Feb 19, 2018
Mambo Ambayo Huwezi Kuyakwepa Unapotafuta Mafanikio Yako.
Katika
safari ya mafanikio, yapo mambo ambayo huwezi kuyakwepa hata ufanyaje, mambo
hayo ni lazima ukutane nayo. Kuna wakati mambo hayo yanakuwa yanakatisha tamaa
sana usipokuwa makini yanaweza kukuangusha. Leo nataka tuyazungumzie mambo haya
ambayo huwezi kuyakwepa kwenye safari ya mafanikio yako;-
1. Kupoteza baadhi ya marafiki.
Unapatafuta
mafanikio yako kuna wakati unatapoteza marafiki zako ambao unaona hamuendani.
Sio marafiki wote mtaokaoweza kwenda nao kwenye safari ya mafanikio. Kuna marafiki
utawapoteza kwa sababu hawakusaidii kuweza kufikia kule unakotaka. Inapotekea
hivyo usishangae huo ndio ukweli, hakuna namna
zaidi ya kuachana nao.
2. Kufikiri kama unachanganyikiwa.
Kuna
wakati vitu vinakua vingi sna kichwani mpaka unaoana kicwa kinawaka moto au
unahisi kama vile unachanganyikiwa. Hizi ni hali zinatokea sana kwa mtu yeyote ambaye
ni mtafuta mafanikio. Ukiona kila wakati
umetulia na kichwa hakikusumbui, utambue bado hujafikia hatua hiyo ya kutafuta
mafanikio yako kwa kasi.
3. Kupatwa na maumivu.
Huwezi
kukwepa kukutana na maumivvu unapotafuta mafanikio yako. Kuna wakati utakutana
na maumivu ya kukataliwa, kuna wakati utakutana na maumivu ya kupata hasara.
Huu ni mojawapo ya mlolongo mchache wa maumivu ambayo unaweza kukutana nayo
kwenye safari ya kutafuta mafanikio
yako.
4. Kupoteza pesa.
Upo
wakati utafika utapoteza hata pesa zako ikiwa kama hujapoteza. Hilo ni jambo
mojawapo pia ambalo unatakiwa ulijue kwamba lipo kwenye safari ya mafanikio
yako. Unapopoteza pesa zako, tafadhari
usikate tamaa, hiyo ni dalili tosha ya mafanikio mengine makubwa yanakuja
kwako, kikubwa ongeza juhudi na tafuta pesa zingine.
5. Kukatishwa tamaa.
Kipo
kipindi wakati unatafuta mafanikio yako utakatishwa tamaa na rafiki zako, ndugu
zako na hata mumeo au mkeo kwamba ndoto hizo haiwezekani kwako kuweza kuzifikia.
Yote hayo unapaswa kuyajua kwamba yanaweza yakakutokea na hutakiwi kukata
tamaa, unatakiwa ujue hali hiyo ipo na unatakiwa kupambana nayo.
6. Utakuwa unajitilia shaka sana.
Pia ni
lazima utafika wakati utakuwa unajitilia shaka kwa kuona kwamba huwezi kitu. Kila
unapoangalia ndoto zako na kuona ni kubwa unakuwa unawaza sana kwamba ‘kweli nitaweza hili.’ Lakini hapa naomba
nikwambie unaweza, haijalishi umejitilia shaka mara elfu moja lakini unao uwezo
wa kuweza kusonga mbele kwenye maisha yako.
7. Utakosolewa sana.
Wakati
unatafuta mafanikio kuna muda utafika kila unachotaka kufanya unakosolewa na
wengine kwamba kitu hicho hakifai. Usipokuwa makini utakuwa unaacha kila kitu kwa
kusikiliza maneno ya watu wa nje. Kikubwa hapa iamini ndoto yako na usisikilize
mtu kwamba huwezi hili au lile, wewe jiamini na fanya.
8. Utashambuliwa bila sababu.
Kuna
watu watajitokeza watu kukutuhumu wewe ni mtu wa kudhulumu, au wewe pesa zako
unatafuta kwa njia ambazo sio halali. Na
watakwambia maneno mengine mengi, lakini ukweli utakuwa unaujua wewe ni kipi
ambacho unakifanya, kwa hiyo unatakiwa usimame imara pasipo kuteteleka kwa
kusikiliza maneno ya watu.
Haya
kwa kifupi ni baadhi ya mambo ambayo ni lazima ukutane nayo katika safari yako
ya mafanikio. Mambo haya yanapojitokeza kwako yasikukatishe tamaa hata kidogo
bali yakupe chachu ya wewe kuweza kusonga mbele. Watu wenye mafanikio
wanakabiliana sana na mambo kama haya na mwisho lakini hushinda.
Fanyia
kazi mambo haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Nakukumbusha
pia, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.