Sep 6, 2017
Ijue falsafa Hii Ya Pesa, Jinsi Inavyowatofautisha Kati Ya Watu Maskini na Matajiri.
Uliwahi
kusikia ya kwamba pesa ina makelele? Kama hujawahi kusikia ngoja nikwambie kitu
leo kuhusu pesa. Pesa hii ambayo unaifahamu ndiyo ambayo inatufanya wengi wetu
tuweze kuisaka usiku na mchana, hii yote ikiwa ili mradi maisha yetu yaweze
kuimarika kwa kiwango fulani.
Lakini
licha ya kuipata fedha hiyo, wengi wetu fedha hiyo imekuwa si rafiki kwetu, hii
ni kwa sababu moja kati ya sifa kubwa ya watu ambao hawana mafanikio ni kwamba wamekuwa
na maisha ya kawaida, hii ni kwa sababu watu hao wamekuwa wanaifanyia kazi
pesa, ila pesa hiyo kwa upande wao
imekuwa haiwafanyii kazi.
Na
hali yote hutokea kwa sababu kubwa moja, wengi wamekuwa hawataki kuifanya pesa
izalishe kwa wingi, wengi kila pesa ambayo wamekuwa wakiipata wamekuwa
wakiifanya katika matumizi ambayo yanaifanya pesa hiyo ipotee bure. Hebu jaribu
kutafakari ni pesa kiasi gani ambazo zimepita mikononi mwako, na je pesa hizo
zimejizalisha kwa kiwango gani?
Ukiwa na falsafa sahihi ya pesa utafanikiwa. |
Bila
shaka majibu ya swali hilo utagundua ya kwamba ni pesa nyingi zimepita mikono
mwako na hujawahi kufanyia kitu chochote cha maana. Hivyo kwa misingi hiyo
utagundua ya kwamba wengi wetu tumekuwa ni watumwa wa fedha, hii ni kwa sababu
pesa imekuwa ikitupelekesha hasa pale ambapo tunapoipata.
Na
ndiyo maana hapo awali nilikuuliza uliwahi kusikia ya kwamba pesa ina makele?
Maana yangu ilikuwa ni hii; ninaposema pesa ina makele nina maana ya kwamba,
mara baada ya mtu kuipata pesa amekuwa hajui ni nini cha kufanya. Utakuta mtu
akipata pesa kila kilichopo mbele yake anataka kukinunua, kwa misingi hiyo
utagundua ya kwamba ni utumwa kiasi gani tulionao katika fedha.
Hivyo
Ili uweze kufanikiwa kifedha, ipo falsafa ya mafanikio ambayo inatumika
kuwaongoza watu na hadi kufikia mafanikio hayo makubwa sana ya kifedha. Falsafa
hiyo ndiyo inayopelekea wengine wakawa na pesa na wengine wakawa hawana,
wengine wakawa matajiri na wengine wakawa maskini.
Kwa
mfano, falsafa kubwa ya watu wenye mafanikio hasa linapokuja suala la pesa,
ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa iko hivi; watu wenye mafanikio
falsafa yao ipo kwenye kuwekeza kila aina ya pesa wanayoipata hata iwe ndogo
vipi. Na kile kiasi kidogo kinachobakia
hukitumia katika katika matumizi ya kawaida, lakini mara baada ya kuwekeza.
Wakati
watu ambao hawajafanikiwa nao pia falsafa yao ya pesa ni kutumia kila pesa
wanayoipata na kiasi kidogo kinachobakia hicho ndio huanza kujaribu kuwekeza.
Watu wasio na mafanikio, matumizi ndio kipaumbele cha kwanza kabisa kabla ya
uwekezaji wowote ule.
Bila
kujali shida zetu tulizonazo, changamoto mbalimbali, Ili kufanikiwa unatakiwa
kujiwekea falsafa ya pesa kama wanavyofanya matajiri, ni lazima uanze kuwekeza
kwanza hata kwa pesa kidogo, halafu matumizi yatafuata, kinyume cha hapo
utakwama sana na utashindwa kufikia uhuru wa kipesa.
Je, unavyofikiri kwa falsafa hizo mbili, je,
hali ya maisha inaweza ikawa sawa kwa watu hao wawili kutokana na matumizi ya
hizo falsafa? Najua majibu mpaka hapo unayo kwamba falsafa ipi ni sahihi. Kama
utatumia falsafa ya pesa ya watu wasiofanikiwa, tambua utakuwa hivyo na
ukitumia falsafa ya pesa ya watu wenye mafanikio, utafanikiwa pia.
Mwisho
tuweke nukta kwa kusema ya kwamba ni vyema uifanye pesa ikufanyie kazi kuliko wewe kuifanya pesa kazi, kwani kufanya hivyo
ni kuwa mtumwa.
Imeandikwa Kwa ushirikiano wa Imani
Ngwangwalu & Benson chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.