Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, January 18, 2017

Ukizingatia Vizuri Maamuzi Haya, Yatabadilisha Maisha Yako Kabisa.

No comments :
Si kile kinachokutokea sasa au kile kilichotokea jana ndicho kinachoamua maisha yako ya kesho yatakuwaje. Kitu kinachoamua maisha ya kesho yakuwaje kipo kwenye maamuzi yako.
Kwa sababu ya maamuzi, hapa ndipo unaweza kujua kama kweli unaweza ukafa maskini au ukafa ukiwa ni mtu mwenye mafanikio. Wengi huwa ni watu ambao hawazingatii sana kuhusu maamuzi yao.
Kutokana na maamuzi ieleweke kwamba ndio hupelekea wengine kuwa na maisha mazuri na wengine kuwa na maisha ya hovyo. Na maamuzi tunayo yazungumzia hapa yamegawanyika katika sehemu tatu.
1. Maamuzi ya kile unachokizingatia.
Kitu unachoamua kukizingatia katika akili yako mara kwa mara ndicho kinachokufanya ufanikiwe au ushindwe. Huwezi kufanikiwa kama kila wakati unafanya maamuzi ya  kuzingatia mambo ambayo hayakusaidii.
Siri ya kuweza kufanikiwa ipo kwenye kuweka nguvu yote ya mawazo kwa kile kitu unachokitaka kwenye maisha. Kwa hili hakuna ubishi usipofanya maamuzi hayo huwezi kufanikiwa.
Ukizingatia Vizuri Maamuzi Haya, Yatabadilisha Maisha Yako Kabisa.
Fanya maamuzi ya kufanya kilichobora kwako, upate matokeo bora.
2. Maamuzi ya kile unachokifanya.
Kila wakati unahitaji kufanya maamuzi ya kile unachotaka kukifanya. Kile ambacho umechagua kukifanya hicho ndicho kinachoamua maisha yako kuwa bora au ya hovyo.
Hebu kila wakati jiulize je, unafanya maamuzi sahihi hasa kwa kile unachokifanya? Au unafanya maamuzi ambayo hata wewe mwenyewe ukiangalia tena yanakuwa yanakuumiza kwa namna fulani?
3. Maamuzi ya jinsi unavyotafsiri mambo.
Pia yapo maamuzi ya jinsi unavyopokea mambo. Kwa mfano, unapokuwa umeshindwa kichwani mwako huwa unapokea vipi taarifa hizo au pengine huwa unajisikiaje.
Ili kufanikiwa jifunze kuchukua maamuzi ya kutafsiri mambo au taarifa kwa chanya zaidi. Unapokuwa unatafsiri mambo kwa chanya itakufanya uweze kufanikiwa, kwa sababu utakuwa unafanya maamuzi bora.
Kwa kifupi, haya ndiyo maamuzi ya msingi sana kwa mtu yoyote anayetaka kufanikiwa. Mafanikio au kushindwa kwa namna yoyote ile msingi wake mkubwa unatokana na mamauzi hayo ambayo umejifunza.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
No comments :

Post a Comment