google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Feb 13, 2018

Hata Kama Unapitia Kwenye Mambo Haya, Nafasi Ya Kufanikiwa Bado Unayo.

No comments :

Hata kama unaona siku nyingi sana zinapita na kuona maisha yako kama yanarudi kila siku nyuma na wewe unafikiri ndio basi tena huwezi kufanikiwa, hiyo unatakiwa kutambua haiko hivyo, unayo nafasi nyingine ya kubadilisha maisha yako na kuweza kusonga mbele ukiamua.
Hata kama tena itaonekana kila rasilimali uliyokuwa nayo imepotea na wewe unaona giza limekufika na unafikia mahali unaona ndio basi tena haiwezekani kufanikiwa kwako, lakini bado tena nakwambia nafasi ya kufanikiwa kwako ipo.
Usijaribu kukata tamaa kabisa kwenye maisha yako, hata kama hali ulionayo inaonekana ni mbaya sana na haiwezekani tena kufanikiwa kwako, yale matumaini ya kukuwezesha wewe kufanikiwa yapo na yanakuja mbele yako.


Huna haja ya kulia sana au kujutia kila aina ya hali kwamba imenikwamisha. Kama ilivyo kuna giza hata liwe giza vipi kwamba ni lazima nuru itatokezea na hata wewe ni vivyo hivyo, ule uwezekano wa mafanikio yako utaanza kuonekana.
Kupitia ugumu wa maisha unaopitia,  unatakiwa kujifunza kuwajibika zaidi na kujifunza pia kupitia hayo magumu. Hapo inawezekana upo kwenye funzo la ukomavu zaidi wa maisha yako, hicho unapaswa kukijua pia.
Unapaswa kujua hata kutokee ugumu vipi wa maisha yako, lakini kama wewe umeamua kwamba utafanikiwa, hilo sina wasiwasi litatokea kwako. Hakuna kitakachokuzuia ikiwa ndani yako umeamua kufanikiwa.
Najua ni rahisi utateseka sana kwa hili ama lile katika haraka za kufikia mafanikio yako, lakini utafika mwisho ni lazima uweze kufanikiwa. Usikubali uwe mshindwaji kwenye maisha yako hata kitokee kitu gani.
Hata kama utapitia magumu haya, amua lakini kufanikiwa kwako ni lazima. Pawepo na mtu au kitu kitakachokufanya wewe ujihisi kwamba huwezi kufanikiwa. Mafanikio yanajengwa kwa wewe kuweza kujiamini na kuamua kusonga mbele.
Washindi katika mafanikio hawazuiliwi na hali yoyote ile inayotokea mbele yao. Ni kweli wana kutana na magumu, lakini huamua kukabiliana nayo sana kwa nguvu zote hata kuweza kufikia mafanikio ya mkubwa.
Na wewe unaweza ukawa mmoja wao, amua kufanikiwa leo pasipo kujali mazingira ni ya aina gani yanakuzunguka. Na ukifanya hivyo ni kweli utakuwa mshindi, kama tu hutajali unapitia kwenye kitu gani.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.