Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Thursday, July 21, 2016

Kitu Unachotakiwa Kuanza Nacho Ili Kujitengenezea Utajiri.

No comments :
Watu Wengi wanatafuta utajiri kwa udi na uvumba, japo wengine wachache wanapata na walio wengi wanakosa na kukata tamaa. Jambo ambalo ni dhahiri kabisa ni kwamba, watu wengi tunaanza safari ya kutafuta utajiri kwa kutumia vituo tofauti fofauti na mbavyo vingi havitufikishi kwenye huo utajiri. Kwahiyo, kitu cha kujiuliza je? Safari Yetu ya kutafuta utajiri inapaswa kuanzia wapi?

Katika utafiti na uzoefu wangu nimegundua kwamba, UTAJIRI unaanzia kwenye Fikra.Na "Fikra ni Nguvu Pekee inayoweza kuzalisha utajiri wa kuonekana kutoka kwenye vitu visivyoonekana. Fikra, hichi ndicho kitu unachotakiwa kuanza nacho ili kujitengenezea utajiri.  


Kila Kitu unachokifanya sasa hivi kimeanza kama wazo kutoka ndani yako. Hakuna matendo utakayotenda bila kuanzia kwenye fikra (Mawazo). Kwahiyo, ukiwaza kwa namna fulani, basi ujue kwamba utapata utajiri wa namna fulani sawa na ulivyowaza mwanzoni kabla ya kupata utajiri huo. 

Fikra au mawazo, ndio kitu pekee ambacho huweza kukusukuma kufanya vitu fulani fulani ambavyo ndivyo huweza kukuletea utajiri. Utajiri sio dhambi, bali ni sehemu ya Maisha, tumeletwa hapa duniani kuweza kutawala vilivyopo na kama ukiweza kuvitawala vizuri ni lazima utakuwa tajiri.


Unachohitaji ni kuweza kugeuza ndoto yako kuwa kweli. Wakati ukifanya yote hayo, kumbuka Kuwa, wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana isiyokuwa na mwisho. Hata kama wewe unajiona sio mtu mbunifu, hata kama ulishashindwa huko nyuma, hata kama unafikiri umeshajaribu kila Kitu ila ukashindwa, jua kwamba bado una nafasi Kubwa ya kupata Chochote unachotaka. 

Huwezi kuishi maisha unayoyataka, huwezi kuishi maisha yenye uhuru kama huna utajiri. Huwezi kuinuka na kufikia juu kwenye chochote unachofanya kama Kweli huna uhuru wa kipato. Ndio Maana ni muhimu sana Kwako Kuwa tajiri.

Kwa Kawaida binadamu tunazo nia tatu ambazo nazo tunaishi, yaani mwili, akili Na roho. Njia hizi ndizo utengeneza maeneo muhimu ambayo utuongoza Kuishi ama maisha ya utajiri au maisha ya umaskini. Maeneo hayo yote matatu ni muhimu sana katika kuishi maisha yenye mafanikio na furaha. Ni Lazima mwili Uwe na utajiri, akili iwe ya utajiri Na Roho pia iwe na utajiri, hapo ndipo itawezekana wewe kuifikia ndoto yako ya utajiri. 

Lengo la maisha yetu ni maendeleo yaletwayo na utajiri na wala si Kitu kingine. Msingi mkuu wa maisha ni kuendelea kupiga Hatua za kusonga mbele.  

Kama kila Kitu kwenye maisha kinakazana kuwa zaidi ya kilivyo sasa, iweje wewe leo uendelee kuwa hivyo miaka na miaka yote?
 Mti unakazana kukua zaidi ya ulivyo sasa.  

Na Wewe Binadamu pia ni Lazima ukazane kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa kwa maeneo yote muhimu ya maisha yako. Katika harakati zako za kutafuta utajiri, Lazima kuhakikisha Kuwa fikra zako zinakuwa safi muda wote. Unatakiwa kutumia nguvu ya utashi wako kuzuia akili yako isilishwe mambo ya Umasikini, na ifanye akili yako ibaki imeshikiria imani na kusudi la maono ya kile unachotaka kufanya au kuumba. 

Kamwe usizungumze: Jitahidi usizungumzie kuhusu matatizo yako ya ya zamani kifedha kama Ulikuwa nayo; usiyafikirie kabisa. Usizungumze kuhusu umaskini wa wazazi wako au ugumu wa maisha yako ya huko nyuma. Kufanya lolote Kati ya hayo ni kujiweka katika umaskini kwa wakati Huu ulionao sasa.

Weka umakini na mambo yote yanayohusiana nao kado au nyuma yako kabisa. Linda mazungumzo yako: Kamwe usizungumze kuhusu masuala yako au chochote kile kwa namna ya kuvunja moyo au kukatisha tamaa. Kamwe usikubali uwezekano wa kushindwa au kuzungumza kwa namna inayoashiria kushindwa. 

Unatakiwa kutozungumza Kuhusu nyakati kuwa ngumu au mazingira ya Baza Kama Vile una mashaka. Nyakati zinaonekana kuwa ngumu kwa wale walio na usawa wakushindana na wenzao. Lakini, wewe unayetafuta utajiri wako hunabudi kuanza kujifunza maisha yale ambayo unashindana na malengo yako au ndoto zako basi. 

Kumbuka siku zote Mafanikio ni mchakato siyo tukio . Kwahiyo, Kama Wewe umeweza kujifunza Kitu Chochote kipya na cha Thamani kutoka kwenye makala hii ni Wazi kwamba Tayari umeanza mchakato wa kuelekea mafanikio.

Makala hii imeandikwa na Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP.  

No comments :

Post a Comment