Sep 13, 2017
Ikiwa Utajua Hatma Ya Maisha Yako Iko Hivi…Utafanya Nini?
Ikiwa
leo utajua kwamba utasababisha matokeo ya aina fulani kwenye maisha yako kama
tu utafikiri kwa makini, utachukua hatua sahihi, utaweka nguvu za uzingativu
siku hadi siku na hatua kwa hatua, ni kitu gani utakachofanya cha ziada, hebu fikiri?
Ikiwa
tena leo utajua kama utaondoa kila aina ya shaka ndani mwako hiyo itakusaidia
kutimiza malengo yako mapema, unafikiri ni kitu gani utajitoa kukifanya kwa
ukamilifu kabisa katika maisha yako na kuwa huna shaka nacho hadi ukifanikishe?
Ikiwa
utajua imani yako na kufikiri kwako kwa namna fulani ndiko kunako umba maisha
yako yawe kama hivyo yalivyo, je, unafikiri utachagua imani ipi na kufikiri kwa namna gani ambako kutakusaidi
kubadilisha maisha yako?
Fikiri vizuri hatma ya maisha yako. |
Ikiwa
utajua pia nidhamu binafsi ndio msingi wa kukutengenezea maisha ya mafanikio
unayoyataka, je, unafikiri utajenga nidhamu ipi binafsi ambayo itakusaidia
kujenga maisha ya mafanikio makubwa maishani mwako?
Ikiwa
utajua juhudi endelevu, juhudi za kila siku, juhudi ambazo hazina kikomo
zikiambatana na kujifunza haziwezi kukuacha salama mpaka zikuache ukiwa na
mafanikio, je, unafikiri utaweka juhudi hizo kwa muda gani bila kuchoka?
Ikiwa
utajua umebakiza siku chache sana za kuishi duniani, maisha utakayoishi,
utaishi maisha ya aina gani, muda utakaokuwa ukiutumia utakuwa unatumia muda
wako kwa namna gani, ilimradi tu kuhakikisha unatimiza ndoto zako kwa muda
mfupi?
Ikiwa
utajua fursa za mafanikio zipo kila mahali na ikiwa utajua namna ya kufikia
mafanikio yako, je unafikiri ni kitu gani ambacho utafanya ili kuzitumia fursa
hizo kwa uhakika mkubwa hadi kufanikiwa?
Kimsingi,
ipo nguvu kubwa sana ya kutenda kwa ziada au kutenda hovyo kama utajua hatma ya
maisha yako inaishia wapi? Hapo tu inategemea umejua nini kwenye akili yako. unachotakiwa
kutambua kwanza je, unajua nini?
Mara
nyingi wengi wanashindwa sana kwenye maisha yao au wanatenda hovyo kwa sababu
ya kutokujua hatma za maisha yao zinaishia wapi. Lakini hata inapotokea ukajua,
je, unatumia kujua huko kukusaidia kufanikiwa?
Kitu
cha msingi unachotakiwa kuelewa ni kwamba, ikiwa utajua kile unachotakiwa
kukifanya kwamba ni cha msingi na kinakupa mafanikio makubwa, ni kitu gani
ambacho utakifanya cha ziada na kikakupa manufaa na mafanikio?
Acha
kuwa miongoni mwa kundi la watu ambao wanachezea sana fursa za mafanikio ingawa
wana kila kitu wanachokijiua. Kuwa miongoni mwa watu wachache ambao wanafaidi
kwa kujua kwao mambo au vinginevyo unataka kuendelea kuteseka?
Maisha
ya mafanikio yanakuja kutokana na kujua vitu na kisha vitu hivyo kuvifanyia
kazi na sio kujua tu peke yake na kuviacha vitu hivo vikiwa hewani bila msaada
wowote. Jilulize leo kujua kwako kuna kusaidaia?
Je,
kwa sasa unakutumia kujua kwako yale mambo ya msingi kuweza kukusaidia
kufanikiwa katika maisha yako? Ikiwa utajua leo, umebakiza mwaka mmoja ili ufe
nini ambacho utafanya, juhudi zipi utaweka na mikakati ipi utaweka?
Anza
leo kuishi kwa kutumia falsafa ya ikiwa utajua…itakusaidia sana kuweza kubadili
maisha yako na kuwa ya tofauti. Je, uko tayari ikiwa utafanya hivi… maisha yako
yakatakuwa vile?
Chukua
hatua na kufanyia kazi mambo haya ya msingi uiyojifunza hapa, au je bado
unasitasita kuchukua tena hatua?
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.