Sep 3, 2017
Sheria Za Lazima Kufuata Wakati Unatafuta Utajiri.
Kama
lengo lako katika maisha ni kutafuta mafanikio makubwa na hadi kufikia utajiri,
zipo sheria za msingi ambazo unatakiwa kuzifuata na kufanyia kazi ili
zikusaifdia kufika huko. Kwa kufuata sheria hizo zitakupa hamasa na mwongozo wa
kufikia mfanikio yako unayoyahitaji kwenye maisha yako.
1. Wekeza kwenye maarifa.
Unatakiwa
kuwekeza kwenye maarifa kila siku ili yakusaidie kutengeneza utajiri wako.
Ukiwa tajiri, halafu ukakosa maarifa sahihi, utajiri huo kuporomoka itakuwa ni
kitu rahisi sana. Unatakiwa kupata maarifa sahihi kila siku kwa kujisomea ili
kulinda utajiri wako wa kesho, maarifa ni kitu cha muhimu sana kwako.
2. Fanya kazi sana.
Tumekuwa
tukisema mara kwa mara, huwezi kufanikiwa sana kama unafanya kazi zako nusu,
nusu. Unatakiwa ufanye kazi sana ili kufikia utajiri wako. Kazi ndio kitu pekee
kitakachokufanikisha hata kama maisha yako yapo chini sana. Kama utatumia
sheria hii ya kufanya kazi kuliko, haitakuangusha utafanikiwa lazima.
Kila wakati jiandae kwa chanagamoto za mafanikio. |
3. Jiandae kwa changamoto.
Hakuna
mafanikio utakayoyapata bila kukutana na chamgamoto. Kwa hiyo unatakiwa kila
wakati kujiandaa na changamoto na uzishinde. Kama mafanikio yangekuwa ni rahisi
basi kila mtu angekuwa nayo. Hivyo, unaona wengi wanashindwa kwa sababu ya
changamoto hizi, ambazo wewe unatakiwa uzishinde.
4. Kataa madeni yasiyo na msaada.
Wakati
unaelekea kwenye safari yako ya utajiri, kuwa makini sana na madeni ambayo siyo
ya lazima kwako. Kama unakopa, kopa mkopo ambao moja kwa moja utauingiza kwenye
biashara lakini sio kukopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Unapokuwa upo
kwenye madeni sana, unakuwa unajiingiza kwenye utumwa ambao sio wa lazima
kwako.
5. Tengeneza picha kamili ya maisha yako
unataka yaweje.
Hutakiwi
kuishi tu kiholela, unatakiwa uwe na picha kamili ya maisha yako unataka yaweje
baada ya kipindi fulani. Jinsi maisha yako unavyotaka yawe, unaweza kuandika
kwenye karasi na kupitia karibu kila siku. Kwa kuishi kwa kanuni hii,
itakusaidia sana kufikia utajiri wako kwa uhakika.
6. Tumia kile ukifanyacho kwa makini
kukupa utajiri.
Chochote
unachokifanya kina uwezo wa kukupa utajiri. Hakuna kazi maalumu ambayo unaweza
ukasema kwa kuifanya kazi hiyo itakufanya lazima uwe tajiri. Kikubwa ishi kwa
kujua kwamba kazi yoyote unayoifanya, ukiifanya kwa umakini mkubwa na kwa
juhudi itakupa utajiri, hivyo acha visingizio chapa kazi.
7. Ishi maisha ya amani na watu wengine.
Hutakiwi
kuwa mtu mkorofi kwa watu wengine, tengeza maisha ya amani kwa watu wengi. Hakikisha
watu wengi wanafurahia sana uwepo wako. Hilo litakusaidia kupata watu wengi
watakaokusaidia katika safari yako ya mafanikio. Ukitumia kanuni hii itakuwa na
faida kwako sana wakati unaelekea kwenye utajiri.
Kwa kifupi,
hizo ndizo sheria za msingi ambazo unatakiwa uzifuate ili zikusaidie kufikia
mafanikio yako makubwa kila wakati.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.