Sep 12, 2017
Hizi Ndizo Aina Kubwa Za Hofu Zinazotawala Kwenye Maisha Ya Watu Wengi.
Kwenye
maisha zipo hofu ambazo zinatawala maisha ya wanadamu wengi kama sio wote. Hakuna
mtu ambaye hana hofu hizo, isipokuwa hofu hizo zinakuwa zinatofautiana kati ya
mtu mmoja na mtu mwingine. Wengine
utakuta ni watu ambao wana hofu hizo nyingi zaidi na wengine wana hofu hizo
chache.
Kupitia
makala yetu hii ya leo, nataka tujifunze pamoja aina za hofu ambazo
zinawasumbua watu wengi sana duniani. Kwa mujibu wa mwandishi nguli wa vitabu
dunia, Napoleon Hill ameeleza hofu hizi ambazo karibu kila binadamu
anazo dunia zipo hofu kubwa za aina sita.
1. Hofu ya kuogopa kifo.
Karibu
kila mtu aliye duniani linapokuja swala la kifo limekuwa likitishia amani au
hofu kubwa sana. Hii inasemekana ni hofu ya kwanza ambayo watu wengi wanayo. Wengi
wanahofia sana hasa wanapokumbuka kuna kufa.
2. Hofu ya kuogopa umaskini.
Harakati
nyingi za maisha ya watu wengi duniani zinatokana na watu kupigana kuupinga
umaskini. Hii pia ni hofu ambayo binadamu anayo, hataki kabisa kuuona umaskini
ukiwa donda ndugu kwenye maisha yake. Wengi wamekuwa wakiishi kwenye hofu hii
sana.
3. Hofu ya kuogopa uzee.
Pia hofu
hii inatawala kwa wengi hasa wanapokumbuka kwamba uzee unakuja. Kila mtu anatamani
aishi maisha yake akiwa kijana siku zote lakini ni kitu ambacho hakiwezekana
kutokana na sababu za kimaumbile inakulazimu kuzeeka.
4. Hofu ya kuogopa kukataliwa na mwenzi
wako.
Binadamu
pia wamekuwa ni waoga kukataliwa na wenzi wao hasa wale wanaowapenda kwa dhati
kutoka mioyoni mwao. Aina hii ya hofu pia inawatesa wengi hasa lile kundi
linalopendana kwa moyo mmoja.
5. Hofu ya kuogopa kuwa na afya mbovu.
Ugonjwa
pia ni kitu ambacho kimekuwa kikimtishia sana binadamu. Kila binadamu anapenda
afya yake iwe bora wakati wote. Kwa sababu hiyo, hii ni hofu ambayo kila mtu
amekuwa karibu anayo isipokuwa zinatofautiana tu.
6. Hofu ya kuogopa kukosolewa.
Kila
mtu napenda kile anachokisema kikubalike na wengine. Hakuna mtu ambaye anapenda
akosolowe sana. Kwa hiyo kutokana na hilo hii ni mojawpao ya hofu inayowasumbua
watu wengi duniani, nikiwa na maana wengi hawataki kukosolewa, ukitaka ugomvi
mkosoe mtu, utaona.
Kama
nilivyoanza kusema hofu hizi zinatofautiana kati ya mtu mmoja na mtu mwingine. Lakini
hizo ndizo hofu kubwa zinazotawala maisha ya mwanadamu wakati wote.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio.
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.