Katika safari ya kuelekea au kupata mafanikio hakuhitaji kuvitazama tu vitu bali ni lazima ufanye uchunguzi wa kutosha. Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule hasa somo la hesabu wengi wetu tulikuwa tukiyatazama maswali tulikuwa tunasema haya yameisha kwa maana ya kwamba uhakika wa kupata majibu ya maswali hayo upo wazi, lakini kinyume chache baada ya kusema hivyo tulikuwa tunakosa na kufeli somo hilo kwa sababu tulikuwa wazuri sana wakuona na kusema kuliko kutenda.

Jaza kichwa chako mawazo chanya.
Mfano huu ndivyo unavyoendelea mpaka leo hii kwa watu wanaotaka kupata mafanikio. Wengi wao hutumia macho tu na kujipa majibu kwamba watafanikiwa. Kwa mfano mtu anataka kufungua biashara mahali fulani kwa kuwa anatumia macho peke yake katika kuona, anaona wafanyabiahara wengine wanafanikiwa na yeye kwa kutumia uzoefu wake wa kuona tu hujikuta na yeye kaanza biashara mara moja.

Lakini inapotokea pale mtu huyo ambapo biashara hiyo haitakwenda vizuri utamsikia mtu huyo anasema karogwa ila ukweli hakuna atakayekuwa amekuroga zaidi ya kujiroga mwenyewe. Pia daima kumbuka kuona peke yake haitoshi bali uchunguzi wa kina huhitajika kwa jambo ambalo unataka kulifanya.

2. Kujaza kichwa chako mawazo chanya.

Mawazo chanya ni mawazo yatakayokufanya uweze kutoka hatua moja hadi nyingine ya kimafanikio. Swali dogo la kujiuliza kabla siku mpya haijaisha, je huwa unajiuliza ni mawazo gani chanya ambayo umewaza kutwa nzima? Na umeyachukulia hatua kwa kiasi gani? Na kama umechukulia hatua yana uwezo gani wa kubadili maisha na kinyume chake ni vipi.


Nikumbushe tu ya kwamba moja ya sifa ya watu wenye mawazo chanya kwa kile ambacho anakiwaza hukiandika katika kumbukumbu huku utekelezaji ukisubiri kuanza mara moja. Mawazo chanya ndiyo ambayo humbadilisha mtu siku zote na mawazo hasi ndiyo ambayo yamekuwa yakiwafanya watu waishi mawazo ya umaskini kila siku.


Mara nyingi mtu huanza kuwaza maamuzi mazuri ila namna ya kutekeza ndiyo huja mawazo hasi ya utekelezaji, Kwa mfano mtu anawaza kuwa mfanyabiashara mkubwa wa maduka ya nguo ndio hayo ni mawazo chanya lakini mawazo ya utekelezaji jambo hilo yanakuja mawazo mabaya kama vile tumia njia za kishirikiana hapo utafanikiwa. Baada ya hapo kwa kuwa mtu huyo baadala ya yeye kuiongoza akili yake ila yeye anaongozwa na akili yake mwisho wa siku anaingia katika kutekeza jambo lake kwa njia zisiso rasmi na mwisho wa siku anakuwa maskini maisha yake . Badili mtazamo na waza chanya ama hakika utafanikiwa.

Nukuu  ya leo inasema ; Hakuna Binadamu aliyeletwa duniani kuzurura.

Imeandikwa na Afisa Mipango; Benson Chonya.
Simu ;0757-909942
E-mail:
bensonchonya23@gmail com

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.