Sep 30, 2017
Njia Ya Mafanikio Yako Ipo Hapa...
Mojawapo ya kosa kubwa linalofanywa
na watu wengi katika safari ya mafanikio, ni kule kukata tamaa hasa wanapokutana
na changamoto.
Kwa kukata tamaa huko kwa
sababu tu ya kukutana na changamoto, naweza nikasema ni moja ya kosa ambalo linaweza
kukufanya usifanikiwe.
Washindi katika maisha
wanajua kwamba, changamoto au kushindwa kwa namna moja au nyingine sio ‘tiketi’ pekee ya kuanza kukata tamaa
mapema.
Inapotokea kitu hakijaleta
majibu unayoyataka, sio swala la kukimbilia kukata tamaa bali ni kubadilisha
njia hadi uweze kufanikiwa.
Inawezekana kabisa njia
unazotumia ni butu na hazifai, sasa hapo sio rahisi sana kuweza kufanikiwa,
bali kufanikiwa kunakuja kutokana wewe kutumia njia mbadala.
Kama njia ya kwanza
imekataa, jaribu ya pili na kama ya pili imekataa, jaribu ya tatu na nyingine
na nyingine tena mpaka kuweza kufanikiwa.
Ipo njia ya kukufikiasha
kwenye mafanikio yako, njia hiyo ipo. Ili uifikie njia hiyo, acha kukata tamaa
mapema. Sumu kubwa sana ya kufanikiwa kwako ipo kwenye kukata tamaa.
Jifunze sana kutokana na
matokeo yanayokatisha tamaa na kisha baada ya hapo tafuta njia mpya
utakayoitumia kufanikiwa tena.
Kuendelea kufanya tena na
tena hata kama unashindwa ni njia muhimu ya kukusaidia kufanikiwa. Kwani amini
njia ya mafanikio yako ipo, huhitaji kukata tamaa.
Kama nilivyokudokezea watu
waliofanikiwa wanatumia njia nying sana, ambazo njia hizo huwasidia kuweza
kufikia mafanikio yao.
Hata wewe unaweza kutumia
njia hizo pia. Lakini usiwe mtu wa kukimbilia tu kuacha kila kitu hasa
unapokutana na changamoto.
Maisha ya watu wengi yapo
hatarini na ni magumu kwa sabbu ni watu wa kuacha tu hasa wanapokutana na
changamoto.
Watu hawa hawajafundishwa au
hawajui kutumia njia mbadala, ila wao wanachojua ikitokea changamoto dawa ni
moja tu ni kuacha.
Ukiwa hata wewe ni mtu wa
kuishi maisha ya namna hii, itakuwia vigumu sana kuweza kufikia mafanikio yako
makubwa.
Siri ya wewe kufanikiwa
unatakiwa kujifunza kufanya jambo kwa namna nyingi sana, ambazo zitakupa
mafanikio na sio kukata tamaa kila unapokuatana na changamoto.
Unachotakiwa kuelewa hapa kupitia
makala hii ya leo ni kwamba, njia ya mafanikio yako ipo, acha kukimbia mapema
kwa sababu ya changamoto. Changamoto zipo na ni za muda.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 29, 2017
Maeneo Manne Ambayo Unatakiwa Kuwa Msikivu Sana Ili Kujenga Mafanikio Yako.
Usikivu
ni moja ya kitu muhimu sana katika safari yako ya mafanikio. Unapokuwa msikivu
inakusaidia kujifunza mambo mengi sana tofauti na ambapo ungejifanya wewe ni
mjuaji wa kila kitu hali ambayo ingekufanya ukose mengi.
Kitu
cha kujiuliza ni watu wangapi ambao ni wasikivu, bila shaka ni watu wachache
sana ambao wanajenga utulivu wa kusikiliza wengine wanasema nini au wao wenyewe
ndani mwao wanasema nini hadi kuweza kufanikiwa.
Kwa kawaida
tunapozungumzia usikivu, wengi wanajua ni usikivu wa kuwasikiliza tu watu
wengine. Lakini jinsi ilivyo upo usiku wa aina nne ambao kila mtu anatakiwa
kuwa nao makini ili kujenga mafanikio yake.
Jenga hali ya usikivu mkubwa ili kujifunza. |
1. Usikivu kwa wengine.
Unatakiwa
kujifunza kusikiliza wengine wanasema nini, nini maoni yao kwako bila kujali wanachokisema
ni chanya au hasi. Kuna kitu cha msingi na cha kubadili maisha yako utakipata
kama ni msikilizaji wa wengine kuliko ambavyo ungebaki wewe kama wewe ukawa
unafuata yako bila kusikiliza mtu yeyote.
2. Usikivu kwako wewe mwenyewe.
Pia unatakiwa
kujisikiliza mwenyewe na kuheshimu maoni yako. Pengine unajiuliza kivipi? Ndani yako kuna sauti ambayo huwa inasema na wewe. Sasa, kuwa makini kusikiliza sauti
yako, maana hio ni muhimu sana kuliko hata sauti zinazotoka nje. Ukiwa msikivu
kwako utapata uwezo wa kujenga pia mafanikio yako.
3. Usikivu kwa dunia.
Kwa jinsi
tunavyoishi, dunia inatufundisha mambo mengi. Unapopata changamoto kuna vitu
unajifunza na kwa namna hiyo unatakiwa kujua kujifunza jinsi dunia inavyosema
na wewe. Utakuwa ni mtu wa ajabu kama hutaki kabisa kujifunza kutokana na dunia.
Yapo mafundisho mengi sana unayoyapata hata
huhitaji kwenda shule.
4. Usikivu kupitia maarifa.
Vile
vitu unavyojifunza vina sema bila kujali ni maandishi au kitabu. Sasa jifunze
kusikiliza kile ambacho waandishi wanasema, kitabadilisha maisha yako kuliko
jinsi ambavyo unang’ang’ana na kuwa mbishi bila kutaka kubadilika. Ukiweza
kuyatumia maandishi vizuri yatakusaidia sana kuboresha maisha yako.
Hayo
ndiyo maeneo muhimu ambayo unatakiwa kuwa msikivu sana ili yaweze kukusaidia
kujenga mafanikio yako. Fanyia kazi maeneo hayo ili yawe msaada mkubwa kwako.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 27, 2017
Ukiwa Makini Na Matokeo Haya…Utafanikiwa.
Nafikiri
na naamini pia, umeshawahi kufanya kitu ambacho haupo nacho makini nacho sana
au hutegemei kupata matokeo makubwa kwenye kitu hicho.
Unajua
nini kilichotokea wakati unafanya kitu ambacho hukuwa na matarajio nacho sana?
ni wazi tu hukufanikinikisha jambo hilo, hicho ndicho kilichokutokea.
Na unajua
ni kwa nini hukufanikisha? najua ulikuja na sababu na visingizio vingi sana
kwamba umeshindwa kufanya jambo hilo kwa sababu ulizoziweka wewe.
Hata
hivyo pia hukufanikisha jambo hilo kwa sababu nguvu ulizokuwa ukiweka hazikuwa
nguvu kubwa sana, ulikuwa ukifanya tu kama unacheza na hutilii mkazo.
Kwa hiyo
hata unapopata matokeo hayo, hayakukushangaaza sana kwa sababu ni kitu ambacho
ulikitegemea kwa kiasi fulani.
Njia
na siri ya pekee ambayo inaweza ikakusaidia wewe kutimiza lile lengo
unalolitaka au mafanikio uyatakayo ni kuwa makini na matokeo kwanza
unayoyahitaji.
Ni rahisi
kushindwa kwa chochote kama haupo makini na matokeo unayotaka, kwa sababu kila
kitu utafanya kizembe tu, kwa sababu matokeo kwako sio muhimu kivile.
Unapokuwa
makini na matokeo unayoyataka,ni wazi utaweka kila aina ya nguvu mpaka
kuhakikisha unakipata hicho unachokihitaji bila kuzuiliwa.
Ikiwa
hujali sana kile unachokifanya, basi jiulize kwa nini unafanya kitu hicho? Maana
hutaweza kuvuna matokeo unayoyahitaji hata kidogo.
Hiyo
maanake nini? Unatakiwa uwe na sababu ya kile unachokifanya ili sababu hiyo
ikupe nguvu ya kutaka matokeo unayoyahitaji.
Kuanzia
leo jifunze kujali sana kile unachokifanya, kifanye kwa ukamilifu na kwa kujali
huko utajikuta ukipata matokeo unayoyahitaji.
Hata
juhudi unazokuwa unaziweka kwa sababu unajali, zitakuwa ni juhudi
zinazokusaidia kwa sababu zinakupa matokeo unayoyahitaji kwenye maisha yako.
Utashindwa
na utaendelea kushindwa ikiwa hujali na hauko makini na matokeo ambayo
unayahitaji kwenye maisha yako.
Umakini
unahitajika sana unatata matokeo yale unayoyahitaji ili uweze kufanikisha
chochote kile unachokifanya, tofauti na hapo utakuwa ni mtu wa kushindwa sana.
Nini
unachokitaka? Nini unachotaka kukifanikisha kwenye maisha yako? kwa chochote unachokitaka
kumbuka, kuwa makini na matokeo, utavuna jinsi unavyopanda.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 26, 2017
Nguvu Ya Mtazamo Katika Kushindwa Au Kufanikiwa Kwako.
Mtazamo una nguvu ya
kubadili hali mbaya inayoonekana na kuwa hali nzuri kabisa. Nguvu yote hiyo ya
kubadili hayo inatoka kwenye mtazamo alionao mtu huyo.
Mtazamo unafanya maisha
kuonekana ya maana, hata pale ambapo wengi wanaona maisha hayana maana tena na
yanachosha.
Mtazamo una nguvu kubwa sana
ya kulainisha kile kinachoitwa kigumu na kuonekana kirahisi, hiyo yote ni kazi
ya mtazamo.
Unapokuwa upo kati kati ya
matatizo, hakuna kitu kingine kinachoweza kukuokoa na kutoka hapo na kuwa na
amani zaidi ya kubadilisha mtazamo wako.
Unapobadili mtazamo, hata kama tatizo lako lilikuwa kubwa sana, tatizo
hilo unaona linaanza kulainika na linakuwa linawezekana kutatuliwa.
Wengi wanaoshindwa katika
maisha na kuamua kukata tamaa kabisa ni watu ambao mara nyingi wameshindwa
kutawala mitazamo yao.
Kiuhalisia unaposhindwa kutawala
mtazamo wako na ukajikuta una mtazamo hasi, elewa kabisa maisha yako yatakuwa
magumu sana katika kila eneo.
Kwa hiyo unaona kabisa
mtazamo una nguvu kubwa sana ya kubadili maisha yako, inategemea tu wewe
unautumiaje huo mtazamo wako ulionao.
Ndio kila wakati unashauriwa
kukaa na watu chanya, watu ambao wataweza kukusaidia kukujengea mtazamo mzuri
wa kufanikiwa.
Kwa hiyo kuanzia sasa
hutakiwi kushangaa, unapoona wengine wanafanikiwa na wengine wanashindwa hilo
ni swala la mtazamo.
Kwa mfano, utakuta ni watu
wanaokaa katika mji mmoja au nchi moja lakini wengine wamefanikiwa na wengine
wameshindwa, hapo hakuna kingine zaidi ya mtazamo.
Anguko kubwa la watu
linaanza na mitazamo yao. Kwa jinsi unavyokuwa na mtazamo mbovu ndivyo maisha
yako yanazidi kuwa mabovu pia.
Lakini mtazamo mzuri una
siri kubwa ya kugeuza chochote kuwa mafanikio. Mtazamo mzuri unaweza kugeuza
hata maji kuwa almasi.
Mtu mwenye mtazamo mbovu
mara nyingi hata apewe fursa nzuri vipi sio rahisi kufanikiwa, kinachomwangusha
ni mtazamo wake tu.
Hiyo yote inaonyesha
kushindwa kwa wengi kunasabbishwa na mtazamo wake sana, na hapo ndipo ulazima
kwa kubadilisha mtazamo unahitajika kwa nguvu zote.
Leo kama unataka kufanikiwa,
hebu anza kubadili mtazamo wako ili ukusaidie kwani una uwezo wa kubadili chochote
na kuwa kizuri.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 25, 2017
Ubora Wako Unatokana Sana Kufanya Hivi…
Kwa jinsi unavyofanya kitu chochote
kile kwenye maisha yako, ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi katika kitu hicho.
Kwa mfano, kama wewe ni
mwimbaji kwa jinsi unavyoimba kila siku na kufanyia mazoezi ndivyo unavyozidi
kuwa bora katika uimbaji wako.
Kama wewe ni mwandishi, kwa
jinsi unavyoandika kila siku, hivyo ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uandishi
wako.
Kama wewe ni mtu wa
kujifunza vitu, kwa jinsi unavyojifunza, utashangaa unajikuta unakuwa ‘mlevi’ wa kutupwa wa kujifunza.
Kama wewe ni mtu wa
kulalamika, kwa jinsi unavyoendelea kulalamika, hivyo ndivyo sasa utakuwa
mlalamikaji mbobebezi, utalalamikia kila kitu.
Fanya kitu, uongeze ufanisi wako. |
Kama wewe ni mtu mwenye
tabia za kukopa kopa pesa kwa watu, utashangaa kwa jinsi siku zinavyokwenda
unakuwa mkopaji kweli na una madeni kibao.
Kama wewe ni mtu wa kutoa
sababu, basi hutafanya kitu cha maana, ni rahisi kuendelea kutoa sababu sana
karibu kwa kila mtu.
Kama wewe ni mtu wa visasi,
kuwa makini hapo, unaweza ukawa na mtu wa visasi kwa watu wengi sana kwa sababu
ndio kitu unachokifanya.
Kama wewe ni mtu
unayehakikisha jambo unalolianza lazima lifanikiwe, basi elewa utaendelea
kufanikisha pia mambo mengine kwenye maisha yako.
Kwa chochote unachokifanya,
bila kujali kitu hicho ni chanya au hasi utazidi kupta matokeo bora ynayoendana
na kitu hicho unachokifanya kila siku.
Hebu jaribu kuangalia katika
maisha yako ni kitu gani ambacho unakifanya sana? kwa kifanya kitu hicho utapata
matokeo yake.
Hivyo basi kila wakati, chagua
kufanya kwenye maisha yako mambo bora na fanya kila siku, baada ya muda utakuwa
bora kwenye mambo hayo na kufanikiwa vikubwa.
Ni vigumu sana kuwa mshindi
katika maisha yako kwa kufanya kitu mara moja na kutegemea mafanikio makubwa. Unatakiwa
kufanya kila siku.
Kwa hiyo unaona mafanikio au
kushindwa ni matokeo ya kufanya kitu fulani unachokifanya kila siku na kwa muda
mrefu.
Kufanikiwa au kushindwa
hakutokei mara moja kama wengi wanavofikiri, ni matokeo ya kuwekeza nguvu zako
kila siku kwenye jambo hilo.
Anza leo kufanya mambo
yatakayokusaidia kujenga ubora utakao kusaidia kufanikiwa sana na sio
yatakayokuangusha.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 24, 2017
Kama Utaitumia Nguvu Hii… Ndiyo Itakayokufanya Ufanikiwe.
Kwa nguvu ya ung’anga’nizi,
ndiyo inayopelekea tone moja la maji linalodondoka kila siku ipo siku livunje
jiwe hilo kabisa.
Kwa nguvu ya ung’ang’anizi,
mbegu dogo kabisa inauwezo wa kukua kwenye tawi la mti mkubwa na hatimaye kuwa
mti mkubwa sana pia.
Kwa nguvu ya ung’ang’anizi
kila mtu ana uwezo wa kubadilisha maisha yake, hata kama mtu huyo yupo kwenye
wakati mgumu sana.
Kwa nguvu ya ungang’anizi,
ndiyo inayofanya maisha ya wengine yawe mazuri na maisha ya wengine kuwa mbaya
kutokana na kung’ang’ania vibovu.
Kwa nguvu ya ung’ang’anizi,
ndio inayompa mtu mafanikio hata kama anatokea chini kabisa bila kuwa na kitu.
Hakuna kinachoshindikana,
hakuna mafanikio ambayo utashindwa kuyapata kama kweli leo, utaamua kung’ang’ania
kile unachokitaka kwenye maisha yako.
Nguvu unayotumia kung’ang’ania
mambo, hata kama nguvu hiyo ni kidogo itakusaidia sana kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa.
Watu wengi wanashindwa
kufanikiwa sana, kwa sababu ya kushindwa kutumia nguvu ya ung’ang’anizi kwenye
yale mambo wanayoyafanya.
Sio ajabu sana kumkuta mtu
kaanzisha jambo leo, lakini kesho mtu huyo akikutana na changamoto anaacha kila
kitu.
Huwezi kufanikiwa kwa
viwango vikubwa kama wewe si king’ang’anizi. Kama mafanikio kweli utayapata, lakini utapata mafanikio ya rasharasha.
Unatakiwa utambue hata
ukutane na changamoto, unatakiwa kukomaa mpaka kieleweke. Hakuna mafanikio yanayokuja
kirahisi.
Ikiwa kuna kitu unakifanya
hata sasa na unaona hakikupi matokeo ya upesi kama unavyotaka, jipe muda kwanza
na usikimbilie kukata tamaa.
Kama utakuwa ni mtu wa
kukata tamaa mapema na kushindwa kuwa king’ang’anizi basi elewa utashindwa
kwenye mambo mengi sana.
Ifike mahali ujiulize ni
wapi unapotaka kufika kimaisha, ni wapi unapotaka kwenda na ukishajua hivyo
amua kabisa kung’ang’ania mpaka kieleweke.
Usikubali kitokee kitu eti
ambacho kitakuzuia kufanikiwa kwako. amua kwamba iwe itakavyokuwa bila kujali
utatumia muda gani mafanikio yako ni lazima.
Ukijivusha ujasiri huo wa
kuwa king’anganizi mafanikio yeyewe yatakupisha na kutakuwa hakuna namna
nyingine ya kukuzuia.
DAIMA TUPO
PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 23, 2017
Ongeza Uwezo Wako Wa Kufikia Mafanikio Yako Hivi…
Haijalishi
maisha yako ni mazuri kiasi gani, lakini
unayo nafasi ya kuyafanya maisha yako yakazidi kuwa bora kuliko ya hapo ulipo
Haijalishi
una hali ngumu vipi za kimaisha, lakini unaweza kuboresha maisha yako kidogo
kidogo na mpaka kuwa bora kabisa.
Haijalishi
ni kwa jinsi gani unajua mambo mengi sana, lakini kwako ipo nafasi ya kujifunza
na kuendeleza kupata maarifa yatakayokusaidia.
Chochote
unachokifanya leo jiulize, kina uwezo wa kukua kesho na kuendelea kukupa
mafanikio makubwa?
Ongeza uwezo wa mafanikio yako. |
Ni kitu
gani ambacho utakifanya leo na kikaendelea kukuweka juu tena na tena kwenye maisha yako ya kimafanikio?
Ukikaa
na ukatulia, utagundua zipo njia ambazo zina uwezo wa kukufanya ukakua na
kuongeza nafasi ya mafanikio yako sana.
Huhitaji
kujilinganisha na wengine ili kuwa bora, unatakiwa kujilinganisha wewe tu
mwenyewe na kuongeza ubora ulionao kila wakati.
Usikubali
kuyafanya maisha yako yakaonekana mabovu kwa sababu ya kusimama au kuridhika
kwa namna fulani.
Mashujaa
katika maisha ni watu ambao wanajipa changamoto sana za kukua kila siku kwenye
maisha yao.
Hicho
ndicho kitu ambacho unatkiwa ujipe au ukifanye ili kufanikiwa. Unatakiwa ujipe
changamoto ambazo zitakusaidia kukua.
Kwa
mfano, kama umeamua kusoma, soma idadi kubwa sana ya vitabu ambayo itakufanya
uwe mkomavu kiakili.
Kama
umeamua kuwekeza, wekeza sana na isifike mahali ukatikisa kichwa na kusema kama
ni kuwekeza sasa imetosha.
Unatakiwa
kukua, unatakiwa kuongeza misuli ya kile ukifanyacho na kuwa kikubwa sna zaidi
ya hapo ulipo kwa sasa.
Ukumbuke
hakuna mtu ambaye ataweza kukuzuia katika hilo, zaidi yako wewe. Unao uwezo
mkubwa wa kuongeza mafanikio yako.
Hautakiwi
kusimama sasa, unachotakiwa kufanya sasa ni kuweka nguvu zako za uzingativu
eneo unalotaka ukue.
Ukishaweka
nguvu zako za uzingativu eneo hilo, anza kufanyia kazi huku ukiweka kila aina
ya juhudi inayotakiwa ili kufanikiwa.
Nuia
kubadilisha maisha yako tena, nuia kubadilisha matokeo ya maisha yako tena,
nuia kubadilisha chochote maishani mwako.
Usikubali
kukaa kama jiwe, mwanza wa mabadiliko katika maisha yako ni sasa kwa wewe
kukubali kuuongeza uwezo wa mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 22, 2017
Sifa Moja Ya Muhimu Sana Katika Kukupa Mafanikio.
Mafanikio
yako yanakuja kutokana na wewe kuwa wa muhimu. Mafanikio yako ya kweli hayaji
kwa sababu ya bahati nasibu wala hayaji kwa sababu ya kuwanyonya watu wengine
sana, mafanikio yako ya kweli na ya kudumu yanakuja kwa sababu ya wewe kuwa wa
muhimu katika maisha yako.
Kwa
jinsi yoyote ile unavyotafuta mafanikio unatakiwa kuwa wa muhimu na kutoa
thamani inayohitajika ili kufikia mafanikio yako. Hutakiwi kuwepo kuwepo tu
kwenye maisha yako, unatakiwa uwe na machango wa kimafanikio kila siku iitwayo
leo.
Jiulize
kitu gani ambacho utakifanya sasa kitakuwa na mchango na umuhimu kwenye maisha
yako? Jiulize tena ni juhudi gani kubwa ambazo unaendelea kuweka mwenye kazi na
hata kwenye maisha yako kwa ujumla?
Kuwa mtu wa thamani utafanikiwa. |
Ni
rahisi kuweza kuiba na kufanya kitu chochote ambacho sio haki ili ujipatie
mafanikio. Lakini ukumbuke kwa njia hizo sio rahisi kabisa kupata mafanikio ya
kweli yatakayokufanya ung’are na uwe miongoni mwa watu waliofanikiwa.
Kupata
mafanikio ya kweli kunaanza ndani mwako kwanza, kutokana na thamani unayoitoa,
ambapo thamani hiyo ndiyo itakayo kufanya kila kona uwe wa muhimu na kupelekea
kila mtu akikutamani uwe nae karibu kwake.
Kwa
hiyo mpaka hapo unaona ili kufanikiwa, unahitaji kuwa wa tofauti, unahitaji
kuwa wa thamani, unahitaji kuwa wa pekee ili kutengeneza thamani ambayo
ukiipata ni lazima uweze kufanikiwa hata kama mazingira yanakataa.
Kama
unatilia shaka hilo la umuhimu wako kwenye maisha ya wengine, ngoja tu
nikwambie wewe ni wa pekee sana na mchango wako mkubwa unahitajika katika
maisha ya wengine pia ili uweze kuyabadilisha.
Kama
una umuhimu mkubwa hivyo kwa wengine, jifunze kuweka juhudi kubwa sana kila
siku ili kutengeneza umuhimu na thamani yako zaidi. Umuhimu wako hauji kwa
kukaa tu, umuhimu wako unakuja kutokana na kujituma na kuweka juhudi hadi
kufanikiwa.
Anza
kuwa wa muhimu leo kwa kubadilisha maisha ya wengine, kwa jinsi unavyobadilisha
maisha ya wengine unazidi kuwa baraka kwa wengine , nawe pia maisha yako
yanakuwa yanabadilika vivyo hivyo.
Ni
kipi unachosubiri kuwa wa muhimu? Kuwa wa muhimu, ni sifa mojawapo kubwa sana
ya kukupa mafanikio yako. Anza sasa na
chukua hatua katika kuelekea kufikia mafanikio yako makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 21, 2017
Mara Ngapi Umeshindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Hizi?…
Ni
mara ngapi umekuwa ukitaka kubadilisha hali fulani hivi kwenye maisha yako,
lakini cha ajabu tena umekuwa ukikata tamaa kwa mara ya kwanza hasa pale
unapokutana na changamoto kwenye maisha
yako?
Ni mara
ngapi umekuwa ukijiwekea malengo yako na kusema lazima nitatimiza lengo hili,
lakini kitu cha ajabu umekuwa ukiyasahau malengo hayo mara moja na tena umekuwa
huyakumbuki kama vile hukuweka malengo kabisa?
Ni
mara ngapi umekuwa ukitoka nje ya mstari wa malengo yako uliyojiwekea hasa
kutokana na maoni au malengo ya watu waliokwambia kwamba huwezi kitu hiki na
wewe kutokana na kuwasikiliza ukaacha kweli?
Usikatishwe tamaa na chochote |
Ni mara
ngapi umekuwa ukisema utaweka akiba, ambayo itakusaidia baadae kuwekeza kwenye
maisha yako, lakini umekuwa hufanyi hivyo kutokana na sababu zako ambazo
unazijua wewe?
Ni
mara ngapi umekuwa ukitoa sana visingizio badala ya kutoa matokeo yanayotakiwa
kutolewa? Umeshawahi kujiuliza hili? Kila kitu unakuwa umejipanga kama vile
unataka kutoa sababu badala ya kutoa matokeo yanatakayokusaidia kwenye maisha?
Ni
mara ngapi umekuwa ukiishi maisha chini ya kiwango, maisha ya kuhuzunika na
kuacha kuchukua hatua sahihi ambazo hatua hizo zinaweza kukupeleka kwenye
mafanikio yako makubwa uyatakayo?
Muda
huu na wakati huu ulionao una mahusiano moja kwa moja na kesho yako ya
mafanikio. Hivyo, jinsi ambavyo umekuwa ukiahirisha mambo na kusema utafanya
hili na hufanyi, elewa kabisa ndivyo umekuwa ukijiangusha mwenyewe kwenye
maisha yako.
Unatakiwa
kuishi kwa nia moja na hamu kubwa ya kujitoa hadi kufikia mafanikio. Lakini kama
kila mara unasema unafanya hili halafu hufanyi, utakuwa unajenga tabia ambayo
moja kwa moja msingi wake mkubwa ni kukuangusha na si kufanikiwa.
Najua
changamoto kweli zipo katika maisha, lakini changamoto hizo isiwe sababu kubwa ya
wewe kuacha mipango yako kila mara na kutoka nje ya mstari. Wakati wa kufanya
na kutimiza ndoto zako ni sasa, fanya kitu.
Usikubali
kushindwa kwenye maisha yako kwa sababu ya kutokufanya, usikubali kushindwa eti
kwa sababu kila mara unaahirisha. Chukua hatua sahihi za kubadili maisha yako
ili ufikie mafanikio makubwa.
Tunakutakia
siku njema na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 20, 2017
Jinsi Unavyoweza Kujifunza Kuweka Nguvu Za Uzingativu Eneo Moja.
Ni
kama kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona mtu akiwa anakula huku
macho yake yote yakiwa kwenye simu, tv au kitu kingine tofauti. Hiki si kitu
cha ajabu kwa siku hizi, japo naweza kusema limekua kama tatizo ambalo
linawasumbua watu wengi.
Watu
wengi kwa nyakati hizi wamekosa sana utulivu, wamekuwa ni watu wakutaka kufanya
mambo mengi sana na kwa mkupuo. Kutokana na hili, ufanisi wa kazi umekuwa ukipungua
na hakuna cha maana ambacho kimekuwa kikifanyika.
Kutokana
na ujio wa teknolojia hasa ingizo la simu janja/ ‘smart phone’ hili limechangia sana kwa kiasi kikubwa kwa kuelekeza
watu nguvu zao nyingi kwenye simu na kusahau majukumu ya msingi. Kwa mfano,
ukiingia kwenye gari, ofisini au nyumbani ni rahisi kumkuta karibu kila mtu
anatazama simu yake.
Lakini
ukichunguza hata kile anachokitazama kinaweza kisiwe na maana sana, lakini ni
hali ambayo ipo na inapelekea badala ya kufanya majukumu ya msingi, muda mwingi
unakuwa unapotea kwenye simu na bila faida yoyote.
Nimekupa
mfano kidogo ili upate picha ya kile ambacho nataka kusema. Simaanishi tu kwamba
simu peke yake ndio imekuwa chanzo cha watu kufanya mambo kwa undumila kuwili,
la hasha, bali watu wamekuwa na mambo mengi sana wao kama wao kutokana na
kuibua tabia hii mpya.
Weka nguvu zako za uzingativu eneo moja. |
Kwa sasa
haishangazi tena kama mtu akianza jambo hili kabla hajamaliza anataka tena
kurukia jambo lingine. Unaweza ukajiuliza kama akili haitulii sehemu moja,
ukishika hiki unaacha na unakimbilia kitu kingine, sasa kwa mwendo huo ni kitu
gani ambacho utaweza kweli kukifanikisha kwenye maisha yako?
Kwa kifupi
hili ni tatizo na kwa wengi imekuwa ngumu sana kuweza kuvunja tabia hii kwa
sababu ya mazoea, ingawa zipo mbinu au njia za kufanya hivyo. Kitendo cha
kushindwa kuishinda hali hii, ni sawa na kuamua kuendelea kuharibu maisha yako.
Kwa vyovyote
vile iwavyo, unatakiwa kujua jinsi utakavyoweza kuweka nguvu zako za uzingativu
katika eneo moja ili uweze kutenda mambo yako kwa ufanisi na mafanikio. Itakuwa
ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa ikiwa utashindwa kuvunja tabia hii. Je,
unawezaje hili;-
Hivi
ndivyo jinsi unavyoweza kujifunza kuweka nguvu za uzingativu eneo moja.
1. Chagua jukumu moja la muhimu
kutekeleza.
Asubuhi
unapoamka mara baada ya kusali na kufanya ‘meditation,’
kabla hujawasha simu yako anza kutekeleza jukumu lako la muhimu. Najua unaweza
ukawa una vitu vingi vya kufanya, lakini chagua kitu kiomoja tu cha kuanza
nacho na vingine vyote visahau kwa muda mpaka ukamilishe jukumu lako moja la
muhimu kwa wakati huo.
2. Jukumu ulilichagua lifanye kwa dakika
15 bila kuacha.
Katika
dakika hizi usikubali kuingiliane na kitu chochote, tumia dakika hizo vizuri
nguvu zako zote zihamishie hapo. Usichague dakika nyingi sana za kuanza kuweka
nguvu za uzingativu kwa pamoja, anza kwanza na dakika chache, ikitokea umeshindwa
dakika 15, punguza ziwe hata 10 au 5 lakini lazima uibuke mshindi.
3. Fanya kila siku na kwa kila kitu.
Ili tabia
hii iweze kukaa na iwe yako, fanya kila siku na kwa kila kitu kiwekee nguvu ya
uzingativu. Unapoamua kufanya kitu fulani mawazo yako yote hamishia hapo na bila
shaka hapo utakuwa na ufanisi mwema wa kazi yako. Lakini ikiwa utashindwa zoezi
hilo hiyo itakuwa ngumu kwa wewe kuweza kufanikiwa.
Inabidi
ieleweke kwamba, kuweka nguvu za uzingativu katika eneo moja kwa masaa kadhaa,
kwa siku kadhaa na kwa muda fulani maalumu kuna leta mabadiliko ya maisha yako
bila kipangamizi chochote.
Ni jukumu
lako leo kuanza kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kila ukifanyacho ili
kikuletee mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 19, 2017
Ukiweza Kutumia Muda Huu Vizuri, Utafanikiwa.
Kama unavyojua dakika moja si muda mrefu sana.
Hata hivyo pamoja na kwamba muda huo ni mfupi sana ila kila kitu kilichofanyika
duniani na kikaleta mafanikio, kilianza kufanywa kwa kuanza na dakika moja tu
na sio vinginevyo.
Kipi ambacho unataka
kukifanya, hakitaanza kufanywa kwa dakika moja ya kwanza, bila shaka hakuna.
Kama una kitu unataka kukifanya na unaona uvivu fulani jipe muda wa dakika moja
tu kwanza, dakika hiyo itakupa nguvu ya kuendelea zaidi.
Kama unaweza kufanya
kitu chochote kwa dakika moja, kama unaweza kuvumulia kwa dakika moja, basi
unaweza kuendelea zaidi ya hapo kwa kutumia muda wako vizuri sana ikiwa pamoja
na kila dakika unayoipata kwenye maisha yako.
Ukimudu kuweza kuitumia dakika moja yako vizuri, itakusaidia
kuokoa muda wako mwingi ambao ulikuwa unaupoteza bila manufaa yoyote kwako.
Dakika moja ukiitumia vizuri na ukaendelea kutumia zingine vivyo hivyo, ni
msingi mkubwa wa mafanikio yako.
Sep 18, 2017
Jinsi Watu Wanavyoweza Kukurudisha Nyuma Kwenye Maisha Yako, Ikiwa Utawaruhusu.
Wapo
watu katika safari ya maisha ambao wapo tayari kukusaidia kukua kimafanikio na
kukuona wewe ukifanikiwa na pia wapo watu katika safari ya maisha ambao wao
wapo tayari kukuona wewe ukikamwa na hawapendi sana ufanikiwe.
Unapokuwa
na kundi kubwa la watu hasa hili la pili ambalo halitaki kukuona wewe
ukifanikiwa kwenye maisha yako, uelewe kabisa unakuwa upo katika hatari kubwa
sana ya kutokufanikiwa kwa kile ukifanyacho.
Nasema
hivyo kwa sababu, watu hawa wanakuwa wanatumia njia au mbinu zao kuhakikisha
unakwama au husogei kabisa, yaani wanataka uwe kama wao. Je, watu hawa
wanakurudisha vipi nyuma kwenye maisha yako?
Kuwa makini na watu wanaotaka kukurudisha nyuma. |
1. Kukukosoa sana.
Watu
wenye lengo la kukurudisha nyuma, moja ya njia au mbinu wanayoitumia ni kukosoa
sana. kila wakati watajaribu kukuonyesha kwamba wewe ni mtu wa kukosea na hadi ujione
hufai. Kwa mbinu hii ukiikubali hutafanya kitu, zaidi utatulia usifanye kitu kwa kuogopa kukosolewa.
2. Kutokuthamini mchango wako.
Njia
nyingine ambayo watu wenye lengo la kukurudisha nyuma kwenye maisha huitumia
sana ni kutokujali mchango wako kabisa. Kila utakachokifanya kitaonekana kwao
hakuna kitu. Sasa kwa kuwa umejua hili usijisikie vibaya, kama kuna kitu umekifanya
wewe endelea kukifanya kwa moyo wote kwa sababu unajua ni nini ukifanyacho.
3. Kukufanya ujitilie shaka.
Kati
ya kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu kwenye maisha yako ni kumruhusu mtu
mwingine akushushe au akutilie shaka ule uwezo wako mkubwa ulionao. Watu wanaotaka
kukurudisha nyuma mara nyingi hutumia mbinu ya kutaka kukufanya ujione huwezi
kitu yaani wewe ni mtu wa kawaida tu. Ukiruhusu hali hii utakwama.
4. Kutaka kukufanya ujione maisha yako
yamekwama kabisa.
Mbali
na kukukosoa sana, kutokukuthamini mchango wako na kukufanya ujitilie shaka,
pia watu wanaokurudisha nyuma wanataka wakuonyeshe maisha yako yamekwama kabisa
na hakuna njia mbadala ya kuweza kutoka hapo. Hapo watakuonyesha kwamba wewe
huwezi kitu.
Hivi
ndivyo watu wanavyoweza kukurudisha nyuma kwenye maisha yako ikiwa utawaruhusu kufanya
hivyo. Kitu cha msingi ni kuwa makini na njia zao hizo na kuepuka kuendana kama
wao wanavyotaka iwe.
Chukua
hatua na kila la kheri katika kufikia mafanikio yako makubwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 17, 2017
Sababu Zinazofanya Watu Wengi Kufanya Maamuzi Mabovu.
Kati
ya kitu kimojawapo kinachofanya watu washindwe sana kwenye maisha ya mafanikio
ni kile kitendo cha kufanya maamuzi mabovu. Maamuzi mabovu yanaharibu na
yanapoteza maisha ya mafanikio ya watu wengi sana.
Ni vyema
kujua maamuzi mabovu ni chanzo cha kushindwa kwa watu wengi sana na maamuzi
hayo mabovu yanafanywa karibu kila siku na wengi. Kitu cha kujiuliza, je, ni
kwanini watu wengi wanafanya maamuzi mabovu ambayo yanapelekea kuharibu maisha
yao?
1. Mitazamo mibovu waliyonayo.
Kitu
ambacho kinasemwa na wataalamu wengi wa mafanikio kwamba kinapelekea kwa watu wengi
kuwa na mamuuzi mabovu mitazamo mibovu au ‘poor
mindset’ walizonazo, hiki ndicho kitu kinachofanya watu wengi wanakuwa na
maamuzi mabovu sana.
Hivyo
ili kuwa na maamuzi sahihi, unatakiwa kuwa na mtazamo sahihi. Na mtazamo sahihi
hauji hivi hivi tu bali ni matokeo ya kujifunza kila siku kupitia vitabu na
kujua mawazo ya wengine. Ukijifunza hiyo ni njia itayokusaidia kuwa na mtazamo
sahihi utakao kufanya uwe na maamuzi sahihi pia.
2. Kufuata
sana maamuzi ya watu wengine.
Kuna
wakati maamuzi mabovu yanakuja kwa sababu tu ya kufuata maamuzi na taratibu za
jamii. Hapa unajikuta mtu unaamua jambo fulani kwa sababu jamii yako inafanya hivyo
au inaishi hivyo na wewe unaamua kuamua
hivyo.
Mfano
wa athari za maamuzi haya zinajitokeza kwa watu hasa wanapokuwa wanataka pengine
kujiunga na masomo ya aina fulani, mathalani, utakuta kozi fulani inasemekana
inalipa sana ukiisoma, kwa sababu hiyo utashangaa na mtu mwingine anaifuata, pengine
kumbe kwa maamuzi hayo ni mabovu na kozi hiyo inaweza isimsaidie.
3. Kutokujielewa.
Mbali
na maamuzi mabovu na kufuata maamuzi ya watu wengine kitu kingine
kinachopelekea maamuzi mabovu ni kutokujielewa. Watu wengi wanachelewa sana
kujielewa bila kujijua na matokeo yake hufanya maamuzi mabovu sana kila wakati.
Ili kuepuka
kuendlea kufanya maamuzi mabovu elimu ya utambuzi inahitajika karibu kwa kila
mtu ambayo itasaidia kufanya maamuzi yaliyobora. Bila kupata elimu ya utambuzi
itakuwa ni kazi bure tu maamuzi mabovu yataendeea kufanikiwa na kuharibu
maisha.
Kama
tulivyoeleza kila wakati unapoona maamuzi mabovu yamefanikiwa sehemu yoyote
ujue kabisa sababu kubwa zinazochangia ni pamoja na kutokujielewa, mitazamo
mibovu na kufuata mitazamo ya watu wengine.
Chukua
hatua na endelea kutembelea dirayamafaniko.blogspot.com kujifunza kila siku..
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Sep 16, 2017
Ili Ufanikiwe, Ishi Kwa Sababu Hii…
Kipo
kitu kwenye maisha yako ambacho kinakufanya uamke asubuhi na mapema. Kipo kitu
ambacho kinakufanya uongeze juhudi zako hata kama unakutana na changamoto za
kila aina. Kitu hicho kinaweza kuwa ni ndoto au yale malengo unayotaka
kuyakamilisha kwenye maisha yako.
Hiyo
yote inaonyesha unaamka asubuhi na unaweka juhudi bila kukata tamaa kwa sababu
ipo sababu inayokufanya ufanye hivyo, sababu yenyewe si nyingine bali ni
kukamilisha malengo yako. Hiyo hasa ndiyo sababu kubwa inayokufanya ufanye kila
linawezekana mpaka kuona mipango yako yote inatimia.
Kwa hiyo
unachotakiwa kuelewa ipo sababu, katika kila kitu ambacho unatakiwa kukifanya. Unatakiwa
kuielewa sababu hiyo vizuri ili ikusaidie kuchochea moto mkubwa wa mafanikio
ulio ndani mwako. Ukiwa huna sababu ya hicho unachokifanya utashindwa kuweka
juhudi kubwa na mwisho wa siku utashindwa tu.
Ishi kwa sababu maalumu. |
Anza
leo kuishi kwa sababu, jiulize kitu hicho unachokifanya sasa, kwa nini
unakifanya, chanzo cha msukumo wake ambao unatoka ndani mwake ni nini hasa? Ukishaijua
hiyo sababu itakufanya usikate tamaa na kila wakati utatamani sana kukifanya
kitu hicho ili utimize sababu ya kufanya kitu hicho.
Watu
wengi katika maisha wanajikuta hawasogei sana au ni watu wanaotaka kusukumwa
sukumwa tu, hiyo yote ni kwa sababu ni watu ambao hawajui hasa sababu ya
kufanya hivyo wanavyotakiwa kufanya. Ukiwa hujui hasa sababu inayokusukuma
kufanya jambo unalolifanya sio rahisi kufanikiwa.
Hata
safari yoyote unapoianza asubuhi, sina shaka unakuwa una sababu kwa nini
unaenda safari hiyo. Sijawahi kuona mtu anasafiri tu ilimradi asafiri, lazima
awe na sababu huko anakoenda anaenda kufuata nini? Bila ya kuwa na sababu ya
hiyo safari basi itakuwa safari hiyo ni kazi bure.
Halikadhalika,
maisha yetu hasa kwa yale mambo tunayoyafanya yanatakiwa yawe na sababu haswaa,
sababu ndio msingi wa kwanza wa kukusaidia kuweza kupiga hatua za kufanya hicho
unachotakiwa kukifanya. Hatua zako zitakuwa imara na utafika mbali sana ikiwa
unajua sababu ya kile hasa unachokifanya.
Chukua
hatua leo na anza kuishi kwa sababu, hapo utafika mbali kimafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)