Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, February 15, 2017

Usikatishe Ndoto Yako Kwa Sababu Tu Ya Maneno Ya Watu.

No comments :
Inabidi tukubaliane kwamba, kupata mafanikio sio kazi rahisi kunahitaji nguvu na jitahada nyingi sana hadi kufikia kule unakotaka kufika kimafanikio.
Kuna wakati utakatishwa tamaa, kuna wakati utaambiwa huwezi hili au lile, lakini yote hayo yanapotekea yasikukatishe tamaa jipe moyo na endelea kusonga mbele. 
Hata Jesca Cox, alikatishwa sana tamaa na wengi na kuambiwa asingiweza kutumiza ndoto yake ya kuwa rubani eti kwa sababu ya ulemavu wake wa mikono.
Leo hii, Jesca ni rubani wa kwanza duniani ambaye hana mikono, je, jiulize nini kinachokukwamisha wewe? Endelea kupambana na songa mbele.

Usikatishe ndoto yako sababu ya maneno ya watu.
Kwa sababu unajenga maisha unayoyataka hata kama unapata matokeo usiyoyataka hasa kwa kile kitu unachokifanya, acha kujiona mnyonge na kukata tamaa, endelea kuweka juhudi.
Ikiwa unapitia kwenye changamoto nyingi za kimaisha pia acha kukata tamaa, endelea kuweka juhudi upo wakati ambapo utazivuka hizo changamoto hizo na kuwa huru.
Ikiwa huridhiki kabisa na mwenendo wa maisha yako na kujiona kila wakati kama mtu ambaye umepoteza, pia usikate tamaa, endelea kuweka juhudi.
Kwa kila hatua unayochukua kwenye maisha yako hata ikiwa ndogo sana, inaleta mabadiliko kwenye maisha yako. acha kuwasikiliza watu eti kwamba umeshindwa.
Angalia ulikotoka kwenye maisha, sasa kwa nini ukate tamaa na wakati sasa hivi upo mbali sana? Dawa si kukata tamaa ni kuweka juhudi tena.
Hata upate matokeo mabaya vipi ambayo unaona hayakuridhishi kabisa endelea kuweka juhudi, kwani lazima juhudi zako zitaleta matunda.
Hakuna mtu katika dunia hii ambaye ameweka juhudi endelevu, halafu zikaja kumwangusha, mtu huyo hayupo.
Hivyo, hata ushindwe mara nyingi vipi, endelea kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, kwani upo wakati mabadiliko hayo utayaona kwa wazi kabisa, hata kama kwa sasa  huyaoni.
Kila hatua unayoichukua, kumbuka inakusogeza karibu kabisa na mafanikio yako. usikubali hata kidogo kupotezwa na maneno ya watu. Chukua hatua sahihi, ili ufikie mafanikio yako.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja tena kwa ukaribu. Kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

No comments :

Post a Comment