google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 9, 2017

Kama Utajitoa Kikamilifu Kwenye Mambo Haya, Utafanikiwa.

No comments :
Ili kufikia ndoto zako, unalazimika sana kujitoa kwa kile unachokifanya ili uweze kufanikiwa. Kujitoa ndio inatakiwa liwe hitaji la kwanza na la lazima ambalo ukilitekeleza nina uhakika itakusaidia sana katika kuweza kutimiza ndoto zako.
Watu wengi sana, miongoni mwetu inaweza ikawa ni wewe, ni wasemaji wazuri sana hasa linapokuja swala la ndoto kwa kusema kwamba, nitahakikisha lazima ndoto zangu zinatimia kipindi hiki au mwaka huu, lakini kipindi hicho kikipita hakuna kitu kilichotekelezeka.
Kiuhalisia, kila mtu anaweza kusema na kuelezea ndoto yake vizuri sana kama watu hawa wanavyosema, lakini kitu cha kujiuliza je, hivi ndivyo kujitoa kunavyotakiwa kuwa yaani kujitoa kwa maneno ili kutimiza ndoto zako? Nadhani, utakubaliana na mimi kujitoa ni zaidi ya kusema.
Kwa nini nasema hivyo? Ipo hivi, unakumbuka nimekwambia kama kusema kila mtu anaweza kusema tena wengine sana tu. Lakini ndoto zako haziwezi kutimizwa kamwe kama kweli umeamua kujitoa kwenye ndoto zako kwa kuongea.
Wewe unachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kisha jitoe kwa vitendo, jitoe kwa kungang’ania,  jitoe kwa kwa kuweka juhudi na kufanya kila kitu kinachotakiwa kufanyika mpaka kuhakikisha ndoto zako zinaweza kutimia. Ukijotoa hivi huhitaji tena kuongea, matokeo yataongea yenyewe.

Huku ndiko kujitoa unakotakiwa kujitoa ili kuweza kutimiza ndoto na mipango yako. Kama lakini ukikazania tu eti kuongea nakwambia utaongea sana na utaongea mipango yako mizuri sana jinsi ya kuifanikisha lakini hutafika popote, utabaki hapo ulipo tu.
Na njia nzuri itakayokusaidia wewe uweze kujitoa kikamilifu hasa katika mambo niliyotaja hapo kwenye aya ya juu, ni kwa wewe kuamua kuwa na malengo yenye maana kwako. Unapokuwa na malengo yenye maana kwako, malengo ambayo umeamua kuyatimiza kwa dhati zote, utajitoa tu.
Hutaweza kukubali hata siku moja uangushe ndoto zako kwa kosa la kushindwa kujitoa. Ni lazima utajitoa katika vitendo, utajitoa kwa kung’ang’ania ama kuwa mbishi na pia utajitoa kufanya kila kitu mpaka unafanikiwe.
Unapoona mtu au hata wewe hujitoi kikamilifu kukamilisha jambo lako, angalia malengo uliyonayo, mara nyingi utakuta malengo uliyonayo hayako wazi sana, utakuta una malengo mengi au huna kabisa ilimradi upo tu.
Maisha yako uelewe yatazidi kuwa yakuanguka kila iitwapo leo, kama hutajitoa kikamilifu kama inavyojitakiwa kujitoa na ukaendelea kujitoa kwa mdomo. Hakuna aliyefanikiwa kwa kuongea tu peke yake. Mafanikio yanataka uwe mtu wa vitendo sana.
Ni wakati wa kujiuliza wewe mwenyewwe, unajitoa kwa namna gani ili kufikia ndoto zako? Kumbuka nimekwambia huhitaji kujitoa kwa maneno tu,kwa kujitoa kwa maneno hutaweza kufanikiwa, bali nimekwambia jitoe sana katika mambo haya;-
1. Jitoe kwa vitendo,
2. Jitoe Kwa kung’angania,
3. Jitoe kwa kuweka juhudi za kila aina.
Sina shaka mpaka hapo umenielewa, fanyia kazi haya mambo ya msingi kwako na endelea kuchukua hatua hadi kufikia mafanikio yako makubwa, KILA KITU KINAWEZEKANA UKIAMUA IWE HIVYO KWAKO.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.