Sep 15, 2017
Aina Ya Wateja Ambao Unatakiwa Kuwaepuka Mapema Kwenye Biashara Yako.
Katika
biashara ni kawaida kukutana na wateja wa aina tofauti tofauti na wateja wote
kama tujuavyo ni muhimu na hutakiwi kumpa huduma yako mteja vibaya hadi
ajisikie kwamba hataweza tena kuja kwenye biashara yako.
Mteja
anatakiwa kujaliwa na kupewa huduma ambayo itamfanya ajione kwamba yeye ni
mfalme kwa mazingira yoyote yale uliyo. Naamini hilo linawezekana sana kwako na
unatakiwa kulifanya hilo katika uhai wote wa biashara yako.
Pamoja
na kwamba mteja anatakiwa kujaliwa hivyo na ni muhimu, lakini, wapo aina ya
wateja ambao inatakiwa kuwa nao makini sana katika biashara yako ili wateja
hawa wasije wakaleta matatizo mengine kwenye biashara yako.
Wateja
hawa ni wateja gani? Twende pamoja kujifunza;-
Jenga umakini na wateja wako. |
1. Wateja wanaolalamika sana.
Wapo
wateja ambao kazi yao ni kulalamika sana. Wateja hawa wanalalamikia kitu hiki
au kile kwenye biashara na kushindwa kuongea ukweli na kutatua changamoto za
pamoja. Wateja hawa ni hatari sana kwenye biashara yako.
Wateja
hawa ni moja ya wateja unaotakiwa kuwaepuka sana. Ni rahisi kukuharibia
biashara yako na kusababisha wateja wengine wakukimbie kwa sababu ya kulalamika
sana kusiko na msingi. Wateja wapya watafikiri kweli bidhaa zako ni mbovu kumbe
la.
2. Wateja wanaokupotezea muda sana.
Pia
wapo wateja ambao naweza kusema wao ni kama wana nia ya kukupotezea muda wako. Wateja hao si ajabu
ukakuta wanauliza kitu fulani kwa muda mrefu sana na wanakiangalia na
kukichunguza hata bila ya kununua pengine.
Unachotakiwa
kuwa makini nacho hapa ni kuwa makini na wateja wa namna hii unapokutana nao
ana kwa ana na hata wale unaokutana nao kwenye mitandao. Fanya hivi bila wao
kujua kwamba unawaepuka.
3. Wateja wanaojiona wao ni maalumu
sana.
Kuna
wateja ambao wanapenda kujiona wao ni muhimu sana kuliko wateja wengine. Wateja
hao ni rahisi tu kudai namba ya meneja wako au bosi wako ili wamweleze kile
wanachokitaka wao wenyewe.
Kwa
kifupi unapokuwa na wateja hawa nao ni wasumbufu sana na wanapenda kufanya kila
wanachokitaka kwenye biashara yako ilimradi tu waonekane. Hivyo unatakiwa kuwa
makini nao na kujua pia jinsi ya kuwakabili ii wasilete matatizo mengine.
4. Wateja wanaotaka kupatanisha kila
kitu.
Sina
shaka unawajua wateja ambao ukiwatajia bei ya kitu, wao ni kutaka kupatanisha
na kuomba punguzo kila wakati. Unapokuwa na wateja wa namna hii wengi basi
biashara yako itakuwa na usumbufu sana.
Vipo
vitu ambavyo havihitaji kupatanishwa, bei na kila kitu kinaeleweka, sasa
unapokuwa na mteja anayetaka kila kitu kiwekwe kwenye mapatano hapa unatakiwa
pia uwe makini sana, vinginevyo utafanya biashara kwenye mazingira magumu.
Hawa
ndio wateja ambao unatakuiwa kuwaepuka au kuwa nao makini sana kwenye biashara
yako. Sijasema wateja hawa uwafukuze au uwajibu vibaya, ila unatakiwa kuwa nao
makini ili wasije wakakuvurugia wateja wengine ambao ulitakiwa kuwa nao kwenye
biashara.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.