Sep 25, 2017
Ubora Wako Unatokana Sana Kufanya Hivi…
Kwa jinsi unavyofanya kitu chochote
kile kwenye maisha yako, ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi katika kitu hicho.
Kwa mfano, kama wewe ni
mwimbaji kwa jinsi unavyoimba kila siku na kufanyia mazoezi ndivyo unavyozidi
kuwa bora katika uimbaji wako.
Kama wewe ni mwandishi, kwa
jinsi unavyoandika kila siku, hivyo ndivyo unavyozidi kuwa bora katika uandishi
wako.
Kama wewe ni mtu wa
kujifunza vitu, kwa jinsi unavyojifunza, utashangaa unajikuta unakuwa ‘mlevi’ wa kutupwa wa kujifunza.
Kama wewe ni mtu wa
kulalamika, kwa jinsi unavyoendelea kulalamika, hivyo ndivyo sasa utakuwa
mlalamikaji mbobebezi, utalalamikia kila kitu.
Fanya kitu, uongeze ufanisi wako. |
Kama wewe ni mtu mwenye
tabia za kukopa kopa pesa kwa watu, utashangaa kwa jinsi siku zinavyokwenda
unakuwa mkopaji kweli na una madeni kibao.
Kama wewe ni mtu wa kutoa
sababu, basi hutafanya kitu cha maana, ni rahisi kuendelea kutoa sababu sana
karibu kwa kila mtu.
Kama wewe ni mtu wa visasi,
kuwa makini hapo, unaweza ukawa na mtu wa visasi kwa watu wengi sana kwa sababu
ndio kitu unachokifanya.
Kama wewe ni mtu
unayehakikisha jambo unalolianza lazima lifanikiwe, basi elewa utaendelea
kufanikisha pia mambo mengine kwenye maisha yako.
Kwa chochote unachokifanya,
bila kujali kitu hicho ni chanya au hasi utazidi kupta matokeo bora ynayoendana
na kitu hicho unachokifanya kila siku.
Hebu jaribu kuangalia katika
maisha yako ni kitu gani ambacho unakifanya sana? kwa kifanya kitu hicho utapata
matokeo yake.
Hivyo basi kila wakati, chagua
kufanya kwenye maisha yako mambo bora na fanya kila siku, baada ya muda utakuwa
bora kwenye mambo hayo na kufanikiwa vikubwa.
Ni vigumu sana kuwa mshindi
katika maisha yako kwa kufanya kitu mara moja na kutegemea mafanikio makubwa. Unatakiwa
kufanya kila siku.
Kwa hiyo unaona mafanikio au
kushindwa ni matokeo ya kufanya kitu fulani unachokifanya kila siku na kwa muda
mrefu.
Kufanikiwa au kushindwa
hakutokei mara moja kama wengi wanavofikiri, ni matokeo ya kuwekeza nguvu zako
kila siku kwenye jambo hilo.
Anza leo kufanya mambo
yatakayokusaidia kujenga ubora utakao kusaidia kufanikiwa sana na sio
yatakayokuangusha.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.