google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 2, 2017

Jinsi Ya Kuelewa Kwa Nini Unashindwa Kufanikiwa Kwenye Maisha Yako.

No comments :
Kushindwa katika maisha au kushindwa katika jambo la aina fulani unalolifanya katika maisha yako, ni kitu ambacho kinatokea karibu kwa kila mtu. Hakuna mtu ambae ana uwezo wa kusema kwamba hajawahi kushindwa. Mtu huyu hayupo.
Lakini hata hivyo, kushindwa huko tunakokuzungumzia kupo kwa aina mbili. Kuna kushindwa kwa mambo machache na kuna kule kushindwa kwenye mambo mengi sana kwenye maisha yako, kiasi kwamba unajiona kama hujafanikiwa kabisa.
Leo kupitia makala haya nataka tuzungumzie aina hii ya pili ya kushindwa yaani kushindwa kabisa kuona mafanikio katika maisha yako kwa ujumla. Nimesema tunazungumzia aina hii ya pili ya kushindwa kwa sababu hapa ndipo kuna tatizo kubwa kwa wengi.

Kila mtu, ikiwemo na wewe ni shahidi kuwa maisha ya watu wengi ni ya kushindwa sana. Ukiangalia wale wanaokuzunguka au wewe mwenyewe, huhitaji kutafuta ushuhuda mkubwa sana kuthibitishsa hili kwani linaonekana kwa wazi.
Sijui sana, kama umeshawahi kujiuliza kwa nini watu wengi wanashindwa, kwa nini maisha ya watu wengi yamekuwa magumu kwa idadi kubwa, ukilinganisha na wachache ambao wameonekana wakifaidi matunda ya hii dunia.
Inawezekana zipo sababu ambazo zimejificha ambazo wewe hujui na kwa hiyo hata maisha ya watu wengi unapoona magumu au hata ya kwako pia, umekuwa ukichukulia ‘poa’ tu kwamba ndio utaratibu wa maisha jinsi yalivyo.
Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu na tumekuwa wote kwa muda mrefu ukinifatilia kwa namna moja au nyingine, leo nataka nikupe siri ya kwanini unashindwa kufanikiwa kwenye maisha yako kufikia vile viwango unavyotaka?
Najua kuna maisha fulani hivi umekuwa ukiyatamani au ukiyawazia kweli, kwamba, ‘laaa, nikiwa na maisha haya au nikipata maisha haya basi nitakuwa naona dunia ni mahala salama,’ sasa kutokana na kushindwa huko unaiona dunia hovyo.
Kwa kawaida na kitaalamu iko hivi, unashindwa sana kwenye maisha kwa sababu ya kuendelea kutoa visingizio visivyo na vikomo kwenye maisha yako. Kama unataka kujua kwa nini unashindwa kwenye maisha yako angalia kwanza VISINGIZIO VYAKO.
Umekuwa ni mtu wa visingizio vingi sana kwamba hufanikiwi kwa sababu hii au ile. Visingizio vimekuwa ni sumu kubwa sana ya mafanikio kwa wengi. Kama leo unahitaji kufanikiwa unatakiwa kuukata mzizi huu wa visingio mara moja na kuutupa mbali.
Usiendelee kutoa visingizio vyovyote vya wewe kushindwa kufanya jambo fulani. Visingizio vyako havina nia nzuri ya kufanya maisha yako yawe bora. Utakuwa ni mtu wa kuanguka sana kama ukiendekeza visingizio vyako visivyo na msingi.
Washindi katika maisha ni watu ambao hawatoi visingizio kabisa, ni watu ambao wanajua kujipanga na kuchukua hatua. Watu hawa wenye mafanikio wamegundua kwamba visingizio havina msaada kabisa kwenye kufanikiwa zaidi ya kukurudisha nyuma.
Ndio maana kama unaona ni utani, zunguka dunia nzima mtafute mtu ambae ana visingizio vingi sana halafu amefanikiwa. Mtu wa namna hii hutaweza kumpata hata ufanyaje, hayupo kabisa.
Kwa hiyo unaona kabisa ili, kuelewa kwa nini unashindwa kwenye maisha yako, huhitaji kutafuta mtabiri wala mpiga ramli, angalia ni visingizio gani unavyotoa. Utagundua hapo ndipo anguko lako la kushindwa kufikia mafanikio makubwa linapoanzia.
Kumbuka, kama hutaki kuendelea kushindwa, weka visingizo pembeni. Hakuna maelezo mazuri ambayo utayatoa eti kwa nini hujafanikiwa. Nimesema hakuna visingizio. Uamuzi wa kufanikiwa uko kwako kwa kuamua kuweka visingizio mbali kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.