Mar 24, 2016
Vipindi Muhimu Anavyopitia Mwanadamu Katika Maisha.
Katalamu binadamu katika safari
ya ukuaji hupitia vipindi mbalimabali. Katika vipindi hivyo binadamu kwa muda
mwingine huwa na furaha,huzuni,wasiwasi na hofu pia. Pia ni hivi ndivyo vipindi
ambavyo humsaidia kujifunza mambo mabalimbali ikiwa pamoja na tabia na
mafanikio.
Hebu twende pamoja kujua na
kujifunza Vipindi hivyo ni;
Umri
wa mwaka (0-18).
Katika kipindi hiki binadamu huwa
mtoto na anayependwa sana na wazazi wake, katika kipindi hiki mwanadamu anakua
katika kipindi cha kufundishwa vitu
kutoka kwa watu mbalimbali. Mfano mtoto mdogo katika hali kwa kila anachokifanya
kwake huona ni sawa eidha ni jema au baya.
Mzazi huchukua jukumu la
kemkekemea kama anafanya jambo baya na humpongeza pale anapofanya vizuri. Mfano
mtoto hupongezwa kumsaidia mzazi kufanya kazi, kuwaheshimu watu
wote, kufaulu katika masomo yake na mengineyo mengi. Kiujumla katika kipindi
hiki binadamu huwa ni tegemezi kwa jamii inayomzunguka.
Kipindi
cha umri kati miaka (19-35).
Katika kipindi hiki binadamu
huanza kujitambua yeye ni nani.Vilevile katika kipindi hiki ni kipindi ambacho
binadamu anaanza kupanga mipango mingi. Mfano katika kipindi hiki mtu huanza
kupanga mambo mbalimbali nataka katika maisha yangu kitu cha kwanza kuwa nacho
ni gari, mwingine utamsikia mimi nataka nianze kuwa na nyumba, wengine utasikia
nataka kuolewa na mtu mwenye pesa, wapo wengine utawasika nataka kuoa mwanamke
mzuri na mipango mingine mingi.
Katika kipindi hiki utawasikia wanasema ndio kipindi cha kula ujana wakiwa na
maana ya kwamba ni kipindi cha kwenda kumbi mbalimbali za burudani, pia ni
kipindi cha kupendeza, pia ni kipindi cha vijana wengi kujiingiza katika kuiga
mikumbo kutoka kwa watu mbalimbali hatimaye kujiingiza kwenye wizi,kuvuta
bangi,umalaya na mengineyo mengi. Utawasikia wengine wanakiita kipindi cha
tumia pesa ukuzoee.
VIPINDI VYOTE NI MUHIMU SANA KATIKA MAISHA. |
Dah yaani ni kipindi hiki kina
mambo mengi sana. Katika kipindi hiki tupo baadhi ya watu huwa bado wapo katika
kipindi cha utegemezi. Mfano mzuri ni wanafunzi wanasoma elimu za juu yaani
vyuo wao huamini ya kwamba hawawezi wenyewe kusimama na kujitengeneze njia
sahihi ya kujipatia kipato.Pia wanafunzi hawa kwa walio wengi huwa wanafikiri
maisha baada ya elimu zao ni kuajiriwa.
Lakini ndugu msomaji wa makala
hii lazima ufikiri zaidi kuajiriwa peke yake ili uweze kuona mafanikio makubwa
ndani yako. kitu kikubwa ni kuwa mbunifu.Wito wangu kwako ni kwamba endapo
utatumia vizuri kipindi hiki ukiwa na mtazamo chanya utapata mafanikio makubwa
sana.
Umri
kati miaka (36-45).
Ni aina nyingine ya vipindi
ambayo hupitia mwanadamu. katika kipindi hiki ni kipindi cha utekelezaji wa yale
uliyoyapanga katika kipindi ulichopita yaani cha miaka( 19-35). Katika kipindi
hiki ni kipindi ambacho kina majukumu
mengi ambayo yanamfanya mtu akose hata usingizi. Katika kipindi hiki mtu huwa
na majukumu mengi sana kwa mfano kujenga, kusomesha watoto,huenda ukawa tegemeo
katika familia yako.
Kwa kuwa katika kipindi hiki kina
mambo mengi ya utekelezaji ni vema kile unachokipanga katika kipindi cha
mipango yaani miaka (19-35) na utekelezaji uanza katika kipindi hicho. Nasema
hivi nikiwa na maana ya kwamba katika kipindi hiki cha miaka 36-45 watu wengi hujikuta wana mipango
mingi lakini ugumu unakuja katika utekelezaji.
Umri
kati ya miaka 46-na kuendelea
Hiki ni kipindi cha uzee ambacho
mara nyingi huiitwa ni kipindi cha masahihisho. Katika kipindi hiki baadhi ya
watu hupungua uwezo wa kufikiri hatimaye kuwa kama watoto. Pia Watu wengi hapa
hupatwa na magonjwa mbalimbali kama pressure,figo kufeli, kisukari na
mengineyo. Katika kipindi hiki watu hustaafu kazi zao. Katika kipindi hichi
watu wengi hupatwa na pressure kutokana na walishindwa kupanga na kutekeleza
mambo yao katika vipindi vya umri kati (19-35).
Mfano mtu alikuwa ni mfanyakazi
wa serikali na hajawahi kujenga nyumba yake ya kuishi wala hana usafiri vyote alivyokuwa anatumia
vilikuwa ni mali za ofisi. Inafika wakati wa kustafu anapata mafao yake ndo pale
anaanza kupanga mipango yake na kujikuta hela aliyopewa katika kiunua mgongo
imeisha kwa sababu mtu huyu anakuwa ana mipango mingi katika kipindi cha uzee
matokeo haelewi aanze na kipi katika
utekelezaji. Je, aanze na kununua gari? Je aanze na kufungua biashara? Je aanze
na kujenga nyumba? Matokeo yako mipango inakuwa mingi kuliko utekelezaji hatimaye
anapata pressure.
Wito wangu kwako kumbuka siku
zote kupanga ni kuchagua na kutenda ni
kuamua. Katika safari ya mafanikio kila linalowezekana leo lisingoje kesho. Ewe
kijana tambua ya kwamba muda wa kupanga na kutekeleza mambo yako ni sasa achana
na usemi eti kijana ni taifa la kesho kwa kuwa ukiushika usemi huo utakuwa unachelewa katika safari yako mafanikio.
DIRA YA MAFANIKIO inakutakia kila
jema katika safari yako ya mafanikio. Pia endelea kutembelea ukurasa huu kila siku ili ujifunze zaidi
kuhusu mbinu mbalimbali za mafanikio.
Imeandaliwa
na;
Afisa
mipango na maendeleo:Benson .O. Chonya,
Mawasiliano;
Simu;0757-909942/0652-015024
E-mail;bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.