Nov 29, 2017
Ukiruka Mfumo Huu…Umeshindwa Tayari.
Kama
wewe ni msikilizaji mzuri wa muziki, utakubaliana nami kwamba CD nyingi
zimetengenezwa kwa mfumo ambao kama hutaki kusikiliza wimbo unaochezwa basi una
uwezo wa kurusha mbele na kusikiliza wimbo mwingine unaotaka.
Kwa hiyo
utakuta CD moja yenye urefu wa saa moja , unaweza ukaisikiliza hata kwa dakika
ishirini tu, hiyoni kutokana na kuruka ruka huko na pia kuchagua vile vipande muhimu ambavyo
wewe unavitaka na unaviona vya muhimu kwako.
Kwa wengi
wetu tumekuwa tukitaka kujaribu kuishi maisha yetu kwa mfumo kama huo. Tumekuwa
ni watu wa kutaka kuruka vitu vingi au kuishi maisha yaliyopita na kusahau
kuishi sasa na kufanya yanayotuhusu kwa sasa.
Unatakiwa
kuishi maisha yako kama pumzi. Kwa mfano, huwezi ukasema ukavuta pumzi nyingi
leo ili kesho usivute na eti ukabaki unaishi, hicho ni kitu ambacho
hakiwezekani hata kidogo katika maisha yote, ni lazima utumie pumzi yako sasa. Hakuna
pumzi ya akiba.
Na yale
tunayofanya au kwa jinsi unavyoishi, inatakiwa tuishi sasa na si kuishi jana au
kesho. Ukimua kuishi leo na kukazana kufanya ya leo basi uwe na uhakika
utajijengea uwezo wa kutengeneza mafanikio yako moja kwa moja na unakuwa
unaishi kwenye mfumo sahihi jinsi maisha
yanavyotaka.
Wengi
wetu wana shindwa kwa sababu ya kuamua kuishi maisha yao kwa kuyarusha. Utakuta
mtu yupo leo, lakini anaishi kesho. Kuishi maisha kwa namna hiyo huko ni
kujipotezea maisha yako moja kwa moja. Kuruka mfumo unavyotaka, ni sawa na
kuamua kushindwa kabisa.
Unatakiwa
ukumbuke kila wakati, maisha yetu yametengenezwa kuishi kwa mfumo. Kuishi kwa
mfumo sahihi pasipo kuuruka huko ndiko kunapokupa mafanikio. Ila kama utaishi
kwa kuruka mfumo wa aina fulani huko ndiko kujitengenezea anguko kubwa la
kushindwa kwenye maisha yako.
Leo ni
siku yako ya kufanya mambo makubwa. Kesho itakuja kwa wakati wake, kikubwa
kwako fanya mambo yako leo kwa uhakika
mkubwa. Ishi kwa mfumo kama unavyotaka hapo utakuwa unatengeneza mafanikio yako
mwenyewe.
Unachotakiwa
uelewe hapa, hutakiwi kuruka kitu. Fanya mambo kwa mpangilio kama yanavyotakiwa
kufanyika. Usijadanganye kwa kuahirisha au kuacha vitu bila sababu ya msingi,
ukifanya hivyo utakuwa unaishi nje ya mfumo na utashindwa tu.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia rafiki,
kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 28, 2017
Ijue Siri Ya Kuondokana Na Ukata.
Siku
ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na
kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha
hatari sana.
Kauli
hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika
kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika
ujumbe huo, labda ujumbe huo upimwe na
kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa.
Ujumbe
huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena
unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya
msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa.
Binafsi
nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo
huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho
tunachokiita ni woga.
Woga
ndio ambao umekua tatizo sugu lilojengeka machoni mwa watu wengi hata
kuwapelekea watu hao kuweza kufa maskini huku watu hao wana uwezo mkubwa wa kufanya
mambo makubwa yenye kuleta mapinduzi ya kufikia kilele cha mafanikio yao.
Woga
huu si mwingine ni ule woga wa kuthubutu kuweza kufanya mambo mbalimbali. Wapo
watu ambao wanatamani kufanya biashara kubwa ila wakiwatazama watu ambao
walifanya biashara hiyo na kuona ya kwamba walifeli basi nao hujikuta wanaogopa
kufanya jambo hilo.
Achilia
mbali biashara, wapo baadhi ya watu wanavipaji mbalimbali lakini watu hao
wamekuwa ni waoga wa kuonesha vipaji hivyo machoni mwa watu wengine huku
wakiamini ya kwamba watachekwa, watu wa aina hii mara nyingi hufa na ndoto zao.
Wapo
baaadhi ya watu wanaogopa kujenga nyumba zao za kuishi huku wakisema, “kwa
heshima niliyonayo nikijenga nyumba ya kawaida watu wengine wanatanishangaa”
kwa kauli kama hizi basi hujikuta miaka inazidi kukatika bila watu hao kuweza
kufanya kitu chochote cha maana.
Wapo
baadhi ya wanafanzi wamekuwa wanaogopa kusoma masomo ya sayansi huku wakiamini
masomo hayo ni magumu mwisho wa siku watu hao hujikuta wanafeli masomo hayo,
kwa mtazamo wa aina hii ndipo ninapokubaliana na kauli ile ambayo nimesema hapo
awali ya kwamba unachokiogopa ndicho kitakachokua.
Kabla
sijamaliza kusema nawe siku ya leo nitakuwa ni mchoyo wa fadhira kama
nitashindwa kutoa ufumbuzi wa tatizo hili, yawezekana ukawa na tatizo la aina
hii ya kuogopa kufanya jambo fulani la maendeleo eti kwa sababu ya woga uliojengeke
ndani mwako, unachotakiwa kukufanya ni kuhakakisha kila jambo ambalo unataka
kulifanya, kabla hujaanza kulifanya jambo hilo hakikisha ya kwamba jambo hilo
unalichunguza kwa makini na sio
kutanguliza woga mbele na ndiyo itakuwa siri ya kuondokana na ukata.
Mwisho
nimalize kusema ya kwamba “kile unachokigopa kukifanya leo ndicho
kitachokufanya uweze kuwa maskini”. Jambo lolote unalifanya hakikisha
ya kwamba linakuwa jambo chanya ambalo halitavunja sheria na taratibu za sehemu
ambayo unaishi.
Asante
sana kwa kusoma Makala haya nikutakie siku njema na mafanikio mema.
Ndimi Afisa Mipango; Benson Chonya
0757-909942
Nov 27, 2017
Maskini Na Tajiri Wanatofautiana Kwa Mambo Haya…
Kila
kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano
mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika
kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na
mingine midogo ya kawaida.
Pia hata
wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na
nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua.
Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge
wanyonge.
Halikadhalika
linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na
maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna
binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa
hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu.
Kama
mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe
na matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya
wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo mambo mengi kidogo yanayosababisha wengine wawe
matajiri na wengine kuwa maskini.
Lakini
katika makala haya tutaongelea kipengele kidogo cha tabia na jinsi zinavyoleta
utofauti kati ya maskini na tajiri. Ni kweli zipo tabia ambazo matajiri wanazo
na huwafanya wao kuwa matajiri kila kukicha. Ni tabia ambazo huwatenga kabisa
na maskini na kuwaacha matajiri waendelee kufanikiwa.
Ikiwa
utaamua kujifunza na kuzifatilia tabia hizi kwa karibu, uwe na uhakika utajiri
utakuwa mikononi mwako muda sio mrefu. Nasema hivyo nikiwa na maana hii,
ukitaka kuwa tajiri fanya yale ambayo matajiri wanafanya nawe utafanikiwa.
Hebu
kwa pamoja bila kupoteza muda, tuangazie nukta kadhaa, zinazoweza kutuonyesha
tabia zinazowatenga kati ya matajiri na
maskini.
1. Kuwekeza.
Watu
wenye sifa ya utajiri ndani mwao hata kama bado hawajafika huko kwenye utajiri
halisi ni wawekezaji wazuri sana. Si watu wa kuridhika na chanzo kimoja cha
mapato. Wana vitega uchumi vingi sana ambavyo vinawasaidia kuingiza mapato kwa
wingi hata kama wamelala.
Kwa
mfano uatakuta wamewekeza kwenye mashamba, mafuta, migodi na maeneo mengine
mengi. Hii ni sifa mojawapo kubwa inawatenga maskini na matajiri. Ukiona una
kitega uchumi kimoja ujue unajizibia nafasi mwenyewe ya kuelekea kwenye utajiri
mkubwa.
2. Kuweka akiba.
Suala
la kuweka akiba kwa watu matajiri sio suala la hiari, kwao ni lazima. Angalau
huweka asilimia kumi ya kile wanachokipata. Wanajua vizuri akiba hizo ni msaada
mkubwa kwa baadae katika suala zima la kuwekeza. Wao katika kuweka akiba ni
lazima, na pia hawana mchezo katika hilo.
Kutona
na tabia hii, huwafanya wazidi kufanikiwa kila siku na kuwaacha maskini
wakibaki kuwa maskini. Ni kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuelewa kwamba,
akiba ni jambo la msingi sana kujiwekea kama unataka kuwa tajiri. Vinginevyo
acha kuweka akiba, uendelee kubaki kwenye umaskini.
3. Kutoa.
Tabia
nyingine inayowatenga watu matajiri na maskini ni ile hali ya kutoa. Watu
matajiri ni watoaji wazuri sana wa pesa na mali zao. Hufanya hivi si kwa sababu
wanazo nyingi, bali kutoa ni moja ya kanuni kubwa ya mafanikio walioamua
kuitumia. Huwezi kufanikiwa sana kama hutoi.
Ieleweke
hivi, maskini wanaendelea kubaki kuwa
maskini kwa sababu ya uchoyo walionao. Hukumbatia sana walivyonavyo na
kusahau kutoa. Kosa hilo huwafanya wazidi kuendelea kuwa maskini siku zote za
maisha yao. Ili kuwa tajiri ni lazima kutoa.
Kumbuka,
tabia ya kuwekeza, kuweka akiba na kutoa ni moja ya tabia kubwa zinazo watenga
matajiri na maskini. Matajiri wanajikuta wakiwa ni watu wakuzifanyia kazi tabia
hizo na kuwafanya kuwa matajiri na maskini hubaki na umaskini wao kwa sababu ya
kutokuzifanyia kazi tabia hizo. Chukua hatua ya kutenda ili kubadili maisha
yako.
Ansante
kwa kunifatilia na pia endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
.
Nov 26, 2017
Hutakiwi Kukwepa Jambo Hili Kama Unataka Kufanikiwa Kwa Kishindo.
Vipo
vitu vingi katika safari yako ya mafanikio ambavyo hutakiwi kivikwepa hata
kidogo kama unataka kufika juu sana kwenye mafanikio. Ila kama unataka kufika
kwenye mafanikio ya kawaida tu, unaweza ukavikwepa tu hakuna hata shida.
Leo sitataka
kuzungumzia sana vitu vingi, naomba nikudokezee jambo moja tu ambalo unatakiwa kutolikwepa ila unatakiwa ujue
namna ya kukabiliana nalo ili uweze kufanikiwa kwa kishindo kikubwa.
Jambo
hili si lingine bali ni kubeba hali hatarishi au kukabiliana na hali yoyote
hatarishi ili kuweza kufanikiwa. Unaweza ukawa hujanielewa vizuri lakini
ninachomaanisha hapa ni kuchukua ‘risk’
ili uweze kufanikiwa. Mpaka hapo sina shaka tupo pamoja.
Ukumbuke
maisha yamejaa kila aina ya hali hatarishi. Huwezi kukwepa kukutana na hali
yoyote hatarishi katika maisha yako. Ukikwepa hali hii ni lazima utakutana na
hali nyingine hatarishi ambayo unatakiwa kupambana nayo mpaka kuweza kuishinda.
Kama
kila wakati unaogopa kujitoa mhanga kwa sababu ya kuogopa kujihatarisha, basi
tambua hapo ni sawa na kuchagua umeshindwa. Hutaweza kufika popote kama hauko
tayari kuchukua ‘risk’ yoyote inayokupeleka
kwenye ndoto yako.
Inatakiwa
ujitoe mhanga kweli, haijalishi unajitoa mhanga kwenye kitu gani, kwenye
malengo yako uliyojiwekea au kwenye kitu kingine chochote. Swala la kujitoa
mhanga nakukubali kupoteza baadhi ya vitu ili ufanikiwe unatakiwa kulijua kwa
ufasaha sana.
Maarifa
uliyonayo unayatakiwa kuyatumia ili kukabiliana na kila aina ya changamoto na
si kukimbia changamoto yoyote ile. Kukimbia changamoto na kuogopa kujihatarisha
hiyo inaweza ikawa ni sawa na ujinga kwako ambao utakunyima mafanikio.
Unaweza
ukajiuliza ni kitu gani ambacho utakipata hapa dunia pasipo wewe kuweza kujihatarisha.
Ukisema biashara ni lazima uweke muda na pesa zako ili upate kile unachokitaka.
Ukiangalia karibu kila kitu kwanza lazima uhatarishe ndio upate.
Kwa mfano
hata wewe, umezaliwa kwa kujihatarisha pia. Uhai ulionao vilevile wewe kama
wewe hauna uhakika nao, hiyo yote bado unaishi katika hali hatarishi. Hiyo kama
iko hivyo kwa nini usiamue ukubali kujihatarisha kwa chochote ili ufanikiwe.?
Mara
nyingi kuchukua ‘risk’ kwa kile
unachotaka kukifanya, mwisho wa siku huweza kukupa wewe unayechukua ‘risk’ hiyo zawadi kubwa ya mafanikio. Ukumbuke
tu mafanikio yote yanaanza kupatikana kwa wewe kuchukua ‘risk’ na sio kinyume chake.
Kwa hiyo
badala ya kukimbia hali hatarishi yoyote kwako, unatakiwa kujua namna ya kuweza
kukabilina nayo ili uweze kufanikiwa. Kama hautafanya hivyo utashindwa tu hata
ufanyaje, hutaweza kukwepa kushindwa.
Ukumbuke
kama nilivyokwambia mafanikio yanapatikana kwa wale watu ambao wanajitoa mhanga
sana yaani kwa watu wanaochukua ‘risk’ kama
wewe si miongoni mwao sahau kidogo kuhusu kufanikiwa, waache wachukua ‘risk’ wafanikiwe.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 24, 2017
Mambo Ambayo Unatakiwa Kuyakumbuka Kila Wakati.
U
hali gani mpenzi msomaji wa DIRA YA
MAFANIKIO naamini siku yako imekwenda poa na unaendelea kuweka juhudi za
kweli katika kubadilisha maisha yako. Kwa harakati hizo tu nakupa hongera na
endelea kupambana mpaka kieleweke.
Naomba
pia nitumie wasaha huu kuweza kukaribisha katika makala yetu ya leo ili tuweze
kujifunza juu ya mafanikio. Naamini unajua kujifunza hakuna mwisho, hivyo
unatakiwa kila siku kuweka maarifa ya kukusaidia, ukishindwa kufanya hivyo
utakwama.
Katika
makala yetu ya leo nitaomba tu nikukumbushe mambo ambayo unatakiwa uyakumbuke
kila wakati kwenye maisha yako . Ni
mambo ya msingi kwani yatakusaidia kuweza kuwa na mtazamo chanya na kubadili
mambo mengi sana kwako.
1. Mambo yaliyopita hayawezi
kubadilishwa tena.
Unatakiwa
kuelewa kama kuna mambo ambayo yameshapita huwezi kuyabadilisha tena hata kama
yalikuumiza au ulifanya makosa kiasi gani. Kwa sasa unatakiwa kuganga yajayo,
habari ya mambo yaliyopita yatumie kama fundisho tu kwako, lakini ndio
yameshapita, usiumize kichwa na kujilaumu sana.
2. Maoni ya watu hayaamui hatima ya
maisha yako.
Hata
siku moja usije ukakaa ukafikiri kwamba maoni ya watu wengine wanayosema juu ya
wewe ndiyo yanaamua maisha yako yawe vipi. Maisha yako yanabaki hivyo yalivyo
kwa sababu wewe umeamua yawe hivyo. Lakini usikubali hata siku moja maoni ya watu
yakurudishe nyuma na usiyatumie kama kisingizio.
3. Maisha yako yatakuwa mazuri tu
ukijipa muda.
Ukiamua
siku zote kubadilisha maisha yako unaweza. Kikubwa jipe muda wa kutosha
kubadilisha maisha yako hatua kwa hatua na kila kitu kitabadalika. Haijalishi
unaona maisha yako ni magumu kiasi gani, lakini muda ndio kila kitu. Muda
unaweza kusawazisha mambo mabaya na yakawa mazuri kabisa. Tumia muda wako vizuri.
4. Utashindwa tu, kama utakata tamaa.
Ndoto
yoyote ile uliyonayo au ambayo unatamani kuifikia una uwezo mkubwa wa kuifikia.
Ila hautaweza kuifikia ndoto yako hiyo ikiwa utafika mahali wewe mwenyewe
utaamua kukata tamaa. Moja ya sumu kubwa ya kimafanikio ni kukata tamaa, ukikata
tamaa ujue kila kitu kwako kimeishia hapo na hutaweza kusogea tena.
5. Furaha ya kweli inapatikana ndani
mwako.
Ukweli
huu hautakaa ubadilike kamwe kwamba furaha ya kweli inapatikana ndani mwako na
wala si nje yako. Unaweza ukakazana sana kutafuta furaha nje kwa kufanya vitu
ambavyo unaamini vitakupa furaha, lakini ukivipata vitu hivyo unashangaa ile
furaha tena bado huna. Hivyo jifunze kutafuta furaha ya kweli ndani mwako.
6. Mawazo chanya, ni njia ya mabadiliko
chanya pia.
Mbinu
mojawapo ya kuwa na maisha bora. Ni kwa wewe kuwa na mawazo chanya. Unapokuwa
na mawazo chanya ni rahisi sana kwa wewe kuweza kuleta mabadiliko chanya pia.
Watu wengi wanashindwa kwa sababu ya kuwa na mlundikano wa mawazo mengi ambayo
kwao ni hasi. Kuwa na mawazo chanya ubadili maisha yako.
Yapo
mambo mengi ya kukumbuka kila unapoelekea kwenye mafanikio yako. Kwa leo hii
nimekukumbusha mambo haya machache. Kwa kuyafanyia kazi itakuwa sehemu kubwa ya
mabadiliko kwenye maisha yako.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 23, 2017
Ukitaka Kufanikiwa Zaidi, Hakikisha Unashughulika Na Jambo Hili.
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima na unaendelea na pilikapilika
zako za kila siku. Hivyo nichukue wasaa huu nikukaribishe katika kujifunza kwa
pamoja, ambapo siku ya leo nataka tujifunze jambo ambalo inakupasa kushughulika
nalo kwanza ili uweze kufanikiwa.
Kabla
sijajikita katika kiini cha somo letu la leo, nataka tujiulize, hivi ili uweze
kufanikiwa katika maisha yatu inatupasa tushughulike na nini hasa? nini ambacho
huwa kinakuja katika kichwa chako hasa pale ukiambiwa kuhusu mafanikio?
Binafsi
niliwahi kufanya uchunguzi usio rasmi kuhusu mafanikio, nikagundua ya kwamba
fikra na mtazamo ya watu wengi juu ya neno mafanikio unaegemea zaidi katika
mitazamo hasi.
Wapo
baadhi ya watu wengi wao huamini ya kwamba, kufanikiwa ni bahati ya mtu
mwenyewe, lakini wapo baadhi ya watu wengine wao huamini ya kwamba mafanikio ni uchawi, huku
wakiamaini ya kwamba huwezi kufanikiwa bila kujihusisha na masuala ya
kishirikina. Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba mafanikio yana
mitazamo mingi sana katika vichwa vya watu.
Lakini
ukweli ni kwamba neno mafanikio ni Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, ambapo
Baraka hizo hujengeka katika kuamini ya kwamba mafanikio yako yanakuja kwa
kuaamini njia sahihi za kuleta mafanikio hayo na si vinginevyo.
Hivyo
ili uweze kuyapata mafanikio hayo inakupasa ushughulike na fikra. Fikra ndio
kitu cha kwanza ambacho unapaswa kushughulika nacho katika kuyasaka mafanikio
hayo. Tuposema neno fikra, tunamaanisha fikra chanya.
Au
kwa maneno mengine ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uweze
kushughulika na mtazamo wako juu ya maisha yako. Swali la kujiuliza ni kwamba
ni nini mtazamo wako juu ya mafanikio?
Endapo
majibu ya swali hilo ni mtazamo hasi, basi jifunze kila wakati kuwa na mtazamo
chanya, kwani endapo utajifunza kuwa na mtazamo chanya kutakufanya uweze kupiga
hatua za kimafanikio.
Mwisho
nimalize kwa kusema ya kwamba ukitaka kufanikiwa katika maisha yako hakikisha
unashulika na fikra, kwani fikra sahihi ndio kiwanda cha kutengeneza maisha
yako.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson chonya,
0757-909942
Nov 22, 2017
Hiki Ndicho Kitu Cha Muhimu Sana Kuzingatia Katika Mafanikio.
Upo ushauri
mwingi sana ambao umekuwa ukitolewa juu ya namna gani mtu afanye ili aweze
kufanikiwa. Waandishi na vitabu vingi vya mafanikio vimekuwa vikiandika sana na
kutoa ushauri wa kipi kifanyike ili mtu kuweza kufanikiwa.
Pamoja
na ushauri wote huo mzuri ambao umekuwa ukitolewa, lakini kipo kitu kimoja cha
muhimu sana ambacho mtu akiamua kukifatilia na kukifanyia kazi hicho ndicho
naweza kusema ndio mafanikio yote yaanzia hapo.
Kitu
hicho si kingine bali ni kujitoa/‘commitment.’ Mafanikio yote
yanaanza kwa wewe kuamua kujitoa na kuamua kweli kufikia mafanikio yako. Hakuna
unachoweza kukifanikisha usipojitoa kikamilifu.
Kuwa
na malengo, shauku ya kufikia malengo yako na hamasa hivyo kweli ni vitu
muhimu, lakini huwezi kufanikiwa hata kama una vitu hivyo ikiwa hautaweza
kujitoa. Kujitoa kwako ndio kila kitu katika kufikia mafanikio uyatakayo.
Ni kweli
ili kufanikiwa unahitaji kufanya kazi kwa juhudi, unahitaji kuwa na nidhamu,
unahitaji kuwa na shauku ya mafanikio yako, lakini lililo muhimu kwako ambalo
unatakiwa ulizingatie sana ni kwa wewe kujitoa kwako.
Angalia
maisha ya watu waliofanikiwa au angalia vile vitu ambavyo umewahi kuvifanikisha
katika maisha, sina shaka utapata jibu kwamba kwenye vitu hivyo ulijitoa sana
na ndio maana ukaweza kufanikiwa.
Kujitoa
kunakuja kwa wewe kuamua kufanya kila linalowezekana hadi kuweza kutimiza ndoto
zako. Hata kitokee kitu gani au kizuizi kipi kwa kuwa umeshaumua kujitoa
utaamua kwa chochote kile utafanya hadi uweze kufanikiwa.
Wataalamu
wote waliobobea katika fani mbalimbali duniani wametokana kwa sababu ya
kujitoa. Ugunduzi wowote duniani umetokeaa kwa sababu ya kujitoa. Kuna watu
walikuwa hawalali hadi wakawa wa wataalamu au wagunduzi wa kitu fulani.
Unapoona
mafanikio ya aina fulani yametokea pia hayo ni matokeo ya kujitoa. Kuna vitu
lazima vilipotea au vilitolewa sadaka ili mafanikio hayo yaonekane. Pasipo kujitoa
kwa nguvu zote ni rahisi tu kusikia mafanikio yakionekana kwa wengine lakini
sio kwako.
Kwa hiyo
huhitaji kukwepa kiujitoa unapotafuta mafanikio. Kama ni kazi unatakiwa kazi
ufanye haswa. Swala la kujionea huruma huko ni sawa na kuamua kuyapa mafanikio
mkono wa kwaheri kwamba hutaki tena.
Hata
kila mtu mwenye mafanikio ukimwona ujue kabisa kuna vitu ambavyo aliamua kujitoa
hadi akaweza kufanikiwa. Kwa namna yoyote ile kama unataka kufanikiwa angalia
unajitoa kwenye vitu gani.
Kujitioa
ni kitu pekee ambacho kitakuhakikishia mafanikio yako wakati wote. kwa sababu
utakapoanza kujitoa basi juhudi, kufanya kazi kwa moyo, kuwa na nidhamu hivyo
ni vitu ambavyo vitakuja vyenyewe kwenye safari yako ya mafanikio.
Kuanzia
leo, amua kujitoa kwa chochote kile unachokifanya kwenye maisha yako. hiyo
itakusaidia sana kuweza kufika katika kilele cha mafanikio makubwa uyatakayo
katika maisha yako kwa sehemu kubwa.
Kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji kuuziwa vifaranga bora na kwa bei
nafuu, waone DM POULTRY FARM PROJECT
kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 14. Wote mnakaribishwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 20, 2017
Mambo Ya Kukumbuka Sana Wakati Unatafuta Mafanikio.
Yapo
mambo ya msingi ambayo kila wakati unatakiwa uyakumbuke unapotafuta mafanikio
yako. Kwa nini unatakiwa kuyakumbuka mambo hayo, hiyo yote ni kwa sababu ndio
kama msingi na nguzo ya kufikia mafanikio yako.
Watu
wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutoyajua au kutoyakumbuka kabisa
mambo hayo na mwisho wa siku hujikuta wakipotea na kushindwa kufikia mafanikio yatakawayo
kimaisha.
Kupitia
makala haya nataka nikukumbushe mambo ya msingi sana ambayo unatakiwa kuyakumbuka
wakati unatafuta mafanikio. Naamini utajifunza na itakusaidia kuchukua hatua ya
kufanikiwa kwa kuyajua mambo haya tena.
1. Jipe muda wa kufanikiwa.
Mafanikio
ni kitu ambacho hakitokei mara moja tu. Mafanikio yanaenda hatua kwa hatua. Si kwa
sababu eti kuna jambo umepanga kulifanikisha basi ulifanikishe leo leo, kama ni
hivyo basi huo utakuwa ni uongo mkubwa sana.
Unatakiwa
ujipe muda wa kufikia mafanikio yako. Acha kuangalia njia za kutaka kujipatia
utajiri wa haraka. Unatakiwa kuweka juhudi kila siku. Hata Roma kumbuka
haikujengwa kwa siku moja na mafanikio pia yanataka mchakato vivyo hivyo.
Wakati
mwingine inaweza ikakuchukua miaka 5, 10, 17 na hata 20 ili kuweza kufikia
mafanikio makubwa uyatakayo. Usishangae huo ndio ukweli, ila kama wewe wa kutaka mafanikio makubwa na
ya haraka, jiandae mafanikio hayo yatakupoteza rafiki.
2. Fanya kile unachokiamini kitakupa
mafanikio.
Usifanye
hata siku moja kosa kwa kuamua kufanya kitu ambacho moyoni mwako unaona
hakikupi mafanikio. Fanya kile ambacho unaamini kinakupa mafanikio, hata kama
kitu hicho kinadharaulika sana kwa wengi.
Kwa kufanya
kile kitu ambacho unaamini kitakupa mafanikio, naamini utaweka juhudi sana hadi
kuweza kufikia mafanikio yako makubwa. Ila kama unataka kushindwa kabisa fanya
kitu ambacho unaamini hakikupi mafanikio, utajuta.
3. Fanya kile unachokipenda.
Hakuna
mafanikio makubwa utakayoweza kuyapata kwa wewe kufanya kile kitu
usichokipenda. Najua hili tumeliongelea sana hapa, lakini nakukumbusha ili
kufanikiwa unatakiwa kufanya jambo unalolipenda kwanza.
Ukiwaangalia
watu wote wenye mafanikio wanafanya vitu wanavyovipenda kwani huko ndiko mafanikio
makubwa yanapopatikana yaani inapotokea chanagamoto ni rahisi kuweza kupambana
nayo mpaka kieleweke.
4. Boresha kile ukifanyacho kila siku.
Haijalishi
kile unachokifanya ni bora kiasi gani, lakini maboresho kwa kile ukifanyacho ni
muhimu sana, kama hautaweza kuboresha kile unachokifanya itafika mahali
utakwama na hautaweza kusonga mbele sana.
Boresha
kuanzia leo biashara yako, uandishi wako, akili yako kwa kujisomea kila siku
ili uweze kusonga mbele. Kitu chochote ambacho hakina maboresho mafanikio yake
ni ya muda mfupi sana na itafika wakati mafanikio hayo hupotea.
5. Jifunze kutokana na makosa yako.
Kwenye
maisha hakuna kitu kinachoitwa ushindi wa moja kwa moja. Inabidi ifike mahali
ukubali kujifunza kutokana na makosa pale unaposhindwa. Ukijifunza tu kutokana
na makosa hiyo itakuwa ni fursa bora kwako ya kukusaidia kuweza kusonga mbele.
Naamini
kwa kujifunza mambo hayo kuna kitu ambacho umetoka nacho na kimekusaidia kuweza
kuchukua hatua ya kuweza kusonga mbele. Fanyia kazi hayo na ukumbuke kila
unapotafuta mafanikio yako.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 18, 2017
Ijue Msingi Ya Kuwa Mbunifu.
Katika
maisha yako yote ambayo unayaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu
basi utaendelea
kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba
asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati katika maisha yako ni lazima uwe mbunifu.
Ubunifu
ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa
hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni
kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo
tayakuwa ni ya kawaida tu.
Kwa sababu
katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu
ambacho unakifanya wewe kwa asilimia
kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa
mfanano wa vitu unazidi kuongezeka swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni,
hivi natajitofautishaje na wenzangu?
Majibu
ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha na wengine unachotakiwa kufanya ni
kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja
kifua mbele akaniuliza sasa afisa mipango huo ubunifu ni nini?
Pasipo
kuona haya endapo niutaulizwa swali kama hilo jibu ambalo nitampa nitamwambia,
ubunifu ni kuongeza thamani kwa kitu ambacho unakifanya, aidha kama utashindwa kuongeza thamani basi utakiwa
kuunda kitu kipya.
Katika
swala kuunda kitu kipya hapa ndipo pamekuwapo na tatizo fulani kwa sababu watu
wengi wanapenda sana ganda la ndizi kuteleza, kwa maneno mengine
tunaweza kusema akili zao zimeganda hasa katika suala la kufikiria wao wamekuwa
wanapenda sana kufanya ‘copy & paste.’ Kufanya hivyo ni kujipoteza
mwenyewe hivyo unachotakiwa kufanya ni kwamba lazima uwe na misingi ya kubuni
kitu cha kwako.
Pasipo
kupoteza kusudio la mada yangu ya siku ya leo, niliona ni vyema niianze na
utangulizi huo ili uelewe maana ya ubunifu. Mara baada ya kufahamua maana ya
ubunifu basi naomba japo kwa dakika chache tuangalie misingi ya ubunifu kama ifuatavyo.
1. Fanya kitu Unachokipenda.
Ukitaka
kuwa mbunifu katika eneo lolote lile , kwanza ni lazima uhakikishe unafanya
kitu ambacho unakipenda. Ukifanya kitu ambacho unakipenda kwa asilimia zote,
upo uhakika wa asilimia zote kwamba ni lazima utakuwa mbunifu ili kuwashinda
washindani wako wanakuzunguka.
2. Wekeza muda katika kuwaza na kutenda
jambo hilo.
Ili
uweze kuwa mbunifu katika jambo ambalo unalifanya jambo jingine ambalo
unatakiwa kulizingatia ni kwamba ipo haja kubwa sana ya kuwekeza muda mwingi
katika kuliwaza na kulitenda jambo hilo. Hivyo kwa kuwa umeamua kuyasaka
mafanikio kwa udi na uvumba huku ukiamini ya kwamba ubunifu ndiyo ambao
utakusaidia kuwa hivyo basi hakikisha ya kwamba unajipanga kikamilifu kuweza
kujitoka kwa kuwekeza muda wako mwingi ili kuweza kulitimiza jambo hilo.
3. Jifunze vitu vipya vinavyoendana na
jambo lako.
Jambo
jingine ambalo litakufanya wewe uweze kuwa mbunifu ni kwamba ni lazima uhakikishe
ya kwamba kila wakati huchoki kujifunza vitu vipya ambavyo vinaendana na jambo
hilo. Sambamba na hilo kwa kuwa binadamu kwa asilimia kubwa kuna uwezekano
mkubwa sana wa kile alichojifunza kuweza kusahau, hivyo kwa kile ambacho
unajifunza ni lazima uhakikishe ya kwamba unakiandika na uwe unakipitia mara
kwa mara ili usikishau.
4. Jiulize maswali mara kwa mara.
Jambo
la mwisho kati ya mengi yahusuyo somo hili ni kwamba kila wakati ni lazima uwe
ni mtu wa kujiuliza maswali ya mara kwa mara. Moja kati ya swali muhimu ambalo
unapaswa kujiuliza wewe katika misingi hii ya ubunifu ni, Je hivi nikifanya jambo
hili nitapata faida gani?
Mpaka
kufikia hapo sina la ziada nikutakie ubunifu mwema na siku njema.
Ndimi: Afisa Mipango ; Benson Chonya
0757-909942
Nov 17, 2017
Sababu Tano Kwanini Watu Wengi Hawafanyi Kazi Zao Kwa Ufanisi Mkubwa.
Si
kitu cha ajabu, mara nyingi kumekuwa na malalamiko mengi kwa ‘mabosi,’
kulalamikia watu walio chini yao kwamba wanafanya kazi chini ya viwango, lakini
si hivyo tu bali wanafanya pia kwa ufanisi mdogo sana, yaani hakuna ubora.
Ni
tatizo ambalo limekuwa likiongelewa sana na kuhusishwa na uvivu, kwamba vijana
wa siku hizi ni wavivu na hawataki kufanya kazi sana na tatizo hili limekua
likikua siku hadi siku katika maeneo mengi makazini.
Je,
kwa wewe binafsi, unafikiri chanzo cha tatizo hili ni nini? Kwa nini watu
wanakwenda kazini karibu kila siku, lakini utendaji na ufanisi wao ni kidogo
sana na hata hauridhishi kwa kiasi kikubwa kuweza kuleta mabadiliko.
Kiuhalisia
zipo sababu kadhaa, ambazo moja kwa moja zinakuwa zinapelekea utendaji wa kazi
kuweza kushuka sana kazini. Sitaki kukutajia sababu nyingi sana, katika somo
hili nakutajia sababu tatu tu, kwa nini watu wengi hawafanyi kazi zao kwa
ufanisi.
1. Mwingiliano wa mambo yasiyo ya msingi.
Ufanisi
wa kazi kuna wakati unapungua sana kutokana na kuingiliana kwa mambo yasiyo ya
msingi. Kwa mfano, utakuta mtu anafana kazi moja lakini wakati huo huo akili
yake ipo kwenye kitu kingine kama simu au Tv au kuongea na watu wakati wa kazi.
Ufanisi
katika kazi na kufanya kazi katika ubora hakuwezi kuja kwa namna hii. Ndio
maana unatakiwa kila aina ya mwingiliano uweze kuutoa ili ufanisi uweze
kuonekana kwa uwazi kabisa kwenye kila unachokifanya.
Sababu
hii peke yake, ni chanzo kikubwa sana cha watu wengi kutokufanya kazi kwa ufanisi
mkubwa. Matokeo ya hili ni kuendeleza kushindwa kwenye maisha. Kama unataka
kufanya kazi kwa ufanisi na kufanikiwa, punguza mwingiliano wa mambo yasiyo ya
msingi kwako.
2. Kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Pia kuna
wakati ufanisi katika kazi unakufa kwa sababu ya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Inapofika
kipindi wewe ni mtu mmoja halafu ukawa na kazi nyingi kwa wakati mmoja ni ngumu
sana kuweza kuleta ufanisi.
Kitu
cha muhimu kuzingatia hapa, ni kufanya kazi zako kwa utaratibu. Usijipe kazi nyingi
kwa wakati mmoja, huko kutakuwa ni kujichosha na utapoteza ufanisi sana na usishangae
hutaweza kupiga hatua kwa jambo hata moja.
Siri
kubwa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele, chagua jambo moja na kisha jambo hiilo
lifanye kwa uhakika sana. Nguvu na mawazo yako yote yaweke hapo mpaka jambo
lako lilete matokeo na ufanisi mkubwa sana.
3. Kukosa hamasa kutoka kwa
wanaowaongoza.
Kuna
wakati kama unafanya kazi kwenye kampuni yaani uko chini ya mtu, unaweza
ukakosa ufanisi kwa sababu ya kukosa hamasa kutoka kwa wanaokuongoza. Ni muhimu
sana kwa watu wanaokuongoza au viongiozi wakatoa hamasa kubwa.
Pengine
unajiuliza hamasa hii ni ipi? Ni muhimu na kwa viongozi pia nao kuweza kujitoa
kufanya kazi ili kuonyesha mfano. Kinyume cha hapo unaweza ukakatishwa tamaa
kwa kujiona kama hiyo kazi unayoifanya ni kazi yako tu peke yako.
Lakini
kwa kushirikiana pamoja kuanzia viongozi hadi wafanyakazi wa kawaida ingawa
kila mtu anakuwa anafanya kazi kwa sehemu yake hiyo itasaidia kukupa motisha na
mwisho wa siku kuleta ufanisi mkubwa katika kazi.
Kimsingi,
hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanapelekea moja kwa moja watu kuweza
kufanya kazi chini ya ufanisi mkubwa.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Nov 16, 2017
Maisha Yako Yanajengwa Sana Na Mambo Haya Matatu.
Yapo
mambo mengi ambayo yanajenga maisha yako au yanafanya maisha yako yawe kama
hivyo yalivyo. Lakini hata hivyo pamoja na mambo hayo mengi, yapo mambo matatu
ya msingi ambayo yanajenga maisha yako au ndio msingi wa maisha yako.
Kama
utapuuzia ama hautaweza kujali mambo hayo matatu tu, basi kufanikiwa kwako kutakuwa
ni kitu ambacho hakiwezekani. Mimi na wewe tunatengeneza mafanikio au kushindwa
kwetu kupitia mambo hayo.
Sina
shaka, una hamu ya kutaka kujua ni mambo gani ambayo yanapelekea maisha yako
kujengwa. Sasa kamata kalamu na karatasi, kisha twende pamoja kwenye darasa
kuweza kujifunza somo letu la leo.
Jambo la kwanza, mawazo yako.
Kila
kitu unachokitaka kinaanzia kwenye mawazo yako. Hakuna jambo ambalo lipo
duniani limeanzia nje ya mawazo. Mawazo yana mchango mkubwa katika kukupa chochote
ukitakacho kwenye maisha yako.
Ukishindwa
katika mawazo yako, na nje utashindwa pia. Ndio maana ili kufanikiwa unatakiwa
kila wakati uwe na mawazo chanya sana, mawazo yakujenga, mawazo ambayo
yatakutoa sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine.
Na
mawazo haya hayawezi kuja kwa bahati mabya tu, mawazo haya yanakuja kwa wewe
kujilisha vitu chanya karibu kila siku. Unatakiwa ujifunze vitu chanya, unatakiwa
uwe na marafiki chanya ambao watakusaidia kuwa na mawazo bora.
Kuendelea
kuwa na mawazo yale yale ambayo yamekuweka hapo ulipo, ni sawa na kuchagua
kupotea kwenye maisha yako. Kila siku hakikisha una mawazo bora yatakayoweza
kukusaidia wewe kufanikiwa na si kukuangusha.
Jambo la pili, vitendo vyako.
Mawazo
bora peke yake hata yawe mazuri vipi hayawezi kukusaidia kitu au hayawezi
kukufikisha mbali. Kitu kingine ambacho kinajenga maisha yako kwa sehemu kubwa
ni hatua unazozichukua kila siku.
Inatakiwa
ujiulize hatua unazochukua kila siku hata kama ni kidogo sana lakini katika
kuelekea ndoto zako ni zipi? Kama hakuna hatua unazochukua basi ujue sio
unajenga maisha yako bali ndio unayaharibu kabisa na kuwa maisha ya hovyo.
Hakuna
mafanikio ya kukaa tu, hakuna mafanikio ya kuyaongelea mdomoni, mafanikio yanajengwa
kwa kuchukua hatua. Ukiona hakuna hatua unazochukua usijidanganye kwamba
unatafuta na wewe mafanikio, maana wewe utakwama hata iweje.
Watu
wanaochukua hatua karibu kila siku, watu hao ndio wanaofanikiwa na kujenga
bahati kubwa katika maisha yao. Kwa hiyo unaona, vitendo ni kitu kimojawapo ambacho
kina mchango mkubwa sana pia katika kujenga maisha yako.
Jambo la tatu, maneno yako.
Pamoja
na kwamba una mawazo mawazo mazuri na una vitendo vizuri, lakini unatakiwa
kukumbuka maneno yako pia yanamchango mkubwa sana katika kujenga maisha yako na
yakaonekana kama hivyo yalivyo hapo.
Maisha
ya wengi yamejengwa au kuharibiwa kutokana na maneno yao waliojinenea siku za
nyuma. Ndio maana kabla hujaongea inabidi ujiulize unaongea kitu gani na je
kitu hicho kinamchango upi katika kuelekea ndoto zako.
Unaweza
ukawa mtabiri wa maisha yako, eidha kwa kwa kubomoa au kuyaumba. Maneno yako yanaumba
sana maisha yako kwa sehemu kubwa. Ukijinenea vibaya, uelewe kabisa ndivyo
maisha yako yataharibika kabisa.
Hivyo
ni muhimu kuwa na uchaguzi wa maneno bora ili ikusaidie kuweza kufanikia. Usiwe
mtabiri wa kuharibu maisha yako kila wakati. Jifunze kuwa mtabiri wa kuweza
kukusaidia kujenga maisha yako.
Kwa
kifupi, hayo ndiyo mambo makubwa matatu ambayo yanajenga maisha yako sana, ingawa
ukienda kinyume na hapo ndivyo unaharibu maisha yako kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)