Feb 10, 2018
Huhitaji Kusahau Kwamba Wewe Ni Binadamu.
Kwenye
maisha yako, kuna wakati unakumbana na kukatishwa tamaa, msongo wa mawazo na
maumivu makubwa sana, ni rahisi sana kufikiri kwamba huna thamani na dunia
ndiyo kama imekugeuka na huna bahati nayo kabisa.
Lakini
kwa upande mwingine unaweza ukawa unasahau, hayo yote yanayokutokea ni kweli yanakutokea
wewe, na kwa sababu wewe ni binadamu. Hayo hayawezi kulipata jiwe au mti ni wewe
na mwingine yanampata kwa wakati wake.
Hakuna
njia au namna ya kukimbia. Kama ni maumivu yakabili vivyo hivyo utafika wakati
yataisha, kama ni kukatishwa tamaa vumilia, nako pia kutakwisha, hali zote hizo
unatakiwa kupambana nazo mpaka uzivuke.
Unatakiwa
ujue wewe ni binadamu na yapo mambo mengi ambayo utakutana nayo na ambayo yanakupasa
kiuhalisia uwe mvumilivu kukabilina nayo. Kuna wakati kutokana na makosa ya
kibinadamu utaumizwa na pia kuumiza wengine pasipo kujua au kwa kujua.
Kuwa
binadamu maanake hujakamilika, kwa nini ububujikwe na machozi muda wote na kila
wakati kwa sababu ya kuumizwa na watu wengine au kwa sababu ya makosa fulani
fulani. Kumbuka wewe ni binadamu hayo yote kukutana nayo inawezekana.
Kwa hiyo
unapokuwa unaona kwamba umepoteza thamani yako na ubinadamu wako pia, kwa
sababu tu ya yale unayokutana nayo, hapo kumbuka unakosea kwa kiasi kikubwa. Thamani
yako haiwezi kushuka ipo pale pale.
Unahitaji
kuyafuta mawazo hayo mara moja, kama ulikuwa nayo ya kujiona wewe si kitu,
kumbe una thamani kubwa sana ndani yako ambayo haina mfano. Ndani yako wewe,
utaendelea kubaki yule yule wewe wa thamani kubwa, pasipo kujali nini
kinakutokea.
Inapofika
mahali unajiona wewe si mzuri sana kwa yale unayoyafanya, unatakiwa
kujikumbusha wewe ni binadamu unaweza kubadilika.
Inapofika
mahali ukashindwa, tena ukajaribu ukashindwa, jikumbushe wewe ni binadamu,
uwezo wa kushinda unaoa tena na hapo sio mwisho wako.
Inapofika
mahali unaona huoni tumaini tena kwenye maisha yako, kumbuka wewe ni binadamu,
tumaini jipya unaweza kuliona tena.
Wewe
ni wa thamani sana na unaweza kufanya makubwa yoyote, kwa sababu wewe ni binadamu
na fursa hiyo unayo. Unaweza ukatumia akili yako na ikakuletea chochote kile
unachokitaka kwenye maisha yako.
Wapi
unapokwama, kipi kinachokuliza, hicho kitu kisiwe sababu yoyote kwako ya
kushindwa, unaweza kubadilisha giza likawa nuru mara moja. Ni wangapi walikuwa
kwenye hali duni na sasa hivi maisha yao ni mazuri sana, nawe unaweza.
Ule uwezo
ulionao ndani mwako ni mkubwa vya kutosha kama utaamua kuutumia na kuweza
kufikia ndoto zako. Huna haja ya kujitilia shaka kwamba hivi kweli mimi
nitaweza, ndio unaweza, chukua hatua utaona matokeo yake.
Kama
kuna watu wanakusema kwa sabau ya wewe kushindwa, acha waendelea kusema wao ni
binadamu na wewe ni binadamu pia, chochote kinaweza kutokea kwenye maisha
wasamehe bure, badili maisha yako na kuwa mwingine kabisa.
Kama
hujui ni kivipi utabadilisha uwezo wako ulionao ndani mwako na kuweza
kukubadilishia maisha yako, endelea kujifunza wakati unafika utajua. Wewe ni
binadamu jifunze na utabadilika tu bila pingamizi lolote.
Tunajua
mawe, udongo, milima ni vitu ambavyo havibadiliki, lakini wewe ni binadamu,
usikalili maisha yako yawe hivyo hivyo milele , utakuwa unajizulumu sana. Maisha
yako yana haki ya kupiga hatua, usijizuie kwa kusema aah mimi siwezi tena.
Acha
kuishi kwa ndoto na kujisemea mimi mbona maisha yako ya hivivi tu siku zote,
wewee, utakuwa unajidanganya na kujipoteza. Unao utajiri mkubwa ndani yako,
jenga subira wakati utajiri huo unaousubiri kufumuka mbeleni unakuja.
Wewe
ni binadamu na unaweza kubadailika na kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha
yako na kwa wale ambao unao wazunguka kwenye maisha yako wakati wote, yote hayo
yanatokea kwa sababu wewe ni binadamu.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.