google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 6, 2017

Tafuta Kwanza Kufanikisha Jambo Hili, Litakupa Mafanikio Sana.

No comments :
Lipo jambo moja tu ambalo kila mtu anayetafuta mafanikio anatakiwa alijue na kuweza kulifanyia kazi ili kuweza kutengeneza mafanikio makubwa. Kushindwa kulijua vizuri jambo hili, sio rahisi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Watu wengi wanajikuta ni watu ambao wanaishi maisha ya kati, maisha ya kubahatisha kwa sababu ya kutokulijua vyema jambo hili na matokeo yake kuleta hasara kwa maisha yao, kwa sababu tu ya kushindwa kulijua.
Jambo ambalo unatakiwa ulijue ili uweze kufanikiwa iwe kwenye biashara au kwa chochote kile unachokifanya, ni lazima ujue namna ya kutoa huduma bora. Pasipo kujiweka upande wa kutoa huduma bora uwe na uhakika utakwama.

Bila kujali unauza nini, toa huduma bora ya uhakika utafanikiwa.
Ukiwaangalia viongozi wakubwa duniani wanafanikiwa sana kwa sababu ya kujiwekea mazingira ya kuwa watumwa wa watu, yaani wamekuwa ni viongozi wanaojali watu na kuwahudumia, mwisho wa siku nao hufanikiwa.
Pia hata wafanya biashara walio wakubwa zaidi duniani, wanafanya biashara zao kwa kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi ambayo haipatikani mahala popote. Kwa kutoa huduma hiyo, mafanikio humiminika tu kwao.
Kutafuta mafanikio makubwa, hakuna njia ya mkato zaidi ya kukubali kwanza wewe kuwa sehemu ya watu wanaotoa huduma bora zaidi. Achana na habari ya kupata pesa, kama ni pesa zitakuja zenyewe kwa kufuata huduma yako bora.
Kosa linalofanywa na wengi ni kuamua kufanya biashara, lakini wakati huo huo wanakuwa ni watu ambao hawazingatii huduma bora. Kama unafanya biashara kwa namna hii, nikwambie tu utafanya kweli, lakini hutafika mbali sana.
Unatakiwa ufike mahali uachane na fikra za kikale, unatakiwa kutengeneza wateja wengi zaidi ambao hao wateja hao watakusaidia wewe kuweza kufanikiwa. Lakini hata hivyo jambo hilo halitakuja kwa bahati mbaya zaidi ya wewe kutoa huduma bora.
Thamani unayotoa kulingana na huduma yako, hiyo ndiyo itakayokupa mafanikio yako. Haijalishi utakuwa unafanya biashara gani au kitu gani, lakini kikubwa kwako tafuta ile thamani kubwa inayostahili hapo utafanikiwa.
Kila wakati ukitafuta kwanza kufanikisha juu ya kutoa huduma bora, bila kujali mtaji wako ni mdogo, mtaji huo utakuwa mkubwa. Kwa chochote unachokifanya hata kama unaona hakifanikiwi kwa sasa, itafika wakati utaona mafanikio ya wazi kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.