Nov 23, 2017
Ukitaka Kufanikiwa Zaidi, Hakikisha Unashughulika Na Jambo Hili.
Habari
za muda huu mpenzi msomaji wetu wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka u mzima na unaendelea na pilikapilika
zako za kila siku. Hivyo nichukue wasaa huu nikukaribishe katika kujifunza kwa
pamoja, ambapo siku ya leo nataka tujifunze jambo ambalo inakupasa kushughulika
nalo kwanza ili uweze kufanikiwa.
Kabla
sijajikita katika kiini cha somo letu la leo, nataka tujiulize, hivi ili uweze
kufanikiwa katika maisha yatu inatupasa tushughulike na nini hasa? nini ambacho
huwa kinakuja katika kichwa chako hasa pale ukiambiwa kuhusu mafanikio?
Binafsi
niliwahi kufanya uchunguzi usio rasmi kuhusu mafanikio, nikagundua ya kwamba
fikra na mtazamo ya watu wengi juu ya neno mafanikio unaegemea zaidi katika
mitazamo hasi.
Wapo
baadhi ya watu wengi wao huamini ya kwamba, kufanikiwa ni bahati ya mtu
mwenyewe, lakini wapo baadhi ya watu wengine wao huamini ya kwamba mafanikio ni uchawi, huku
wakiamaini ya kwamba huwezi kufanikiwa bila kujihusisha na masuala ya
kishirikina. Kwa maneno mengine tunaweza tukasema ya kwamba mafanikio yana
mitazamo mingi sana katika vichwa vya watu.
Lakini
ukweli ni kwamba neno mafanikio ni Baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu, ambapo
Baraka hizo hujengeka katika kuamini ya kwamba mafanikio yako yanakuja kwa
kuaamini njia sahihi za kuleta mafanikio hayo na si vinginevyo.
Hivyo
ili uweze kuyapata mafanikio hayo inakupasa ushughulike na fikra. Fikra ndio
kitu cha kwanza ambacho unapaswa kushughulika nacho katika kuyasaka mafanikio
hayo. Tuposema neno fikra, tunamaanisha fikra chanya.
Au
kwa maneno mengine ili uweze kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uweze
kushughulika na mtazamo wako juu ya maisha yako. Swali la kujiuliza ni kwamba
ni nini mtazamo wako juu ya mafanikio?
Endapo
majibu ya swali hilo ni mtazamo hasi, basi jifunze kila wakati kuwa na mtazamo
chanya, kwani endapo utajifunza kuwa na mtazamo chanya kutakufanya uweze kupiga
hatua za kimafanikio.
Mwisho
nimalize kwa kusema ya kwamba ukitaka kufanikiwa katika maisha yako hakikisha
unashulika na fikra, kwani fikra sahihi ndio kiwanda cha kutengeneza maisha
yako.
Ndimi; Afisa Mipango: Benson chonya,
0757-909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.