google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Sep 13, 2016

Mambo Matatu Madogo Yanayoua Ubunifu Wako.

No comments :
Kati ya kitu ambacho unalazimika kukijua vizuri, ili kikusaidie kuongeza thamani kubwa ya maisha yako ni ubunifu. Hiyo ikiwa na maana, katika kila eneo la maisha yako ambalo lina ubunifu mara nyingi mafanikio ni ya wazi.
Hebu jaribu kuangalia ubunifu unaofanywa na kampuni mbalimbali. Ukipita mtaani ukawa na jicho la kichunguzi, utagundua vipo vitu vingi sana vinavyobuniwa kila kukicha.
Je, ulishawahi kujiuliza hata mara moja, kwa nini kampuni kubwa nyingi zimeng’ang’ana na ubunifu sana? kama bado hujawahi kujiuliza, je unafikiri wanapoteza muda wao kwa kubuni huko?
Kwa kile ambacho wengi hawajui, ipo siri kubwa sana ya mafanikio iliyofichika kwenye ubunifu. Ndio maana, kwenye kila kitu unachofanya ili kukuletee mafanikio umekuwa ukisisitiziwa lazima uwe mbunifu kwanza.
Lakini pamoja na umuhimu mkubwa wa ubunifu katika suala zima la kutupa mafanikio, bado wengi si wabunifu. Na kwa sababu hiyo maisha yao huendelea kuwa duni kadri siku zinavyokwenda.
Hebu leo hii kwa kusoma makala haya naomba tuangalie mambo machache ambayo huua ubunifu. Kwa kujifunza mambo hayo itakusaidia sana kuchukua hatua na hatimaye kuweza kusonga mbele.
1. Kushindwa kupata usingizi wa kutosha.
Kitaalamu, binadamu wa kawaida anatakiwa kupata usingizi kwa wastani wa saa saba hadi nane kwa siku. Inapofika mahali ukakosa kulala kwa muda huo, huwa yapo matatizo ambayo yanaweza kujitokeza kama ya kiafya na kukosa ubunifu.
Mara nyingi unapokosa usingizi wa kutosha na kwa muda mrefu, polepole unaua ubunifu wako bila kujijua. Hili ndilo linalotokea kwa wengi, hasa wale ambao kwao usingizi hawapati wa kutosha.

Kutokuwa tayari kujifunza, ni chanzo cha kuua ndoto zako.
Kikawaida sio rahisi kufikiria vitu vya maana kama kichwa chako kimejaa usingizi, zaidi utakuwa unawaza kulala. Hivyo, kama unataka kuongeza ubunifu wako jitahidi sana kupata usingizi wa kutosha.
Ndio maana, ukilala vizuri na kupata usingizi wa kutosha akili yako inakuwa ina nguvu sana ya kubuni mambo na inakuwa inafikiria kwa ufasaha. Jambo la kuzingatia hapa, hakikisha unapata usingizi wa kutosha ili usiue ubunifu wako.
2. Kutokuwa tayari kujifunza.
Watu wengi wanafanya vile wanavyofanya lakini hawako tayari kujifunza kwa undani mambo hayo wanayoyafanya. Kwa mfano, utakuta mtu ni mfanya biashara, lakini hayuko tayari kujua kwa undani sana biashara anayoifanya.
Sasa katika hali ya kawaida inakuwa ni ngumu sana kuweza kuwa mbunifu, kama hata jambo unalolifanya hauko tayari kujifunza changamoto zake na uzuri wake kwa undani. Na kwa sababu hii, wengi hujikuta wakiua ubunifu wao na ndoto kwa pamoja.
3. Kutokuwa karibu na watu wabunifu.
Pia jambo lingine ambalo linaonekana ni la kawaida, lakini linaua ubunifu wengi ni kule kukaa mbali na watu wabunifu. Ili uwe mbunifu mzuri ni lazima ujifunze na kuwa karibu na wabunifu wenzako.
Haiwezekani lengo lako ni kukuza ubunifu, halafu ukaendelea kukaa na watu wa kawaida ambao hawana maono hayo. Kwa wale wote ambao wako mbali na wabunifu wengine, ni wazi ubunifu wao hupotea siku hadi siku.
Kwa kumalizia makala haya, ni vyema ukatambua hayo ndiyo mambo yanayochangia kuua ubunifu wako kwa sehemu kubwa. Chukua hatua kubadili mambo haya na endelelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.