Sep 30, 2017
Njia Ya Mafanikio Yako Ipo Hapa...
Mojawapo ya kosa kubwa linalofanywa
na watu wengi katika safari ya mafanikio, ni kule kukata tamaa hasa wanapokutana
na changamoto.
Kwa kukata tamaa huko kwa
sababu tu ya kukutana na changamoto, naweza nikasema ni moja ya kosa ambalo linaweza
kukufanya usifanikiwe.
Washindi katika maisha
wanajua kwamba, changamoto au kushindwa kwa namna moja au nyingine sio ‘tiketi’ pekee ya kuanza kukata tamaa
mapema.
Inapotokea kitu hakijaleta
majibu unayoyataka, sio swala la kukimbilia kukata tamaa bali ni kubadilisha
njia hadi uweze kufanikiwa.
Inawezekana kabisa njia
unazotumia ni butu na hazifai, sasa hapo sio rahisi sana kuweza kufanikiwa,
bali kufanikiwa kunakuja kutokana wewe kutumia njia mbadala.
Kama njia ya kwanza
imekataa, jaribu ya pili na kama ya pili imekataa, jaribu ya tatu na nyingine
na nyingine tena mpaka kuweza kufanikiwa.
Ipo njia ya kukufikiasha
kwenye mafanikio yako, njia hiyo ipo. Ili uifikie njia hiyo, acha kukata tamaa
mapema. Sumu kubwa sana ya kufanikiwa kwako ipo kwenye kukata tamaa.
Jifunze sana kutokana na
matokeo yanayokatisha tamaa na kisha baada ya hapo tafuta njia mpya
utakayoitumia kufanikiwa tena.
Kuendelea kufanya tena na
tena hata kama unashindwa ni njia muhimu ya kukusaidia kufanikiwa. Kwani amini
njia ya mafanikio yako ipo, huhitaji kukata tamaa.
Kama nilivyokudokezea watu
waliofanikiwa wanatumia njia nying sana, ambazo njia hizo huwasidia kuweza
kufikia mafanikio yao.
Hata wewe unaweza kutumia
njia hizo pia. Lakini usiwe mtu wa kukimbilia tu kuacha kila kitu hasa
unapokutana na changamoto.
Maisha ya watu wengi yapo
hatarini na ni magumu kwa sabbu ni watu wa kuacha tu hasa wanapokutana na
changamoto.
Watu hawa hawajafundishwa au
hawajui kutumia njia mbadala, ila wao wanachojua ikitokea changamoto dawa ni
moja tu ni kuacha.
Ukiwa hata wewe ni mtu wa
kuishi maisha ya namna hii, itakuwia vigumu sana kuweza kufikia mafanikio yako
makubwa.
Siri ya wewe kufanikiwa
unatakiwa kujifunza kufanya jambo kwa namna nyingi sana, ambazo zitakupa
mafanikio na sio kukata tamaa kila unapokuatana na changamoto.
Unachotakiwa kuelewa hapa kupitia
makala hii ya leo ni kwamba, njia ya mafanikio yako ipo, acha kukimbia mapema
kwa sababu ya changamoto. Changamoto zipo na ni za muda.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.