Sep 14, 2017
Mbinu Zitakazo Kusaidia Kuwa Bora Katika Maisha Yako.
Katika
maisha yako unahitaji kutambua mambo mbalimbali yatakayokufanya uweze kuwa bora
zaidi, huwezi kusema unataka mafanikio wakati mambo ambayo unajua ni yale mwaka
47. Hivyo kwa kila jambo ambalo unataka kuwa bora katika eneo hilo ni vyema
ukajua ni kwa namna gani utaweza kuwa bora. Swali linaweza kunijia ghafla, sasa
nafanyaje ili kuwa bora?
Ipo
hivi ukitaka kuwa bora katika maisha yako unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;
Anza kuwa mwaminifu kwenye mafanikio yako. |
1.
Kuwa
mwaminifu.
Bila
uaminifu katika maisha yako, basi ujue fika mafanikio utayasikia kwa majirani
zako waliofanikiwa. Na moja kati ya kushindwa kufanikiwa kwa maisha yetu
husasani sisi vijana ni kwamba wengi wetu hatuaminiki.
Wapo
baadhi ya watu wakipata kazi huwa wanakuwa wanyenyekevu sana, ila baada siku
chache mara baada ya kuizoea kazi hiyo
huwa wanakuwa ni watu ambao hawaminiki hata chembe, roho na hulka zao ni kutaka
kufanikiwa kwa haraka wapo baadhi ya watu hudiriki hata kumuibia mtu ambaye
ameawajiri. Kufanya hivyo hufanya mwajiri wake kumfukuza kazi, hata kupelekea
doa kwa vijana wengi ya kwamba vijana hatuaminiki.
Hivyo
iwe ni mwajiriwa au umejijiri siri kubwa ya kuweza kufanikiwa zaidi ni
kuweza kujijengea misingi ya uamifu, kwani uaminifu ni siraha iyoisha
risasi katika mapambano ya maisha.
2.
Weka
vipaumbele.
Maisha
bila kuwa na vipaumbele ni sawa yule muhenga aliyesema mtegemea cha nduguye hufa
maskini. Mtu ambaye hana vipaumbele huwa mara nyingi hana muongozo rasmi wa
maisha yake na ndio maana hata ukimwambia fanya hiki hata kiwe ni kibaya huwa
yupo tayari hii ni kwasababu huwa hana kanuni ambayo inaongoza maisha yake bali
huwa yupo tayari kuwasikiliza watu wengine wanasema afanye nini, kwa mantiki
hii si sawa hata chembe kama kweli unataka mafanikio ya kweli.
Mara
nyingi nimekuwa nikisema hatma ya maisha yako unayo wewe mwenyewe hivyo kila
wakati usiwe ni mtu wa kuyumbishwa na jamii ambayo inakuzunguka, hivyo jifunze
kuweka ni vipaumbele, hii itakusaidia wewe kwa kiwango kikubwa kujua ni jambo gani la kufanya na ni lipi si
la kufanya.
Kuweka
vipaumbele humsaidia mtu katika kiwango kikubwa kuweza kutimiza kusudio lake
kwa kiwango kikubwa, endapo utaamua kufanyia kazi vipaumbele hivyo, huwezi
kusema unataka kuwa bora harafu vipaumbele ulivyoweka ukawa huviweki katika
matendo. Hivyo daima jifunze kujikuweka vipaumbele katika maisha yako.
3.
Fanya
kazi kwa ustadi.
Sambamba na hilo ili uweze
kuwa bora katika maisha yako jifunze kufanya kazi kwa ustadi, na kufanya mambo
yale ya msingi. Mara nyingi epuka kufanya kazi zisizo za msingi kwani kufanya
hivyo ni kupoteza muda. Na katika kufanya kazi hizo za msingi ni kwamba lazima
uwaze ni kwa jinsi gani kazi hiyo inavyoweza kukupitia kipato.
4.
Thamini
muda ulionao.
Ili uweze
kuwa bora kila wakati katika maisha yako ipo haja ya wewe kuweza kuthamini thamani ya muda ulionao
katika kufanya kazi. Huwezi kusema unataka mafanikio harafu huwezi kuuheshimu
muda ulionao. Muda ulionao ni mtaji nambari mbili, hii baada ya kupata mtaji nambari moja, ambao ni
mtaji wa uhai. Mtaji muda, wengi wetu tumekuwa tunaupoteza pasipo kujua, hivyo
kila wakati ni vyema ukajua thamani ya muda ulionao katika kuyabadilisha maisha
yako.
Kwa
leo naomba niiishie hapa tutakuna siku nyingine ambapo tutazungumza kwa kina zaidi kuhusu mbinu nyingine ya kuwa bora
katika maisha.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson
chonya
0757909942
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.