Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Saturday, July 29, 2017

Tafuta Sheria Zinazokuongoza Kwenye Maisha Yako.

No comments :

Kwa kawaida kila sehemu unayokwenda zipo sheria za kufuata. Zipo sheria za kuendesha gari, zipo sheria za kufanya biashara, zipo sheria za kuingia ‘club’,  zipo sheria za mchezo wa mpira miguu. Inawezekana unajiuliza kwa nini sheria hizi zipo? Jibu ni rahisi tu, zimewekwa ili kuleta ufanisi na mafanikio katika maeneo hayo.
Kunapokuwa na sheria zinazoongoza jambo lolote, zinafanya kwanza kunakuwa na nidhamu kubwa ya ufanyaji wa jambo hilo na mwisho wa siku huleta mafanikio. Kwa mfano, kama kungekuwa hakuna sheria ya mpira wa miguu, mchezo huo usingefanikiwa na badala yake kungekuwa na fujo tu uwanjani.
Kama kila kitu chenye mafanikio kinaongozwa na sheria, hata maisha yako yanatakiwa kuwa na sheria ambazo utazifuata kila iitwapo leo ili uweze kufanikiwa. Kama hautakuwa na sheria zinazoongoza maisha yako itakuwa ni ndoto kufanikiwa. Utakutana na changamoto nyingi bila sababu kwa sababu huna sheria zako.
Labda nikuulize kitu, je, una sheria zinazoongoza maisha yako? Kama huna tafuta sheria za kuongoza maisha yako. Unapokuwa na sheria zako, zinakufanya kutawala maisha yako na si kuishi ishi tu bila mwelekeo. Ishi kwa sheria  zako, hiyo itakufanya kila wakati utakuwa mshindi, tofauti na ambavyo kama huna. 

No comments :

Post a Comment