Sep 29, 2017
Maeneo Manne Ambayo Unatakiwa Kuwa Msikivu Sana Ili Kujenga Mafanikio Yako.
Usikivu
ni moja ya kitu muhimu sana katika safari yako ya mafanikio. Unapokuwa msikivu
inakusaidia kujifunza mambo mengi sana tofauti na ambapo ungejifanya wewe ni
mjuaji wa kila kitu hali ambayo ingekufanya ukose mengi.
Kitu
cha kujiuliza ni watu wangapi ambao ni wasikivu, bila shaka ni watu wachache
sana ambao wanajenga utulivu wa kusikiliza wengine wanasema nini au wao wenyewe
ndani mwao wanasema nini hadi kuweza kufanikiwa.
Kwa kawaida
tunapozungumzia usikivu, wengi wanajua ni usikivu wa kuwasikiliza tu watu
wengine. Lakini jinsi ilivyo upo usiku wa aina nne ambao kila mtu anatakiwa
kuwa nao makini ili kujenga mafanikio yake.
Jenga hali ya usikivu mkubwa ili kujifunza. |
1. Usikivu kwa wengine.
Unatakiwa
kujifunza kusikiliza wengine wanasema nini, nini maoni yao kwako bila kujali wanachokisema
ni chanya au hasi. Kuna kitu cha msingi na cha kubadili maisha yako utakipata
kama ni msikilizaji wa wengine kuliko ambavyo ungebaki wewe kama wewe ukawa
unafuata yako bila kusikiliza mtu yeyote.
2. Usikivu kwako wewe mwenyewe.
Pia unatakiwa
kujisikiliza mwenyewe na kuheshimu maoni yako. Pengine unajiuliza kivipi? Ndani yako kuna sauti ambayo huwa inasema na wewe. Sasa, kuwa makini kusikiliza sauti
yako, maana hio ni muhimu sana kuliko hata sauti zinazotoka nje. Ukiwa msikivu
kwako utapata uwezo wa kujenga pia mafanikio yako.
3. Usikivu kwa dunia.
Kwa jinsi
tunavyoishi, dunia inatufundisha mambo mengi. Unapopata changamoto kuna vitu
unajifunza na kwa namna hiyo unatakiwa kujua kujifunza jinsi dunia inavyosema
na wewe. Utakuwa ni mtu wa ajabu kama hutaki kabisa kujifunza kutokana na dunia.
Yapo mafundisho mengi sana unayoyapata hata
huhitaji kwenda shule.
4. Usikivu kupitia maarifa.
Vile
vitu unavyojifunza vina sema bila kujali ni maandishi au kitabu. Sasa jifunze
kusikiliza kile ambacho waandishi wanasema, kitabadilisha maisha yako kuliko
jinsi ambavyo unang’ang’ana na kuwa mbishi bila kutaka kubadilika. Ukiweza
kuyatumia maandishi vizuri yatakusaidia sana kuboresha maisha yako.
Hayo
ndiyo maeneo muhimu ambayo unatakiwa kuwa msikivu sana ili yaweze kukusaidia
kujenga mafanikio yako. Fanyia kazi maeneo hayo ili yawe msaada mkubwa kwako.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.