Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, January 7, 2016

Jifunze Kuyafurahia Maisha Yako Wakati Wote.

No comments :
Ni mara nyingi wengi wetu huwa tunakutana na matatizo, shida na changamoto za aina mbalimbali katika maisha yetu. Kwa kawaida tunapokutana na changamoto hizi wengi wetu huishia kukata tamaa na kufikia mahali kuyachukia maisha na kuyaona hayafai na hayana maana tena.
Hiki ni kipindi ambacho kwa wengi wanapopitia hapa, kila unapokutana nao nyuso zao zinakuwa zimejikunja na kujiona hawafai na maisha hayawatendei haki. Kitu pekee ambacho wanakuwa wamesahau kuwa ni kwamba dunia hii haina usawa kama wanavyofikiri. Dunia haijui kama una matatIizo au huna.
Siri ya kukusaidia kuweza kuishi maisha ya ushindi na furaha ni kwa wewe kuweza kuyafurahia maisha yako wakati wote. Haijalishi unapitia katika hali gani, lakini lilokubwa kwako na la maana ni kuchagua kuishi maisha ya furaha. Kwa hali yoyote uliyonayo hata iwe ya mateso vipi itaisha tu.

Hakuna atakayekufanya uwe na furaha zaidi yako. Chagua kuishi maisha ya furaha. Kama imetokea mtu amekuuzi, kitu kimekukera, mipango yako haijaenda sawa, achana na mawazo ya kukereka. Jifunze kuwa na tabasamu nyakati zote. Siri ya kuyafurahia maisha yako itakusaidia kuyaona maisha kwa uzuri wake badala kuyaona kwa upande wa ubaya tu.
Hivyo tambua kwa namna yoyote ile unalo jukumu kubwa sana la kuyafurahia maisha yako kila siku. Usiruhusu mambo madogo madogo sana ya kakuchukukulia furaha yako. Jifunze kumudu na kutawala biashara yako, utaishi maisha ya ushindi mkubwa sana.
Tunakutakia siku njema, karibu na endelea kujifunza kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment