Sep 8, 2017
Ijue Nguvu Na Siri Iliyopo Katika Matumizi Sahihi Ya ‘Diary.’
Je unaifahamu
‘diary’, unayajua matumizi yake kwa
usahihi?Nimeanza kwa kuuliza swali hilo ili tuweze kujua ukweli, maana watu
wengi wanaijua ‘diary’ ila hawajui
matumizi ya ‘diary’ hiyo. Wengi wetu
huwa tunachanganya sana, wengi tumekuwa tukifanya matumizi ambayo yalitakiwa
yafanyike kwenye notebook utakuta yanafanyika kwenye diary. Kama na wewe hujui
nguvu iliyopo kwenye diary nakusihi twende sawa makala haya.
Kwanza kabisa
naomba utambue ya kwamba kuna tofauti kubwa kati ya diary na notebook. Na
miongoni mwa kitu kikubwa ambacho hutafautisha vitu hivyo viwili ni; katika
diary katika kurasa kumeandikwa tarehe, mwezi pamoja na mwaka ila katika
notebook hakujandikwa vitu hivyo. Tarehe, mwezi pamoja na mwaka ambavyo
vimeandikwa katika diary havijandikwa kama mapambo au havijandikwa kwa
bahati mbaya ila vimeandikwa kwa sababu maalum.
Najua bado
unashangaa, na unataka kujua nini nguvu na siri iliyojificha katika diary, wala
usipate tabu ukweli upo hapa leo. Unajua walioitengeneza diary walikuwa na
akili zao timamu, Waliitengeneza kwa kuweka mwaka, mwezi pamoja na tarehe ya
siku husika, ili kukupa mwangaza wa namna ya kuitumia.
Na katika
kuitengeneza vile walitaka diary ile iandikwe mambo ya msingi kwa kila siku,
narudia tena walioitengeneza diary walitaka diary ile iandikwe mambo ya msingi
kwa kila siku. Lakini lengo lao halikuwa sio kila kitu ni lazima kiandikwe
katika diary. Najua unajiuliza ni mambo gani ya msingi ya kuandika katika
diary?
Ipo hivi,
kama ambavyo nilisema nilazima uandike mambo ya msingi katik diary yako
kwa kila siku na kwa tarehe husika , mwezi na mwaka husika, isitokee
akaruka hata siku moja bila kuandika katika diary yako. Kwa mfano unaweza
kuandika kila siku mambo ya msingi ambayo unataka kuyafanya kwa siku husika na
siku hivyo ukafanya tathimini umetimiza jambo hilo kwa kiwango gani, kama
umeshindwa kutimiza angalia ni wapi palipokufanya ushindwe kutimiza jambo hilo,
majibu yote ambayo utayapata hakikisha unayaandika pia katika diary yako, kisha
unaweka utaratibu wa kujikumbusha mara mara ili kupata ufumbuzi.
Kufanya
matumizi ya aina hiyo katika diary yako, kutakusadia wewe katika kutimiza
malengo yako. Lakini ikumbukwe ya kwamba diary sio sehemu ya kuandikia
notes ambazo haziusiani na mambo ya msingi yanayoihusu siku yako, bali diary ni
kijitabu cha kuandika mambo yahusianayo na malengo ambayo unatakiwa kuyatimiza
siku husika.
Hivyo kabla
sijaweka nukta ni imani yangu umenielewa vyema, hivyo nakusihi uweze kuwa na
diary yako na uweze kuandika kile ambacho nimekieleza hapo juu, kwani endapo
hautafanya hivyo basi jiandae kubaki na maisha yale yale ya kila siku.
Ndimi afisa mipango: Benson Chonya
0757909942
bensonchonya23@gmail.com
bensonchonya23@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.