Sep 21, 2017
Mara Ngapi Umeshindwa Kufanikiwa Kwa Sababu Hizi?…
Ni
mara ngapi umekuwa ukitaka kubadilisha hali fulani hivi kwenye maisha yako,
lakini cha ajabu tena umekuwa ukikata tamaa kwa mara ya kwanza hasa pale
unapokutana na changamoto kwenye maisha
yako?
Ni mara
ngapi umekuwa ukijiwekea malengo yako na kusema lazima nitatimiza lengo hili,
lakini kitu cha ajabu umekuwa ukiyasahau malengo hayo mara moja na tena umekuwa
huyakumbuki kama vile hukuweka malengo kabisa?
Ni
mara ngapi umekuwa ukitoka nje ya mstari wa malengo yako uliyojiwekea hasa
kutokana na maoni au malengo ya watu waliokwambia kwamba huwezi kitu hiki na
wewe kutokana na kuwasikiliza ukaacha kweli?
Usikatishwe tamaa na chochote |
Ni mara
ngapi umekuwa ukisema utaweka akiba, ambayo itakusaidia baadae kuwekeza kwenye
maisha yako, lakini umekuwa hufanyi hivyo kutokana na sababu zako ambazo
unazijua wewe?
Ni
mara ngapi umekuwa ukitoa sana visingizio badala ya kutoa matokeo yanayotakiwa
kutolewa? Umeshawahi kujiuliza hili? Kila kitu unakuwa umejipanga kama vile
unataka kutoa sababu badala ya kutoa matokeo yanatakayokusaidia kwenye maisha?
Ni
mara ngapi umekuwa ukiishi maisha chini ya kiwango, maisha ya kuhuzunika na
kuacha kuchukua hatua sahihi ambazo hatua hizo zinaweza kukupeleka kwenye
mafanikio yako makubwa uyatakayo?
Muda
huu na wakati huu ulionao una mahusiano moja kwa moja na kesho yako ya
mafanikio. Hivyo, jinsi ambavyo umekuwa ukiahirisha mambo na kusema utafanya
hili na hufanyi, elewa kabisa ndivyo umekuwa ukijiangusha mwenyewe kwenye
maisha yako.
Unatakiwa
kuishi kwa nia moja na hamu kubwa ya kujitoa hadi kufikia mafanikio. Lakini kama
kila mara unasema unafanya hili halafu hufanyi, utakuwa unajenga tabia ambayo
moja kwa moja msingi wake mkubwa ni kukuangusha na si kufanikiwa.
Najua
changamoto kweli zipo katika maisha, lakini changamoto hizo isiwe sababu kubwa ya
wewe kuacha mipango yako kila mara na kutoka nje ya mstari. Wakati wa kufanya
na kutimiza ndoto zako ni sasa, fanya kitu.
Usikubali
kushindwa kwenye maisha yako kwa sababu ya kutokufanya, usikubali kushindwa eti
kwa sababu kila mara unaahirisha. Chukua hatua sahihi za kubadili maisha yako
ili ufikie mafanikio makubwa.
Tunakutakia
siku njema na endelea kujifunza maisha na mafanikio kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.