Sep 20, 2017
Jinsi Unavyoweza Kujifunza Kuweka Nguvu Za Uzingativu Eneo Moja.
Ni
kama kitu cha kawaida kwa siku za hivi karibuni kuona mtu akiwa anakula huku
macho yake yote yakiwa kwenye simu, tv au kitu kingine tofauti. Hiki si kitu
cha ajabu kwa siku hizi, japo naweza kusema limekua kama tatizo ambalo
linawasumbua watu wengi.
Watu
wengi kwa nyakati hizi wamekosa sana utulivu, wamekuwa ni watu wakutaka kufanya
mambo mengi sana na kwa mkupuo. Kutokana na hili, ufanisi wa kazi umekuwa ukipungua
na hakuna cha maana ambacho kimekuwa kikifanyika.
Kutokana
na ujio wa teknolojia hasa ingizo la simu janja/ ‘smart phone’ hili limechangia sana kwa kiasi kikubwa kwa kuelekeza
watu nguvu zao nyingi kwenye simu na kusahau majukumu ya msingi. Kwa mfano,
ukiingia kwenye gari, ofisini au nyumbani ni rahisi kumkuta karibu kila mtu
anatazama simu yake.
Lakini
ukichunguza hata kile anachokitazama kinaweza kisiwe na maana sana, lakini ni
hali ambayo ipo na inapelekea badala ya kufanya majukumu ya msingi, muda mwingi
unakuwa unapotea kwenye simu na bila faida yoyote.
Nimekupa
mfano kidogo ili upate picha ya kile ambacho nataka kusema. Simaanishi tu kwamba
simu peke yake ndio imekuwa chanzo cha watu kufanya mambo kwa undumila kuwili,
la hasha, bali watu wamekuwa na mambo mengi sana wao kama wao kutokana na
kuibua tabia hii mpya.
Weka nguvu zako za uzingativu eneo moja. |
Kwa sasa
haishangazi tena kama mtu akianza jambo hili kabla hajamaliza anataka tena
kurukia jambo lingine. Unaweza ukajiuliza kama akili haitulii sehemu moja,
ukishika hiki unaacha na unakimbilia kitu kingine, sasa kwa mwendo huo ni kitu
gani ambacho utaweza kweli kukifanikisha kwenye maisha yako?
Kwa kifupi
hili ni tatizo na kwa wengi imekuwa ngumu sana kuweza kuvunja tabia hii kwa
sababu ya mazoea, ingawa zipo mbinu au njia za kufanya hivyo. Kitendo cha
kushindwa kuishinda hali hii, ni sawa na kuamua kuendelea kuharibu maisha yako.
Kwa vyovyote
vile iwavyo, unatakiwa kujua jinsi utakavyoweza kuweka nguvu zako za uzingativu
katika eneo moja ili uweze kutenda mambo yako kwa ufanisi na mafanikio. Itakuwa
ngumu sana kwako kuweza kufanikiwa ikiwa utashindwa kuvunja tabia hii. Je,
unawezaje hili;-
Hivi
ndivyo jinsi unavyoweza kujifunza kuweka nguvu za uzingativu eneo moja.
1. Chagua jukumu moja la muhimu
kutekeleza.
Asubuhi
unapoamka mara baada ya kusali na kufanya ‘meditation,’
kabla hujawasha simu yako anza kutekeleza jukumu lako la muhimu. Najua unaweza
ukawa una vitu vingi vya kufanya, lakini chagua kitu kiomoja tu cha kuanza
nacho na vingine vyote visahau kwa muda mpaka ukamilishe jukumu lako moja la
muhimu kwa wakati huo.
2. Jukumu ulilichagua lifanye kwa dakika
15 bila kuacha.
Katika
dakika hizi usikubali kuingiliane na kitu chochote, tumia dakika hizo vizuri
nguvu zako zote zihamishie hapo. Usichague dakika nyingi sana za kuanza kuweka
nguvu za uzingativu kwa pamoja, anza kwanza na dakika chache, ikitokea umeshindwa
dakika 15, punguza ziwe hata 10 au 5 lakini lazima uibuke mshindi.
3. Fanya kila siku na kwa kila kitu.
Ili tabia
hii iweze kukaa na iwe yako, fanya kila siku na kwa kila kitu kiwekee nguvu ya
uzingativu. Unapoamua kufanya kitu fulani mawazo yako yote hamishia hapo na bila
shaka hapo utakuwa na ufanisi mwema wa kazi yako. Lakini ikiwa utashindwa zoezi
hilo hiyo itakuwa ngumu kwa wewe kuweza kufanikiwa.
Inabidi
ieleweke kwamba, kuweka nguvu za uzingativu katika eneo moja kwa masaa kadhaa,
kwa siku kadhaa na kwa muda fulani maalumu kuna leta mabadiliko ya maisha yako
bila kipangamizi chochote.
Ni jukumu
lako leo kuanza kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kila ukifanyacho ili
kikuletee mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.