Sep 4, 2017
Weka Pembeni Tabia Hizi, Ujenge Maisha Ya Mafanikio Unayoyataka.
Je, uko tayari kufanikiwa kwa namna yoyote ile? Je, kuna
changamoto unazopitia na zinakuzuia kufanikiwa, ingawa wewe kiu yako ni kutaka
kuona mafanikio yakiwa kwenye maisha yako? Endapo utamuuliza mtu yeyote swali
hili, wengi sana watakwambia, ndio wanataka kufanikiwa, tena utajibiwa kwa
haraka sana.
Lakini hata hivyo ni kweli, karibu kila mtu katika maisha yake ana
kiu ya kufanikiwa lakini si kila mtu anajua jinsi ya kufanya ili kufanikiwa.
Kuna vitabu vingi vimeandikiwa, na makala nyingi zimeandikwa zikieleza kwa wazi
nini unapaswa kufanya ili kufanikiwa, na nini ambacho unatakiwa kuepuka sana
ili kufanikiwa.
Pamoja na wingi wote wa vitabu na makala hizo za mafanikio, lakini
bado watu hawafanikiwi, wamekuwa ni watu wa maisha yale yale, mpaka unaweza
ukaa chini ukajiuliza hivi, shida kubwa ipo wapi? Leo kupitia makala haya, nataka
nikukumbushe kwa kifupi sana, baadhi ya tabia unazotakiwa uziweke pembeni ili
ufanikiwe.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia ambazo
unatakiwa kuziweka pembeni kwa haraka
sana ili kufanikiwa.
1. Ubinafsi.
Sumu mojawapo kubwa katika biashara na mafanikio kwa ujumla ni
ubinafsi. Haitakiwi kuwa mbinafsi unapokuwa kwenye biashara, inatakiwa kutoa
ushirikiano na kwa wengine ili mafanikio yako ya kibiashara yaweze kukua. Ukiwa
mbinafsi, utakosa ushirikiano kwa wengine na utakwama.
2. Hofu.
Hutaweza pia kufanikiwa kama kila wakati kama una hofu kubwa
kwenye kila kitu unachotaka kukifanya. Hofu zako zote ulizonazo, zitupe kule. Hofu
ni sumu na kizuizi kikubwa sana cha mafanikio yako. Hata hivyo kila mtu ana
hofu, lakini hofu zako pia unatakiwa kuzishinda hadi kuchukua hatua kwenye
ndoto zako.
3. Uvivu
Je, umeshawahi kukutokea asubuhi ambapo kunapokucha unakuwa
unajishauri uamke au usiamke, ndani yako kuna kuwa na mabishano mengi sana ya
nini ufanye? Kama hali hiyo ilishawahi kukutokea basi ni dalili mojawapo ya
uvivu, ambapo ni kitu kimojawapo unachotakiwa kukitupa kule ili uweze kufanikiwa.
4. Hisia
hasi.
Kuendelea kuwa na hisia hasi, wakati unatafuta mafanikio, huko ni
kujitafutia balaa la kushindwa kwenye maisha yako. Hisia hasi ni mbaya katika biashara
yako, hisia hasi ni mbaya katika maisha yako pia. Zinakufanya ushindwe kufanya
mambo yako kwa ufasaha nakujiona kuwa ni mtu kama wa visasi, ziepuke hisia hizi
ili ufanikiwe.
5. Waepuke
watu hasi sana.
Kama unataka kuwa na mafanikio, epuka sana watu hasi, watu ambao
wanaweza kuwa sumu kubwa kwenye maisha yako. Watu hawa hawawezi kukusaidia kitu
chochote zaidi watakurudisha nyuma kutokana na maneno yao, kutokana na
hisia zao. Wakimbie watu hawa ili
utengeneze mafanikio yako.
Je, unataka kubadilisha maisha yako? basi,
leo tunakwambia hivi, anza kubadilisha kwanza tabia zako na kutupa kule tabia
zisizofaa.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.