May 31, 2017
Zijue Faida Za Kumheshimu Kila Mtu Katika Kazi Yeyote Uitendayo.
Hapo
zamani za kale kulikuwako na mfalme mmoja ambaye alijulikana kwa jina la
mhavila. Mfalme huyu alikuwa na utu sana kwa watu wake. Japo kutokana na
majukumu yake ya hapa na pale ilikuwa ni ngumu sana kwake kuonana na watu
wake mara kwa mara.
Kila
mwakijiji wa jamii ile alitamani sana kukutana uso kwa uso na mfalme mhavila,
kwa kukuwa mfalme huyu alikuwa ni mtu mcheshi sana kwa watu wake. Siku moja
mfalme mhavila aliandaa mkutano mkubwa sana ambapo kila raia wa eneo lile
alihudhuria katika mkutano ule.
Watoto
kwa wakubwa, vijana kwa wazee wote walimiminika katika mkutano ule. Mfalme
mhavila aliwaeleza watu wake mambo mbalimbali ambayo kimsingi yalikuwa yana
manufaa sana katika kufanikisha masuala ya
maendeleo ya jamii na maendeleo ya watu hao kwa ujumla.
Mara
baada ya mkutano kuisha mfalme mhavila alikutana na mtu mmoja ambaye alikuwa ni
mjane, mjane huyo alionekana kwa macho ni maskini wa kutupwa, tunaweza kusema
hivyo hii ni kutokana na muonekano wake. Mjane yule alimtazama mfalme mhavila
kwa macho yenye kutia unyonge sana, baada ya dakika chache ndipo mjane yule
akafungua kinywa chache na kusema;
‘’samahani
mfalme mhavila kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta nafasi ya kuzungumza na wewe
ila kwa bahati mbaya nafsi hiyo sikuweza kuipata, ila kwa siku ya leo nina kila
sababu ya kumshukuru Mungu wangu kwa sababu tumeweza kukutana.
Kabla
ya mfalme hajainua kinywa chache mjane akandelea kusema ‘ nafahamu ya kwamba
upo bize na shughuli za hapa na pale, na unafanya hii yote kwa sababu ya
kusongesha kurudumu hili la maendeleo, kwa kufanya hivyo nikupongeze sana kwa
sababu kila mwenye macho na maskio anakiona na kukishuhudia kwa kile ambacho
anakifanya.
Mfalme
mhavila baada ya kusikia vile moyo wake ulikwenda kasi kidogo, hii yote ilikuwa
ni mshangao wa kile ambacho mjane alichokuwa amemueleza, mfalme mhavila aliwaza
kidogo, kisha akatafakari ndani ya nafsi yake. kisha mfalme mhavila akajibu
asante sana mama kwa kutambua mchango wangu kwa kile nikifacho, kwa kweli
nakushukuru sana.
Wakati
watu wengine wakishangaa na kujihoji mama mjane na mfalme walikuwa wanazungunza
nini, hakuna aliyepata majibu.
Hivyo
mara ya sekunde chache mama mjane akamwambia mfalme mhavila ‘’ samahani mfalme
mhavila nafahahamu ya kwamba una majukumu mengi sana, ila naomba jioni ya leo
uje tule kwa pamoja chakula cha jioni
nyumbani kwangu.
Mara
baada ya mama mjane kuzungumza hayo, mfalme mhavila akainua kinywa chake na
kusema “ nashukuru sana mama kwa maneno yako yenye kunitia nguvu za kiutendaji
wa kimaendeleo, kwani ulichokisema kimenipa fikra mpya za kuleta mbadiliko
mapya ya kimaendeleo, hivyo nakuahidi siku ya leo tutajumuika kwa pamoja katika
kupata hicho chakula cha jioni kwa pamoja.
Baada
ya mazungumzo hayo mfalme mhavila na mama mjane waliagana na kuahidiana kukutana
hiyo jioni kama ilivyopangwa. Mama mjane
alielekea nyumbani kwake kwa ajili ya kuandaa chakula hicho. Baada ya
dakika chache chakula hicho kilikuwa kipo tayari, hivyo mama mjane akaweka chakula
hicho mezani kwa ajili ya kuliwa. Mama mjane alimsubiri mfalme kwa muda wa saa
nzima, lakini cha ajabu ni kwamba mfalme mhavila hakufika .
Mama
mjane hakuchoka kumsubiri mfalme mhavila kwani alimini atakuja kama ambavyo
walivyokuwa wapenga, muda ilizidi kwenda laikini mfalme hakuonekana kufika.
Hivyo mama mjane akaamua kufunga mlango wake
kwa kuwa muda ulikuwa umeshakwenda.
Ilipita
nusu saaa tangu mama mjane afunge mlango wake lakini cha ajabu mfalme mhavila
hakutokea, wakati mama mjane anatafakari ni nini ambacho kitakuwa kimemsibu
mfalme mhavila ghafla akasikia mlango ukigongwa. Mama mjane aliinuka mahali alipokuwa
ameketi na kuelekea mlangoni kwa ajili ya kufungua.
Kabla
mama mjane haujaufungua mlango , mama mjane alifurahi sana kwani aliaamini
aliyekuwa amegonga mlango alikwa ni mfalme mhavila. Taratibu mama mjane
akashika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kuufungua mlango. Mara baada ya
kufungua alistajabu kumbe aliyekuuwa akigongo mlango hakuwa mfalme mhavila bali
alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anatokwa na jasho sana. Hivyo yule kijana
hakupoteza muda, alimsabahi mama mjane kisha kueleza shinda yake moja kwa moja.
Kijana yule akasema samahani mama nimetoka mbali sana sehemu ambayo ni jangwani
, hivyo nimetembea muda mrefu bila kunywa maji, hivyo naomba unisaidie niweze
kupata maji ya kunywa.
Mama
mjane alipatwa na hasira kidogo kwa sababu alitegemea ambaye aligonga mlango
huenda alikuwa ni mfalme mhavila. Basi mama mjane alimtazama yule kijana kisha
akelekea ndani na kuchua maji ambayo alikuwa amemuandalia mfalme mhavila na
kumpa yule kijana.
Mara
baada ya yule kijana kunywa yale maji alimshukuru mama mjane, kisha kijana yule
akaondoka. Mama mjane alirudi ndani kwa ajili ya kumsubiri mfalme. Lakini cha
ajabu mfalme hukuweza kufika. Mama mjane alitafakari na kusema haiwezekani ni
kwanini mfalme hakuweza kutimiza ahadi?
Wakati
akitafakari hayo mara akasikia tena sauti ikitokea mlangoni, mama mjane
alifurahi sana kusikia sauti ile
ikibisha hodi kwani nafasi hii aliamini yule aliyekuwa akibisha hodi alikuwa ni
mfalme mhavila. Hivyo pasipo kupoteza muda mama mjane alielekea mlangoni kwa
ajili ya kumfungulia mfalme mhavila.
Mara
baada ya kufungua mlango ailikutana na mtoto mdogo ambaye mama mjane hakuweza
kumfahamu mtoto yule, mama mjane alijaribu kuvuta taswira ni wapi ambapo
aliwahi kumuona mtoto yule, mama mjane alikosa majibu kwani mtoto yule alikuwa
ni mgeni machoni pake.
Mtoto
alimsabahi mama mjane kisha akasema “ samahani mama yangu nimetoka nyumbani kwetu wazazi wangu
wameniacha tangu asubuhi, sijaweza kula chochote, hivyo naomba unisaidie
chakula niweze kula mama yangu, kwani naumwa na njaa sana mama.
Mama
alimtazama mtoto kwa macho yenye huruma sana, hivyo kwa kuwa muda ulikuwa
umeenda sana aliamini ya kwamba mfalme mhavila hawezi kufika kwake tena, hivyo
alichukua chakula ambacho alikuwa
amemuandalia mfalme mhavila na kumpa mtoto yule. Mtoto yule alikula na
kumshukuru mama mjane.
Mama
mjane alifunga mlango tena na kuamini ya kwamba mfalme mhavila asingeweza kuja
tena. Wakati akiwa ameketi ndani mwake mama mjane alisikia watu wakija uelekeo
wa nyumba yake wakiimba nyimbo nzuri na za kupendeza sana. Alitafakari kuna
nini? Wakati anazidi kutafakari sauti zile zilikuwa zinazidi kusogea katika
nyumba yake.
Mama
mjane alitoka nje ili kushuhudia kulikuwa kuna nini, ghafla alimuona mfalme
mhavila akiwa na umati mkubwa wa watu, mama mjane aliwaza atamueleza nini
mfalme mhavila kwani chakula alikuwa kakigawa chote. Mfalme mhavila alifika kwa
mama mjane na kusema asante sana kwa kunijali.
Mama
mjane aliwaza na kusema mfalme mhavila ananishukuru kwa lipi tena? Wakati sijamfanya
chochote?
Je mfalme Mhafavila alimshukuru mama mjane
kwa kipi hasa? Usikose itaendelea wiki ijayo siku kama ya leo,
Ndimi
afisa mipango Benson Chonya
0757909942
May 30, 2017
Fanyia Kazi Mambo Haya, Ili Kuendelea Kujenga Msingi Mkubwa Wa Mafanikio Yako.
1.
Zipo kelele nyingi sana katika dunia hii ya habari. Utasikia hiki mara utasikia
kile. Usipokuwa makini utajikuta kila kitu unataka kufatilia. Sasa njia ya
kuweza kujiokoa na kelele hizo na kuweza kufanikisha malengo yako ni kwa wewe
kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kile unachokifanya.
Angalia
kipi unakifanya, kisha kifatilie kitu hicho kila siku. Kelele za huku mara kule
acha kuzifatilia zitakupoteza. Kumbuka, mikwenzi mingi ilimpoteza mbwa
mawindoni, usiwe miongoni mwa watu watakao potea kwa sababu ya kelele. Simamia
na fatilia mipango yako kwa kuweka nguvu za uzingativu kwa kile ukifanyacho na
utafanikiwa.
2.
Maisha na mafanikio ya kweli yanakuja kwa wewe kuweka thamani na kutoa mchango
mkubwa kwa wengine. Mafanikio hayaji kwa bahati nasibu au chochote kile ambacho
kipo kwenye njia ya mkato. Mafanikio ya kweli yanatengenezwa sana na kwa wewe
kuendelea kuweka thamani na kutoa michango kwa wengine.
3.
Kila wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya
kile unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa.
Kupenda kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni
rahisi tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’
hasa kama unafanya kile unachokipenda.
Mara
nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama
hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala
hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango
uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.
4.
Wakati tukiwa vijana wadogo wengi wetu tulikuwa na ndoto nzuri sana kwamba
nikikua nitafanya hiki au kile na ilikuwa rahisi kuweza kuona kama vile kila
kitu kinawezekana na wala hakuna changamoto kubwa sana.
Lakini
kwa kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda zile ndoto zetu zilianza kupotea
hasa baada ya kukumbana na changamoto za kimaisha za hapa na pale. Kitu cha
kujiuliza kwako kwa mfano je, ile ndoto yako ya utotoni unayo au imepotea?
Kwa
vyovyote vile ilivyo ndoto yako ipo ila kikubwa ulichokifanya umeizika ndoto
yako bila kujua.Umeshindwa kufanya namna nzuri ya kuweza kuifufua ndoto yako na
kuiweka wazi hadi iweze kufanikiwa.
Sasa jiulize hivi kama huna mpango na ndoto yako
ambayo ulikuwa unapienda, kwa sasa unaishi maisha a aiana gani? Ni rahisi
kukwama katika maisha na kupata ugumu fulani kama hufuati ndoto yako na hufanyi
kile kitu unachokipenda maishani.
Kuanzia sasa jipe muda wa kufikiri tena na anza
kufatilia ndoto yako ile ambayo ulikuwa umeisahau. Kaa chini ujiulize una ndoto
ipi ambayo unatakiwa kuifailia? Kisha anza kuifatilia ndoto yako na itakuwa
kweli.
5.
Kuna wakati tunajiambia sana ‘mwaka huu nahitaji kuongeza mtaji, mwaka huu
nahitaji pia kufanya biashara ile, au mwaka huu nahitaji kufanya hiki au kile’.
Hizi ni sentensi ambazo naamini umezisikia sana zikisemwa na kuna kipindi hata
wewe umekuwa ukijisemea hivyo.
Katika
ulimwengu wa mafanikio ipo hivi kile kinachokufanikisha si kile unachokihitaji,
bali kile kinachokufanikisha ni kile unachokifanya au kukifanyia kazi, ndicho
hicho kinachokufanikisha na kukupa mafanikio.
Hakuna
atakayejali kwa kile unachohitaji au unakisema sana hata kiwe kizuri vipi,
dunia inajali kile unachokichukulia hatua na kukifanya. Hicho unachokifanya
kila siku, hicho ndicho kinachokusogeza kwenye mafanikio yako.
Unaweza
ukahitaji mambo mengi sana lakini kama huchukui hatua uwe na uhakika huwezi
kufanikisha kitu chochote katka maisha yako, zaidi yako utaishia kusema nahitaji
hiki au kile na miaka inaenda na bado ukajikuta hupati kitu.
Kuna
watu ambao ukiwachunguza karibu maisha yao yote ni watu wa kusema nitafanya
hiki mwaka huu au kile na hawafanyi. Maisha ya mafanikio hayataki ‘blaa blaa’
yanataka ufanye kitu yaani uchukue hatua za kimafanikio.
Kumbuka
unachokihitaji hakiwezi kukupa mafanikio unayoyataka kwa asilimia zote, acha
kulinga na kujidai kwa kile tu unachokihitaji, badala yake uelewe kabisa kile
unachokifanya hicho ndicho kitakachokupa maisha na mafanikio unayotaka.
6.
Kipimo cha mafanikio yako kipo kwako
wewe mwenyewe na wala hakipo kwa mtu mwingine. Njia pekee itakayokufanya uweze
kupima mafanikio yako ni kwa kwewe kuangalia hatua unazozipiga kulekea kwenye
mafanikio hayo.
Mafanikio
yako hayapimwi kwa kuangalia mafanikio ya mtu mwingine. Bali mafanikio yako
yanakuja kwa sababu ya zile hatua zako mwenyewe unazotakiwa uzipige kila siku
kuelekea kwenye mafanikio.
Unawezaje
sasa kujua kama umefanikiwa ikiwa hujilinganisha sana na wengine? Hilo ni
rahisi tu, ni kwa wewe kuangalia ni hatua gani umepiga ukijilinganisha na mwaka
jana au wakati uliopita.
Kumbuka
kila siku hili, chukua hatua kila siku za kuelekea kwenye kile unachokifanya.
Usijali wala usiangalie ikiwa unachukua hatua kidogo, kitu cha msingi chukua
hatua kwani hicho ni kipimo cha mafanikio yako.
7.
Kuna wakati tunakutana na ugumu sana katika kufanya vile tunavyotaka kuvifanya.
Kutokana na ugumu huo na kuna wakati huweza kujikuta hata tukitaka kuahirisha
kufanya mambo yetu. Kwa hali yoyote unayokutana nayo hata kama ni ngumu vipi,
hebu hicho unachotaka kukifanya kifanye.
Usiahirishe
mambo yako kwa sababu ya ugumu, fanya hivyo hivyo, ‘just do it,’. Weka
visingizio pembeni, usiwe kama mtoto mdogo ambaye kila kitu anasingizia.
Tengeneza ukomavu wa kiakili kwa kuamua kufanya hata kama ipo shida na ugumu
vipi wewe fanya kwa kusukuma na utaona mafanikio yakijitokeza kwako.
Nakutakia
siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza kila
siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713
04 80 35,
May 29, 2017
Umuhimu Wa Kujiongeza Katika Maisha Ya Mafanikio.
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, ni matumaini
yetu mazima u mzima wa afya tele na unaendelea vyema katika harakati zako za
kuweza kulisukuma gurudumu hili la maendeleo.
Ni siku nyingine tulivu ambayo sina budi nikukaribishe kwa moyo mkunjufu
tuweze kujifunza kwa pamoja.
Siku
ya leo nataka ttuzungumzie namna ambayo una uwezo mwingine wa kutenda jambo
jingine ambalo linaweza kukupa mafanikio makubwa kwa upande wako tofati na hilo
ulitendalo sasa. Unajua nataka tuzungumzie hili kwa sababu wetu wengi
hawafahamu uwezo mwingine walionao, ambao unaweza kuutumia ili uweze
kukamilisha jambo jingine ambalo Mwenyezi mungu kakujalia kulitenda.
Watu
wengi hudhani ya kwamba hicho ambacho wanakifanya ndicho ambacho wamepangiwa
kufanya. Kwa mfano mtu ni mfanyabishara fulani, labda huenda mtu akawa amesomea
kitu fulani, basi baada kuweza kubobea katika kipengekle hicho, basi anaweka
mipaka katika kitu hicho pekee.
Ongeza thamani ya biashara yako kila iitwapo leo. |
Ukweli
haipo hivyo hata chembe, kwani kila binadamu binadamu kaumbwa na uwezo mwingine wa kufanya vitu vingi
ambavyo vitaweza kumuinua kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ya
kimafanikio. Hata kanuni ya kufanya mazoezi ya mwili inasema ya kwamba huwezi
kutengeneza ‘six park’ kwa kufanya
mazoezi ya aina moja pekee kila wakati, bali unaweza kutengeza ‘six park’ kwa kufanya mazoezi ya aina
tofauti tofauti.
Kwa muktadha huo kama kweli unataka kufanikiwa
zaidi ya hapo ulipo sasa, unachotakiwa kufanya ni kuweza kutambua uwezo
mwingine ambao mwenyezi Mungu kakuwekea ndani yako, ili uweze kujipatia mkate
wako wa kila siku.
Hata
mwandishi mmoja aitwaye Antony Robbison aliwahi kuandika ya kwamba “if you do what you have done you will get
what you always gotten” hii ikiwa na maana “kama utafanya mambo yaleyale
ambayo umekuwa ukifanya siku zote,
utapata yale yele ambayo siku zote umeyapata”. Naomba urudie kusoma tena
aya hii ili uielewe vizuri.
Kwani
aya hiyo ipo wazi kabisa kama umezoea kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile basi
matokeo yake, yatakuwa ni yaleyale. Hivyo ili uweze kupata matokeo ya aina
tofauti na uliyoyazoea, unachotakiwa
kufanya ni kubomoa uzio wako wa kufikiri kwa kuanza kubadili ratiba ya kutenda
mambo yako ya msingi. Lakini pia ongeza uzio wa kufanya mambo yako kwani binafsi naamini una kitu kingine cha
kufanya zaidi ya hicho ambacho unakifanya.
Mwisho
nimalizie makala haya kwa kusema ukitaka kwenda mbali zaidi katika mambo yako
ya msingi acha kujenga uzio ambao utakufanya ushindwe kuona fursa
nyingine, bali unachotakiwa kufanya ni
kubomoa uzio huo ili uweze kuona fursa mbalimbali ambazo zimejificha, kwani
pindi unavyoacha ukuta huo ni kule kutengeneza uwezo wako wa kulalamika, na
mwisho wa siku kuelekea jehenamu ya umasikini.
Narudia
kwa kusema tena pale unaposhindwa kujiongeza ni kutengeneza jehanamu ya
umaskini. Usiogope na kusema afisa mipango anakutisha hapana, ila kazi yangu ni kukwambia ukweli ambao upo wazi, kwani nafasi
uliyonayo sasa unachotakiwa kufanya ni kuwaza ni namna gani utaweza kufika
mbali zaidi.
Kwani
umuhimu wa kujiongeza kunamsaidia mtu kuweza kuwa milango mingi ya kuweza
kufanikiwa zaidi. Pia faida nyingine ya kujiongeza humsaidia mtu kuweza kuwa mbunifu
zaidi kwa kile akifanyacho. Na ubunifu humsaidia mtu aweze kujilikana na
ukijulikana ndo mwanzo wa mafaniko yenyewe. Mpaka kufikia hapo sina la ziada
naomba kazi ibaki kuwa kwako kwa kuamua kwenda kuyatekeleza hayo ambayo nimekwambia. Asante.
Ni wako katika ujenzi wa mafaniko; afisa
mipango, Benson Chonya.
0757909942.
May 27, 2017
Mambo Muhimu Ya Kufanya Ili Kuitawala Biashara Yako Kwa Mafanikio.
Mafanikio
katika biashara ni kitu ambacho karibu kila mafanyabishara anataka kitokee
kwake. Wafanyabiashara na wajasiriamalia karibu wote, wana kiu na shauku kubwa
ya kutaka kuona biashara zao zikifanikiwa.
Hata
hivyo pamoja na kiu hiyo, lakini ukweli unabaki pale pale, kwamba suala la
kutawala biashara na ikakupa mafanikio si jambo la kubahatisha bali yapo mambo
ya muhimu ambayo wewe binafsi unatakiwa uyafanye ili biashara yako iweze kufanikiwa.
Bila
kupoteza muda, fuatana nami katika makala haya ili nikuonyeshe mambo ya msingi
ambayo unatakiwa kuyafanya katika biashara yako na kuifanya biashara hiyo ikawa
ya mafanikio makubwa.
1. Kubali kuwa mwanafunzi wakati wote.
Tafuta
maarifa kila siku ya kukusaidia katika biashara. Jifunze kuhusu washindi katika
biashara zao ni kipi wanachokifanya na hata wale wanaoshindwa ni kwa nini pia
wanashindwa. Kila unapojifunza hiyo inakupa nguvu ya kujiamini na kufanikiwa. Kama ulikuwa hufanyi hivyo hebu
anza sasa kujifunza zaidi juu ya biashara yako.
2. Chukua tahadhari kubwa kwenye biashara
yako.
Ili
biashara yako iweze kufanikiwa, unatakiwa kujua namna ya kuchukua tahadhari
kubwa kwenye hiyo biashara. Unatakiwa kuchukua tahadhari ya nidhamu binafsi
katika matumizi ya pesa na mambo mengi chungu nzima ya lazima ili kukuza biashara
yako. Ikitokea ukakosa tahadhari hizo si rahisi sana kuweza kufanikiwa kwenye
biashara.
3. Unahitaji kutengeneza mtandao mzuri
wa kibiashara.
Mara
nyingi biashara inakuwa na kustawi vizuri sana hasa pale kunapokua na mtandao
mzuri wa kibiashara. Hivyo ni vyema kujenga mtandao mzuri wa kibiashara na
wafanya biashara wenzako, hali ambayo itakupelekea kuweza kukua kimafanikio
katika biashara. Huhitaji kukaa kama kisiwa, jenga mtandao wa mafanikio ya
biashara yako.
4. Unahitaji kuchukua tafahadhari ya
afya yako.
Huwezi
kufanikiwa kwenye biashara au katika maisha kwa ujumla kama afya yako ni mbovu.
Unatakiwa kila wakati kuhakikisha afya yako inakuwa imara ili ikuwezeshe kufanya
mambo mengi yakayoweza kukusaidia kufanikiwa katika biashara kila wakati na kusiwe
na kipangimizi.
Kumbuka
haya ni mambo ya msingi sana ambayo unatikiwa uyazingatie kila wakati na
kuyafanya ii kuweza kuifanya biashara
yako ikawa ya mafanikio makubwa. Chukua hatua na fanyia kazi mambo haya.
Tunakutakia
siku njema na kila la kheri katiika kufikia mafanikio yako makubwa.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0628 92 9816,
May 26, 2017
Ijue Kanuni Halisi Ya Ubongo Wako.
Watalamu
mbalimbali wa masuala ya mafanikio wanasema ya kwamba kanuni ya akili yako
inatokana na ubongo wako, na katika ubongo wako inatokana na mawazo yako ambayo
kila siku unakuwa unayawaza. Swali dogo la kujihoji ni je kila siku huwa
unawaza nini?
Je mawazo yako huwa ni chanya? Au mawazo yako huwa ni hasi?
Kama
mawazo yako ni chanya ni hatua gani ambazo umekwisha kuzichukua mpaka sasa
ambazo kimsingi umekuwa ukijivunia? Majibu naomba ubaki nayo maana wewe ndiye
ujuaye.
Nawe
ndugu yangu ambaye kimsingi kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukiwaza mawazo
hasi, swali dogo ambalo unatakiwa kujiuliza kwanini umewekeza nguvu na akili
zako katika kufikiri vitu hasi ? naomba nawe mwenye tabia hii naomba majibu
usinipe.
Tumia kanuni halisi ya ubongo wako kufanikiwa. |
Nimeanza
kwa tafakari hiyo fupi ili tuone kwa
pamoja akili zetu tumezielekeza wapi? Na akili hizo hizo zinatupa matokeo gani
ambayo yapo maisha yetu ya kila siku?
Kwa
kuwa kama nilivyowahi kueleza hapo awali ni kwamba kanuni ya akili inasema ya
kwamba wewe ni matokeo ya mawazo yako, hii ikiwa na maana kila ambacho
unakiwaza katika mawazo yako ndicho ambacho kinachotokea katika hali halisi.
Hivyo
kama mawazo yako ni hasi, basi hata kile utakochokifanya basi matokeo yake
yatakuwa ni hasi, kama unawaza kutajirika kwa kuwa jambazi basi matokea yake ni
jiandae kufungwa. Maana akiwazacho mtu ndicho kitakochomtokea.
Mwisho
nimalize kwa kusema ya kwamba kama kweli umechoka hali uliyonayo hususani
masuala ya umaskini, jitahidi ufuate mfumo wa kufikiria chanya kila wakati, maana
matokeo ya mawazo chanya ni mafanikio ya kweli.
Asante
kwa kusoma makala hii naomba uweze kuwa bora kwa kuwa na mawazo chanya kila
wakati, kwani ukiwa hivyo mafaniko makubwa yanakuja kwa upande wako.
Ndimi
afisa mipango; Benson chonya,
0757909942.
May 25, 2017
Sababu Sita (6) Ni Kwanini Unatakiwa Kuacha Kutumia Sukari Kwa Wingi.
Kwa sasa vipo vyakula vingi
sana ambavyo vimekuwa na sukari na tunavitumia karibu kila siku. Kwa bahati
mbaya au nzuri vyakula hivi vya sukari vimekuwa vikipendwa na wengi bila ya
kujali madhara yake kiafya yakoje.
Wengi wetu hatujui sana
kiundani hasa pale tunapotumia vyakula vingi vya sukari, ni madhara gani ambao
yanaweza kukutokea zaidi, tumekuwa tukijua juu juu tu kwamba ukila vyakula vya
sukari vinaweza kukuletea shida hii au ile bila kuwa na uhakika sana.
Kwa sababu hiyo ndani ya
makala haya ya afya, tutakueleza kinagaubaga sababu ya msingi ni kwa nini
unatakiwa uache kutumia sukari kwa wingi mwilini mwako na ikiwezekana kuacha
kabisa baadhi ya matumizi ya vitu vyenye sukari nyingi sana.
1.
Sukari nyingi mwilini ni kisababishi cha magonjwa.
Matumizi ya sukari kwa wingi
ni chanzo kimojawapo cha kuongezeka kwa uzito, lakini si hivyo tu sukari
inapokuwa nyingi mwilini inaweza kukupelekea kupata magonjwa kama vile
magonyjwa ya moyo na kuongezeka kwa shinikizo la damu jambo ambalo ni hatari
kwa afya yako kwa kiasi kikubwa.
2.
Sukari nyingi mwilini inapunguza uwezo wa kuona.
Mara nyingi wanaoutumia
sukari kwa wingi sana au wale amabao viwango vya sukari vimeongezeka mwilini
mwao, moja ya madhara yake kwa baadae ni
kutokuona vizuri. Hilo hutokea kwa sababu, sukari inapokuwa nyingi hupelekea lensi ya
jicho kuongezeka na matokeo yake matatizo ya macho huanza kujitokeza kwa
mhusika.
Punguza matumizi ya sukari. |
3.
Sukari nyingi huozesha meno.
Bila shaka hili umeshawahi
kulisikia au kuliona. Na mara nyingi hutokea sana kwa watoto, meno huweza kuoza
baada ya matumizi ya sukari kwa wingi. Kinachotokea sukari huzalisha bakteria
wenye sumu ambapo hao huweza kuharibu meno na kupelekea kuweza kuoza kabisa.
4.
Sukari nyingi inapoteza uwezo wa mwili kukabiliana na magonjwa.
Wale wote ambao sukari
inakuwa imeongezeka miili yao inakuwa haina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Unajua
ni kwa nini? iko hivi,.. unapokuwa na sukari nyingi mwilini inatabia ya kuua
seli nyeupe ambazo husaidia kupambana na magonjwa. Kwa hali hiyo ndio maana
watu wenye visukari hawaponi vidonda kwa sababu kama hii.
5.
Sukari nyingi mwilini zinasababisha mwili kuonekana umeezeka.
Kila sukari inapokuwa nyingi
mwilini, inazalisha kemikali ambazo baadae kemikali hizo hupelekea mwili wako
kuanza kuoneana kama vile umezeeka. Hapa njia pekee ya kuondokana na hali hiyo
ni kupunguza matumizi ya sukari. Vinginevyo utaanza kuonekana kikongwe.
6.
Sukari nyingi husababisha viungo vya mwili kulegea.
Zipo ‘joints’ kama vile za miguu hasa pale unapokuwa unatembea zinakuwa zinachoka
upesi na kulegea kama mwili wako una sukari nyingi. Hali hii hutokea sana hasa
kwa wagonjwa wenye kisukari. Hii ninhali ambayo huwakuta wengi wagonjwa wa
kisukari na inakuwa ni hali inayosumbua.
Mwisho kabisa hapa sina shaka
mpaka unafika mwisho wa makala haya utakuwa umeelewa hatua za kuchukua na hiyo
haitoshi ni vyema ukamshirikisha na mwingine makala haya ili aweze kujifunza na
kundokana na matatizo ambayo pengine yangemkuta.
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
IMANI
NGWANGWALU,
0628
92 98 16,
May 23, 2017
Mbinu Sita Za Ufugaji Bora Wa Kuku.
Kuku wa kienyeji ni wazuri kwa ufugaji kwa sababu:
Wanavumilia sana magonjwa, Ni rahisi kuwahudumia, Chakula chao ni cha bei ya
chini, Wavumilivu wa hali tofauti za hewa, Hawahitaji uangalizi wa karibu sana,
na soko lake ni kubwa sana na bei nzuri (Mayai trei moja Tshs 10,000 mpaka
15,000, kuku wakubwa wanaanzia Tshs 15,000 mpaka 30,000).
Hii haimaanishi kwamba, uwaache kuku bila uangalizi,
kwani nao hupata magonjwa kama wasipo patiwa chanjo sahihi, hupungua uzito na
uzalishaji mayai hushuka kama wasipo patiwa chakula chenye virutubisho vyote.
Hapa naelezea vitu muhimu katika hii formula ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa mafanikio:
1. Aina ya kuku.
1. Aina ya kuku.
Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na
wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa
nyama na upande wa mayai.
Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na
kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini;
kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti za mazingira.
Pia wanauwezo wa kutaga mayai mengi (Wastani wa mayai
matano kwa wiki) karibu sawa na kuku wa kizungu. Aina ya kuku hawa ni kama
vile, Chotara wekundu (Rhode Island Red), Black Australorp (Weusi/Malawi),
Barred Plymouth Rocks (Madoa), New Hamshire Red, Kuroila wanapatikana sana
Uganda, na Kari kutoka Kenya. Hizi ni aina ya kuku zinazo patikana Tanzania.
Chagua kuku waliobora |
2. Chanjo.
Kama nilivyosema mwanzo, kuku wa kienyeji ni wavumilivu
wa magonjwa lakini si kwamba hawayapati, kuna magonjwa ambayo ni hatari pia kwa
kuku wa kienyeji. Chanjo ni muhimu kuwaepusha na hatari ya kuyapata magonjwa
haya.
Chanjo muhimu kwa kuku wa
kienyeji ni; New Castle, Gumboro, Marek’s na Ndui ya kuku. Fuata utaratibu wa
chanjo kutokana na ushauri wa daktari. Hivi karibuni pia makala ya magonjwa na
chanjo itakujia.
Jipatie vifaranga bora na incubators toka DM farm project |
3. Chakula.
Kuku wa kienyeji pia wanahitaji mchanganyiko sahihi wa
chakula, ili waweze kukupatia mazao mengi na bora, na kuwaepusha na magonjwa.
Zipo fomula mbalimbali za chakula kutokana na umri wa kuku, na aina ya kuku.
Kuku wote wanahitaji chakula chenye mchanganyiko sahihi
wa Madini, Vitamini, Protini, Fats, Wanga, Vyakula vya kulinda mwili ili
usipatwe na maradhi, na Maji safi. Muhimu kuwapatia kuku majani kama ziada ya
chakula, hii hupunguza gharama za chakula na kuwafanya kuku waonekane wenye
afya bora.
Ni vizuri kuwapatia vifaranga chakula spesheli cha dukani
kama huna ujuzi wa kutengeneza mwenyewe. Kwani vifaranga wengi hufa kutokana na
kutokupata chakula chenye mchanganyiko sahihi kwao. Kuku wa mayai pia
wanahitaji mchanganyiko sahihi ili waweze kutaga mayai kwa wingi.
Wape kuku wako chakula bora. |
4. Banda.
Kuku wa kienyeji pia, wanahitaji banda au nyumba ya kuku
imara ili kuweza kuwakinga na baridi kali, wanyama hatari, na wizi. Banda pia
liwe na semu nzuri za kutagia na sehemu za kulala ziwe juu , kwani kuku
hupendelea kulala juu. Ni muhimu banda liwe katika hali ya usafi muda wote.
Kwa hivyo ni vizuri linyanyuliwe juu kidogo ili kuruhusu
uchafu kuanguka chini na lijengwe ka kutumia mbao, mabanzi, milunda, nyavu, na
mabati. Vifaranga wanahitaji kutenganishwa na kuku wakubwa. Banda si lazima
liwe la gharama kubwa, kwani mafanikio ya ufugaji wa kuku ni vile unavyo
waangalia na si banda. Mada inayohusu mabanda bora ya kuku itakuja hivi
karibuni.
Tengeneza banda bora. |
5. Majogoo kwa majike.
Ili mayai mengi yaweze kutotolewa, ni vizuri jogoo mmoja
aweze kuwahudumia majike wasio zidi 7. Kwani kuku wanaweza kutaga bila ya
jogoo, lakini mayai hayatoweza kuleta kifaranga. Ili mayai yalete vifaranga ni
lazima yawe yamerutubishwa (Fertilized eggs) na jogoo.
Kwa hivyo ni vizuri kuweka Jogoo 1 kwa majike 7,
hivyohivyo Jogoo 2 majike 14, Jogoo 3 majike 21, n.k. Pia hakikisha kuku wanao
tumika kuendeleza kizazi ni wale wenye afya bora.
Pata pia majike na madume bora. |
6. Vyombo vya chakula.
Hakikisha vyombo vya chakula ni visafi na vinawatosheleza
kuku wote. Vyombo hivi ni vizuri vifanyiwe usafi wa mara kwa mara, ili
kuwaepusha kuku na magonjwa. Maji machafu huwa ni chanzo kikuu cha magonjwa hasa
ya kuhara. Hakikisha kuku wako wanabadilishiwa maji angalau mara mbili kwa
siku.
Kuku wapewe chakula kwenye vyombo safi muda wote. |
Kama
msaada wa ufugaji wa kuku au kama unahitaji vifaranga na mashine za kutotoleshea
vifaranga( Incubators) wasiliana nasi kwa 0767 04 80 35. Karibu sana.
May 22, 2017
Utajiri Wako Unacheleweshwa Hivi...
Kwa jinsi binadamu tulivyo, tunaweza kuona vitu vyote ambavyo havionekani mbele ya macho yetu. Ukifuatilia kwa undani unagundua kuwa vitu ambavyo tunaambiwa na kuamini kuwa havionekani, kiuhalisia vitu vyote vyaweza kuonekana endapo ukiamua. Kwa mazoea, wengi tunafikiri kwamba kama kitu hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, basi tunasema...
hakipo.
Ajabu na kweli ni kwamba, mtu asipoona kitu kwa macho yake ya kawaida, basi udhani kwamba kitu hicho hakionekani na wengine ufikiri kwamba kitu hicho hakipo kabisa duniani. Kumbuka kuwa kuendelea kufikiri na kuamini kwamba kitu fulani hakionekani au hakipo haina maana kwamba hakionekani kwa wengine! Wewe usipoona wengine wanaona.
Tunapodhani kwamba kitu fulani hakipo duniani, wakati kipo, moja kwa moja tunapoteza uwezo wetu wa ndani na nje wa kukifanya kile kisichoonekana kionekane mbele ya macho ya wengi.
Kwa binadamu ni akiri yake pekee iliyo na uwezo wa kuona vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Unapofikiri kwa kutumia akiri (ubongo), hapo tunasema kuwa umeona kwa macho ya akiri au ubongo. Pia, kile uonacho kupitia fikra zako, ndicho ambacho ukusukuma wewe kutumia rasilimali zilizopo, ili kukiweka katika uhalisia.
Kitu kikishakuwa kwenye uhalisia, basi hapo tutasema “umefanya kwa vitendo au umetenda”. Ukisha tenda, maana yake ni kwamba, unakifanya kile ambacho kilikuwa hakionekani mbele ya macho yetu ya kawaida, kionekane sasa machoni mwa wengi. Endapo watu wataona kile ulichotenda, wasijidanganye kuwa “wameona BALI wajue wametazama”.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya “kuona” na “kutazama”. Kutazama siyo kuona, na kuona ni zaidi ya kutazama. Dhana nzima ya “KUONA” ni pale tunapoweza kutumia akiri kuota ndoto, halafu tukapiga picha, halafu tukapanga, tukaamini, na kisha tukatenda.
Kwa maana nyingine ni kwamba, akiri (ubongo) ni kiwanda na karakana ya kuzalisha mambo mapya. Lakini pale tuonapo picha ya kitu kutokea nje (kwa macho ya kawaida), basi huko siyo “kuona” bali ni “KUTAZAMA”.
Binadamu wengi tunao uwezo wa kuona kila kitu endapo tunataka kufanya hivyo. Pamoja na uwezo mkubwa tuliopewa, bado hatuutumii katika kuona fursa za kujiondoa kwenye majanga ya umaskini.
Watu waliofanikiwa mara nyingi wanatwambia kila siku kuwa popote tulipo Tanzania tumezungukwa na fursa nyingi. Kwanini sasa watu wengi ni maskini katika nchi iliyo na fursa nyingi? Jibu ni moja tu nalo ni “watu wengi hawaoni fursa bali wanatazama fursa”.
Utajiri wa uhakika hautapatikana kutokana na watu wengi kutazama fursa BALI ni pale tu watu watakapoweza kutumia akiri zao kuona fursa na kisha kuanza kuchukua hatua za maksudi ili kuzifikia fursa hizo.
Kumbe watu wengi tumekuwa ni watu wa “kutazama” fursa na siyo“kuona” fursa. Unapoona fursa unakuwa na ujasiri, nguvu na shauku ya kutenda ili kufaidi fursa husika. Lakini unapotazama fursa, mara nyingi unajawa sana na uoga, hofu inayotokana na wewe kukosa majibu muhafaka ya maswali unayojiuliza baada ya kuona kwa macho yako kile kilichofanywa na wenzako.
Unapotazama kitu kilicho mbele ya macho yako, mara nyingi utajiuliza maswali mengi bila majibu juu ya jinsi kilivyotengenezwa. Unapokosa majibu sahihi ya mswali yako, mara nyingi utapata hitimisho moja tu! Nalo ni “HAIWEZEKANI”.
Ukishajiridhisha kuwa haiwezekani, basi unaamua kwenda kutazama fursa nyingine ambayo nayo utapata hofu na woga wa kuifanyia kazi. Mwisho wake unaishia kuwa ni mtu wa kutazama na kuongea tu! Huku ukizidi kuandamwa na maisha ya taabu na umaskini.
Watu wenye kuona fursa ndio wenye “maono”. Maono ni ndoto kujumlisha na ukweli wa mambo. Ukiwa na maono yafanyie kazi. Tumia macho ya akiri au ubongo kuona fursa.
Ukitumia macho ya ubongo au akiri, utaweza kuona vinavyoonekana na visivyooekana. Fursa za uhakika hazionekani kwa macho ya kawaida.
Usipoona fursa machoni mwako haina maana kwamba fursa hizo hazipo! ni uhamuzi wako tu! ukiamua zionekane na ziwepo basi, itakuwa hivyo.
Lakini, ukiamua zisiwepo basi, hazitakuwepo wala hazitaonekana mbele ya macho yetu ya kawaida. Jambo hili aliwahi kulisisitiza mwanafalsafa wa Kifaransa aliyejulikana kama Henri Bergson kuwa “Jicho linaona kile ambacho akiri iko tayari kukiona au kuelewa”
Kutokana na maneno hayo ya Bwana “Henri Bergson”, tunajifunza kwamba fursa ambazo hazionekani machoni mwako, ni lazima uziite wewe mwenyewe ndipo zitakuja kwako na usipofanya hivyo watu wengine watafanya hivyo, mwisho wake fursa ulizotakiwa kuzifaidi wewe, utabakia KUZITAZAMA kwa jirani. Endapo jirani au watu wengine wasipoziita fursa hizo, basi zitaendelea kubakia katika hali yake hiyo ya kutoonekana, mpaka zitakapoitwa na vizazi vijavyo.
Leo hii Tanzania kama taifa tunaishi maisha duni kutokana na ukweli kwamba watu wengi wanaanzisha miradi ya biashara baada ya kutazamia kwa wengine. Ni bora ukaona mradi anaoufanya mwingine kuliko kuutazama.
Watu wengi hasa Tanzania, huwa hawaoni miradi bali uitazama tu basi. Kwa maana nyingine ni kwamba, unapoona mwenzako akijishughulisha na mradi fulani wa kibiashara na wewe ukafanya kama anavyofanya bila kuongeza kitu chochote kipya, basi ujue kuwa mradi huo “haujauona”BADALA yake “umeutazama” tu!.
Ni nini faida za kufanya mradi ambao umeuona?
Kimsingi nchi inapokuwa na watu wengi ambao tunafanya miradi tunayoiona kwa macho ya ubongo au akiri zetu, ni wazi kwamba tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua changamoto na kero nyingi ambazo zinasababisha maisha magumu kwa jamii tunayoishi nayo.
Pili, tutaweza kutengeneza bidhaa na huduma za thamani kubwa kwa watu wa Tanzania na dunia kwa ujumla. Tatu, tutasaidia katika kuharakisha ukuaji wa uchumi wetu binafsi na taifa letu kwa ujumla.
Watu wengi tukiona na siyo kutazama miradi ya maendeleo, tutaweza kutegeneza bidhaa nyingi ambazo ni tofauti tofauti. Tukiwa na bidhaa nyingi zenye ubora wa hali ya juu, ni wazi kwamba tutaweza kuvuta pesa nyingi kutoka kwa watu wengine hasa nje ya nchi. Watu wenye pesa zao, watapenda watume pesa zao kwetu, ili kupata bidaa na huduma na hivyo kutufanya sote tuwe na pesa nyingi.
Kwa ngazi ya kitaifa ni kwamba watu kutoka mataifa ya nje watapendelea kutuma pesa zao Tanzania ili kununua suruhisho tulizonazo juu ya changamoto walizonazo kwao – hali hii ndiyo itachangia uwepo wa ajira na hatimaye nchi kuwa na uchumi mkubwa.
Hili tuwe na uwezo wa kuona miradi tufanye nini?
Katika hili hakuna namna na hakuna njia muhafaka ZAIDI ya kuzidi kuwekeza sana kwenye fikra. Ninaposema kuwekeza kwenye fikra ni zaidi ya watu kusoma hadi vyuo vikuu au kubobea kwenye taaluma fulani.
Uwekezaji mzuri kwenye fikra ni ule ambao unajifunza kila siku kwa kutumia njia mbalimbali, kama vile kujenga tabia ya kuwa mdadisi wa kila jambo/kitu na hasa yale yanayohusu kile ambacho unakifanya au unatarajia kukifanya.
Kabla ya kuanzisha mradi wako hakikisha unafanya utafiti wa kero na changamoto zinazowakabili watu waliokuzunguka au wengine wa mbali --- kwa kawaida kero inayo wapata watu waliokuzunguka mara nyingi huwa inawapata pia watu wengi walioko mbali na wewe.
Uzuri wa uwekezaji katika fikra hauna usumbufu na wala hauitaji gharama kubwa. Kinachohitajika ni nidhamu ya kufanya kile ulichopanga kukifanya hata kama ni kigumu. Kwa hiyo, huu ni uwekezaji ambao unaweza kufanywa na karibu wa aina yoyote, ilimradi mtu awe anajua kusoma na kuandika.
May 20, 2017
Jiongeze...Hauhitaji Elimu Kubwa Sana Ili Kufanikiwa.
Hauhitaji elimu kubwa sana
ambayo haina uwezo wa kubadilisha maisha yako, elimu bora ambayo unaihitaji au unatakiwa uipate ni elimu ya kubadilisha
maisha yako, elimu ambayo itakunyanyua au kukutoa sehemu moja na kukupeleka
sehemu nyingine kimaisha. Mafanikio yako makubwa yanakuja kwa kujipatia elimu
inayotoa thamani ya maisha yako na sio vinginevyo.
Kwa hiyo kama kwa namna moja
au nyingine umekosa elimu kubwa ya darasani na kufika mahali unajilaumu kwamba
ningesoma ningefika mbali sana kimafanikio, unakosea, huu sio wakati wa
kusikitika. Jifunze kutafuta elimu yenye thamani itakayobadilisha maisha yako.
na habari njema ni kwamba elimu hiyo haipatikani darasani, inatafutwa mtaani
kwa watu sahihi.
Endelea kuipata elimu hii sahihi ya mafanikio yako kwa kuendelea kusoma dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)